CHADEMA mnakengeuka, mmekuwa kama mmepata kiwewe cha kisiasa

Kadiri mtananage wa uchaguzi mkuu unavyokaribia Chama kikuu cha upinzani nchini kimekumbwa na kiwewe cha kisiasa. Kimekuwa hakina muelekeo wala hoja za msingi kupambana na CCM.

Utasikia kila kukicha wanaibua hoja ambazo hazina mashiko wala mvuto. Kwa ufupi wanaweweseka na kutapatapa. Kila kukicha wanazua uzushi wa kitoto ambao hautawasaidia kisiasa.

Mfano hivi karibuni walivalia njuga suala la CCM kupokezana vijiti kwa wagombea urais kwa kumuachia aliyepo madaralani kuendelea kupeperusha bendera ya CCM bila kupingwa. Wao wanaona kama ni ishu ambayo itawabeba kisiasa wakati ni upuuzi.

Kwani hawajui kuwa Customs huwa zinakuwa kama sheria? Ndio maana hata kwenye jamii zetu tuna customary laws. Hizi ni sheria ambazo hutokana na mila na desturi.

Kwa hiyo kama CCM desturi yao kwa miaka zaidi ya 36 ni kuachiana kijiti kila baada ya miaka kumi, Chadema nyie hilo linawahusu nini? Sababu imeshakuwa kama taratibu yao.

Hapa Tanzania mtu akiua na akakutwa na hatia hukumu yake ni kifo. Lakini sasa imekuwa desturi kila rais akiingia madarakani hanyongi mtu aliyehukumiwa kifo. Japokuwa sheria inataka anyongwe.

Sasa limekuja suala la mswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali ya mwaka 2020. Moja ya sheria inayofanyiwa mabadiliko ni Basic rights and duties enforcement Act. Sasa wameanza kupotosha eti CCM wanajitungia sheria Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na spika hawatashikiwa. Jambo ambalo ni uongo na uzushi.

Mabadiliko haya yanataka mtu akitaka kufungua kesi dhidi ya viongozi hawa awe na hati ya kiapo kuonyesha namna haki yake ilivyovunjwa na namna alivyoathirika.

Pia atapofungua kesi mtu atafungua kesi dhidi ya viongozi hawa kama watafanya makosa wanapotekeleza majukumu yao na atafungua dhidi ya mwanasheria mkuu. Jambo ambalo ni la kawaida.

Chadema acheni kupaniki tunajua mna wakati mgumu sana. Lakini kubalini yaishe. Mliharibu wenyewe kwa hiyo tulieni mnyolewe.

Hapa chini someni vizuri kama hairuhusiwi kumshitaki Rais na viongozi wengine.

Hivi umeandika huku ukikumbuka kuwa kuna marufuku haramu iliyotolewa ili kuviminya vyama vya ushindani wa kisiasa kuendesha shughuli zake za kihalali, huku ikitoa upendeleo wa kipekee kwa chama tawala?
 
Kadiri mtananage wa uchaguzi mkuu unavyokaribia Chama kikuu cha upinzani nchini kimekumbwa na kiwewe cha kisiasa. Kimekuwa hakina muelekeo wala hoja za msingi kupambana na CCM.

Utasikia kila kukicha wanaibua hoja ambazo hazina mashiko wala mvuto. Kwa ufupi wanaweweseka na kutapatapa. Kila kukicha wanazua uzushi wa kitoto ambao hautawasaidia kisiasa.

Mfano hivi karibuni walivalia njuga suala la CCM kupokezana vijiti kwa wagombea urais kwa kumuachia aliyepo madaralani kuendelea kupeperusha bendera ya CCM bila kupingwa. Wao wanaona kama ni ishu ambayo itawabeba kisiasa wakati ni upuuzi.

Kwani hawajui kuwa Customs huwa zinakuwa kama sheria? Ndio maana hata kwenye jamii zetu tuna customary laws. Hizi ni sheria ambazo hutokana na mila na desturi.

Kwa hiyo kama CCM desturi yao kwa miaka zaidi ya 36 ni kuachiana kijiti kila baada ya miaka kumi, Chadema nyie hilo linawahusu nini? Sababu imeshakuwa kama taratibu yao.

Hapa Tanzania mtu akiua na akakutwa na hatia hukumu yake ni kifo. Lakini sasa imekuwa desturi kila rais akiingia madarakani hanyongi mtu aliyehukumiwa kifo. Japokuwa sheria inataka anyongwe.

Sasa limekuja suala la mswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali ya mwaka 2020. Moja ya sheria inayofanyiwa mabadiliko ni Basic rights and duties enforcement Act. Sasa wameanza kupotosha eti CCM wanajitungia sheria Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na spika hawatashikiwa. Jambo ambalo ni uongo na uzushi.

Mabadiliko haya yanataka mtu akitaka kufungua kesi dhidi ya viongozi hawa awe na hati ya kiapo kuonyesha namna haki yake ilivyovunjwa na namna alivyoathirika.

Pia atapofungua kesi mtu atafungua kesi dhidi ya viongozi hawa kama watafanya makosa wanapotekeleza majukumu yao na atafungua dhidi ya mwanasheria mkuu. Jambo ambalo ni la kawaida.

Chadema acheni kupaniki tunajua mna wakati mgumu sana. Lakini kubalini yaishe. Mliharibu wenyewe kwa hiyo tulieni mnyolewe.

Hapa chini someni vizuri kama hairuhusiwi kumshitaki Rais na viongozi wengine.

Akili zenu wote mnafanana na bawana yule
 
Back
Top Bottom