Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Sasa Mkuu, CHADEMA tayari wamewatimua hawa covid-19, siyo wanachama wao. Kwa mujibu wa Katiba yetu, hao siyo wabunge tena. Kwaiyo. Mambo ya covid-19 usiwaulize CHADEMA!Wanabodi.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa Chadema ‘inayohesabiwa’ kuwa na wabunge 20 imepata Sh109.68 milioni, ACT Wazalendo yenye wanne kimepata Sh14 milioni na CUF yenye mbunge mmoja ikipata Sh5.7 milioni za Ruzuku ambayo iliingizwa kwenye account za vyama Nov. 2020.
Mbowe, hili suala mbona kwenye hotuba yako haukulisema umekaa kimya nawashheshimu sana Chadema kwa misimamo yao wameenda mbali zaidi na kususia chaguzi zote mpaka kuwepo na Tume Huru.
Hii ruzuku mnayochukua kutokana na wakina Halima Mdee ni ya nini, wananchi wapenda haki wanataka kufahamu hili jambo.
Kwa mujibu wa taratibu za ruzuku, chama kinakokotolewa ruzuku kutokana na sifa mbalimbali ikiwemo idadi ya kura za urais na idadi ya wabunge, na sifa zingine. Tena hii ya idadi ya kura za urais ndiyo inabeba asilimia kubwa zaidi. CHADEMA ilipewa kura za urais asilimia 13. Nasema walizopewa, kwa kuwa kura zao kihalali zilikuwa nyingi zaidi.
CHADEMA tayari wametekeleza wanayohitajika kufanya kwa mujibu wa taratibu. Si jukumu la CHADEMA kuanza kujiuliza fedha wanayopata kutokana na covid-19 ni ngapi, kati ya sifa ambazo wanazo tayari.
Ni kama tu unawekewa mshahara mkubwa kuliko stahili zako. Wala huhitaji kuhangaika. Wenyewe watafanya makato na kurekebisha inavyotakiwa. Acheni kupotosha mambo