CHADEMA mmemsahau Freeman Mbowe, mmekalia kuongeza mafuta CCM

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,551
11,882
Ninaomba kwenda kwenye mada moja kwa moja.

Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Aikaeli Mbowe yuko rumande kwa muda sasa.Hii ni kutokana na kesi inayomabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria za nchi hii.

Na kwa muda mrefu jukwaa la social media nchini, lilitawaliwa na wanachama,wafuasi wa chadema pamoja na wanaharakati wakishinikiza kwa namna moja au ingine, kuachiwa kwa Mbowe.

Hii imebadilika ghafla baada ya CCM kuingia katika misukosuko na makada wake.
Jambo ambalo limepelekea Spika Ndugai kujiuzuru.

Ghafla CHADEMA wamenyamaza kuhusu Mbowe na sasa wao ndio wapiga zumari wakuu wa huu mgogoro wa CCM.

Ukiwasikia viongozi waandamizi,kina Lema,Msigwa,Heche,Lissu iwe huko the Space kwa sarungi au twitter nk.

Huwasikii kumuongelea kiongozi wao na hatima yake.bali wamehamia CCM kimwili na kimawazo hadi kufikia baadhi yao kupendekeza na jina la spika wanaemtaka, (msigwa ali tweet kumpendekeza Chenge)kabla ya Lema kuingilia kumwambia Msigwa aifute hiyo Tweet yake.

Wanayo maoni meengi kuichambu migogoro ya CCM kiasi kwamba tunashindwa kuwaelewa.Nini hasa ajenda yao rasmi.

Baraza jipya limetangazwa nao wamehamia seat za mbele, sio kwa maoni na ushauri wa ubora au udhaifu wa baraza, wao wamejikita kuwaandama mahasimu wao kisiasa zaidi huku wakihanikiza dalili za visasi zaidi.

Je kwa mfumo huo wanaotuonyesha.
Tuwaelewe chadema katika muktada upi haswa?

Ulipaji visasi na ushangiliaji wa minyukano huko CCM, au mngeutumia muda huu kuwaelimisha wananchi uzito wa giza lililoko mbele yao?

Kuna mfumko wa bei nchini kwa sasa, kuliko hata majirani zetu wanaotumia bandari yetu kwa kuingiza mahitaji yao yote.

Na mfumko wa bei za vyakula ambavyo kiuhalisia sisi ni wazalishaji wakubwa wa chakula na mazao ya nyama katika ukanda huu.

Hilo la uzuri wa mikopo na madhara yake siku za usoni pia mlipaswa kama chama makimi, kutuonyesha watanzania tunasimama wapi kati ya pande mbili.

Lakini mmekaa kimya, pamoja na waziri kutoa lugha za kejeli kwamba,

" hakuna mtanzania atagongewa mlango kudaiwa deni la taifa."

Huku akijua wananchi ndio wahanga wakubwa wa hiyo mikopo kupitia ulipaji kodi zetu.pamoja na upandaji wa gharama za maisha pale riba zitakapoielemea serikali.

Pia kuna Tozo za miamala ya kifedha zilizoanzishwa na ambazo zinakuwa rungu la kichwa kwa mwananchi na kila mjasiliamali nchini.

Ndugai alihoji hilo....kwamba kama bunge lilipisha Tozo kwa mahsusi kutumika kwenye ujenzi wa madarsa na miundombinu ya barabara za TARURA nchini. Huu mkopo wa 1 3 trilioni nao umeelekezwa huko.

Je ni kwa namba gani tutaweza kuambiwa fungu hili la Tozo ambalo linaendelea kukusanywa kila uchao tracking ya matumizi yake nani anatuambia au tunafunikwa macho huku wajanja fulani wakineemeka?

Pamoja na kuambiwa na waziri kauli zenye ukakasi kwamba

"asiyetaka Tozo, ahamie Burundi"

Wapinzani nchi hii mna jukumu la kusimama na kuwatetea wananchi. Badala yake nyinyi mnapigania yale mnayoona yanawatengenezea mazingira mazuri ya kupata vyeo na kujineemesha.

Ndio mnaweka mbele katiba mpya na mnavaa miwani ya mbao kuhusu yale yanayotendeka kwa sasa ambayo hayahitaji katiba mpya nayo ni kama.

Mifumko ya bei.
Tozo za miamala.
Tatizo la kutengenezwa kuhusu ukosefu wa nishati ya umeme .kwa makusudi ya walafi wachache,wenye tamaa binafsi.

Mko wapi?

Nimetoa yangu ya moyoni kama mtanzania mpenda haki.
 
CHADEMA wana AKILI kuliko Unavyodhani.

Suala la Mwenyekiti Wao ndio KIPAU MBELE chao kwa kuwa wewe Sio sehemu ya Chadema una Haki kuwaza kadili Akili zako zinavyokudanganya

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ninyi CCM mmesahau kumkanya mwenyekiti wenu kuwa aache kuwa tapeli anaelaghai Watanzania badala yake mnahangaika na Chadema ambayo inatafuta uhuru pamoja na maendeleo ya watu:

Kwenye kampeni👇😁😁😁
Baada ya kuingia Ikulu👇🐒🐒🐒
 
Back
Top Bottom