CHADEMA mnachanganya Wananchi, mnataka Tume Huru au Katiba Mpya?

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,924
32,336
Wanaukumbi.

Je umeshawahi kujiuliza ni kwa nini CHADEMA hawajawahi kudai Katiba Mpya kipindi cha takribani miaka 6 ya Mhe. Jiwe Madarakani?
Rais, SuluhuSamia, yupo madarakani miezi 3 tu, chokochoko zimeanza!

Kitendo cha kupigania Tume Huru ya Uchaguzi wakati huo huo kupigania Katiba Mpya kumeanza kuwafanya wananchi wadhani kuwa mapambano halisi ya CHADEMA ni kupigania Tume Huru ya Uchaguzi ili waingie madarakani kwa kujifanya wanadai na Katiba Mpya ili kuzuga umma wa watanzania.

Kama ni hivyo kwa nini CHADEMA wamegawanya majukumu:

1. Bavicha Katiba Mpya

2. BAWACHA Tume Huru ya Uchaguzi

Kama bila Katiba Mpya hakuna Tume Huru Uchaguzi basi kwa sasa wadai Katiba tu, harakati za Tume Huru ya Uchaguzi zije wakishapata Katiba Mpya!
 
Wengine tunataka katiba mpya hayo mambo ya tume huru watajua wanasiasa

Sisi tunataka katiba iliyotokana na maoni ya Watanzania over!
 
Wengine tunataka katiba mpya hayo mambo ya tume huru watajua wanasiasa

Sisi tunataka katiba iliyotokana na maoni ya Watanzania over!
 
Wacha kupotosha, Chadema waliidai Katiba Mpya toka enzi za Magufuli, usitake kuchezea akili za watu ionekane Samia anaonewa kwa sababu ya jinsia, dini, wala kule atokapo.

Kuhusu Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi na vingine vyote vinakwenda sambamba, hiyo Tume Huru na muundo wake vyote vitaainishwa ndani ya Katiba Mpya, viraka kwenye katiba sasa inatosha, uwe mwisho.
 
👌
 
Back
Top Bottom