CHADEMA mnaijua mbinu hii hatari ya CCM ya kuviua vyama vikuu vya upinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mnaijua mbinu hii hatari ya CCM ya kuviua vyama vikuu vya upinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Dec 18, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Miaka ya 2000 CUF Ndiyo kilikuwa chama kikuu cha upinzani hapa nchini. Wakati huo mimi nilikuwa shabiki mkubwa sana wa siasa nikikaimu nafasi ya katibu wa wilaya ya Dodoma mjini. Nakumbuka tulikuwa na nguvu kubwa tu kisiasa hali iliyosababisha chama kuwa tishio kwa chama tawala. Yapo mambo mengi ya kusimulia ambayo ndiyo chanzo cha kuporomoka kwa umaarufu wa CUF lakini hapa ntaeleza kwa ufupi tu moja ya mbinu kubwa ya CCM ambayo unaweza usiitilie maanani lakini hutumika sana na huleta usumbufu na madhara makubwa hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi. Kuna mapandikizi wa CCM mbao huingizwa katika chama pinzani kinachowika kuanzia ngazi za chini kabisa za uongozi katika chama. Hawa huingia katika matawi, kata na hata wilaya. Huhakikisha wanafanya kazi za chama kwa nguvu kubwa kiasi cha kuaminiwa na pengine huwa wafadhiri wa chama kiasi hufikia kuaminiwa mpaka kupata uongozi mbalimbali. Kinachofuata baada ya hapo ni kuvujisha siri na mikakati ya chama. Kuhakikisha kuwa wagombea wa ngazi za chini za uongozi mfano wagombea wa uenyeviti wa mitaa, vitongoji, vijiji na hata madiwani wanakosa sifa za kushiriki katika chaguzi kwa kuchelewesha fomu zao kwa makusudi. Kwa mfano, fomu ya mgombea inatakiwa ipite kwake kwa ajili ya kutiwa mihuri ya chama nk. Anaweza kuichelewesha kwa makusudi mpaka muda wa mwisho wa kurejesha fomu kwa tume ya uchaguzi unapita. Hushawishi kuwekwa watu wasiokubalika na wananchi ili kugombea nafasi mbali mbali. Kupandikiza wagombea wao ambao ni wana CCM ambapo matokeo yake hujitoa kabla ya uchaguzi na kusababisha chama kukosa mgombea.. Hawa ni watu hatari kwa sababu ngazi za chini za chama ndizo zipo karibu zaidi na wananchi. Huko ndiko chimbuko la udhaifu wa chama linapoanzia. Wengine huanzisha migogoro ya makusudi kwa ajili ya kuwagawa wanachama. Hii hufanyika baada ya mbinu zote kushindikana. Kwa hivi sasa CHADEMA ndiyo chama chenye ubavu wa kuitingisha CCM na serikali yake. Macho yao wasiyaelekeze ngazi za juu tu. Ngazi za chini nako mapandikizi wa CCM hupenyezwa kwa wingi. Siasa si raha, ni karaha tu hasa ukiwa kiongozi.
   
 2. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Twa twa twaaa! Umenikumbusha mbali. Kulikuwa na mtu anaitwa Chite, na Ndabwe. Hawa walikuwa wanatuhumiwa kuchukua hela kwa malecela
   
 3. d

  dada jane JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Safari hii tutabanana nao hadi penalt. Ndio maana wanafiki wameanza kuumbuliwa. Mbaya zaidi cdm inaungwa mkono na watz wote waliochoka kunyanyaswa na sio Mbowe na Slaa tu. Hao ni akina Musa na Harun kazi yao ni kuwatoa kwa mfalme mwenye moyo mgumu. Subiri yale mapigo 7 yapite. Na saa hizi tayari yamepita_ ___ bado ___.
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ebwanaaa! Mwenzangu u nani wewe, hebu jitambulishe. Ni PM tu tutambuane mtu wangu.
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Teh,teh,teh!Namkumbuka Chite mzee wa kigugumizi.Halafu baadae zikaja enzi za mzee Amani unamkumbuka?Ni kweli CUF wakati ule ilikuwa na nguvu.Nakumbuka hadi bosi mmoja wa maafande akapiga marufuku watu kutumia mafuso kusafirishia abiria.Sasa hivi naona mambo yako doroooo.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Si anaitwa kibwenga?
   
 7. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kumbukumbu zangu hazina jina hili. Ni utaratibu huu wa kuficha majina halisi.
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu hii naikubali'chadema wajitahidi sana kupata watu wasio na background za ki ccm'kuna mapandikizi tayari yapo kazini'shughuli ya kuitoa ccm sio mchezo
   
 9. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Thanks for this food of thought
   
Loading...