Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau amani iwe kwenu.
Ni dhahiri shahiri sasa kwamba Lowasa amejiweka pembeni na siasa za CHADEMA. Lipo fukuto la chini kwa chini ndani ya chama hicho hususan juu ya hatma ya mwanasiasa Mkongwe, Edward Lowasa ambaye amejitangaza kuwa ndiye atakuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2020. Inaelezwa kuwa chanzo cha fukuto hilo ni kutokana na uamuzi wa mwanasiasa huyo kujitangaza kuwa atagombea tena Urais kupitia CHADEMA licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa Oktoba 2015 ijapokuwa aliwahakikishia kuwa atashinda uchaguzi kabla ya SAA NNE ASUBUHI ya Oktoba 25.
Wapo wanasiasa waandamizi wa chama hicho ambao wanajipambanua kama CHADEMA ASILIA ambao wameonesha msimamo wao wa kutoruhusu chama hicho kuingia tena kwenye aibu ya kushindwa uchaguzi wa 2020 kwa sababu tu kimemsimamisha mtu ambaye Watanzania walio wengi hawamkubali (Lowasa). Wanasiasa hao wanaongozwa na Tundu Lissu, Wilfred Lwakatare, John Mnyika na Joseph Selasini. Wanasiasa hao wameapa kuwa ikiwa Mbowe ataendelea kumng'ang'ania Lowasa awe mgombea Urais wao, watafanya maamuzi magumu ambayo hata hivyo hawakuyabainisha.
Wanasema kuwa kwa uzoefu walioupata kwenye uchaguzi wa 2015, Lowasa hana uwezo wa kujenga hoja shawishi majukwaani na hivyo ni vigumu kwake kuweza kushindana tena na Rais Magufuli ambaye anaonekana kuungwa mkono zaidi na wananchi wengi wa kawaida ambao ndio wapiga kura. Tundu Lissu mathalan alisema kuwa ikiwa kuna haja ya CHADEMA kusimamisha mgombea Urais kutoka miongoni mwa makada waliotoka CCM, basi ni mara 100 wakamsimamisha Sumaye ambaye ana uwezo wa kujenga hoja kuliko kumchagua mgombea ambaye ni "BUBU au KIBOGOYO"
Katika kuonesha kuwa kundi hilo linasimamia kile wanachokiamini, walikataa mwaliko wa Mbowe ambaye aliwaalika kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Edward Lowasa nyumbani kwake Dodoma Ijumaa tarehe 29 Aprili 2016. Wanasiasa hao walifanikiwa pia kuwashawishi wabunge wengine ambapo walitoa udhuru wa kutohudhuria kikao hicho na hivyo hakikufanyika kama ilivyopangwa. Baada ya aibu hiyo ambayo Mbowe na Lowasa waliipata, Lowasa aliamua kurejea Dar es Salaam kwa aibu huku akiapa kutojihusisha tena na siasa za CHADEMA mpaka watakapomuomba radhi.
Katika kuonesha kuwa kundi hilo linaonekana kufanikiwa, Freeman Mbowe anaonekana kukubaliana na mapendelezo yao ya kumjenga Sumaye ili aje kuwa mgombea Urais mwaka 2020 badala ya Lowasa. Tayari Mbowe amemteua Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati kuu hali inayotafsiriwa kuwa kumkurubisha mwanasiasa huyo na mambo ya "JIKONI" ya CHADEMA.
Je baada ya haya yanayoendelea ndani ya CHADEMA, nini hatma ya Lowasa kisiasa? Tusubiri wakati ndio utaamua.
Nawasilisha