CHADEMA mmekua, mnapendwa, jiandaeni kujizatiti na mitikisiko jinsi tunavyoelekea 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mmekua, mnapendwa, jiandaeni kujizatiti na mitikisiko jinsi tunavyoelekea 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jul 26, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwamba sasa vita au nia ya kugombea urais imekuwa gumzo si ndani ya CCM bali nje ya CCM. Hapo tumefika pazuri.

  Mwaka 2005, kulikuwa na mnyukano mkali ndani ya CCM. Mimi nilisafiri hadi Dodoma wiki ya mwisho ya vikao vya uteuzi wa wagombea urais mwaka ule kwa CCM.

  Eh Bwana, makovu ya ile vita sidhani kama yataisha mapema. Jakaya Kikwete alipotangazwa kwamba ameshinda kuwa mgombea urais wa CCM kila mtu alijua sasa tumepata Rais. Kwamba humpendi Jakaya, huipendi CCM basi jua kwamba liwalo na liwe Jakaya Kikwete atakuwa Rais wako.

  Nilitoka Dodoma baada ya uteuzi ule nikapita D’Salaam kwa kaka yangu nikakaa kwa wiki mbili. Ana watoto wadogo watatu. TV ikiwashwa na Kikwete akatokea basi watoto wote wanashangilia “Njooni tumuone Kikwete”.

  Askofu Method Kilaini alipoulizwa kuhusu wagombea urais wa 2005 hakusita kumtaja Kikwete kwamba ni “Chaguo la Mungu”.

  Hii ni hali ya mwaka 2005 kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mgombea urais kupitia CCM. Hakuna aliyekuwa na hamu kujua wapinzani watamuweka nani kwani ilikuwa ni wazi mpinzani lazima awe msindikizaji tu.

  Hata kama ndani chama kama CHADEMA kungekuwa na mnyukano wa kugombea urais basi kila mmoja angwaona ni wehu hawa maana wanagombea usindikizaji. Hakuna ambaye angewajali.

  Hata hadi May 2010, hakukuwa na dalili za ugomvi wa kugombea uteuzi ndani ya CCM na ndani ya CHADEMA. Kila mmoja alikuwa anajua Kikwete anapeta tu tena safari hii (2010).

  Askofu Method Kilaini alipoulizwa June 2010 kwamba ni nani anaelekea kushinda uchaguzi safari hii hakurudia kauli yake ya “Cahguo la Mungu”. Bali alieleza kwamba Kikwete atashinda tena kwa sababu baadhi ya washindani wake wa mwaka 2005 wamekata tama na kuchukua fomu za Ubunge.

  Askofu Kilaini alijibu hivyo kwa sababu hadi dakika anahojiwa hiyo Wilbrod Slaa na Freeman Mbowe walishatangaza nia ya kuchukua form za Ubunge.

  Narudia hadi June 2010 hakukuwa na vita ya Urais kupitia chama kingine. Vita pekee iliyokuwepo ni kujitayarisha na ugombea ndani ya CCM kwa mwaka 2015. Kwamba uchaguzi wa 2010 uende lakini wagombea wa 2015 wanajua wanalolifanya kwamba JK akitoka wanasubiri ulaini wa 2015.

  Leo hali ni tofauti. Shibuda katangaza kwamba atagombea kupitia CHADEMA. Zitto anatajwa. Wilbrod Slaa anatajwa. Na kufikia 2014 watatajwa wengi tu.

  Wakitajwa TLP, NCCR wala haina shida. Vipya vinaanzishwa wala haina shida. Shida sasa ni CHADEMA. CHADEMA imefika mahala sasa hata ukitaja wagombea ndani ya CCM hakuna anayejishughulisha bali sasa kila mmoja anaangalia ni nani atajitokeza ndani ya CHADEMA.

  Zamani mtu akisikika kuwa anatangaz ania ya urais basi hata wakificha jina la chama utajua ni CCM. Leo hali ni tofauti. Vita ile sasa ni kama imehamia CHADEMA.

  Maoni yangu ni nini? Maoni yangu ni kwamba hata kama CCM inadhani inafaidika kwa vita hii ya ndani ya CHADEMA basi tafakari nzuri ni kwamba CCM yenyewe ijijue kwamba hata CHADEMA watwangane vilivyo huo mtwangano ni kwamba watu wameishaachana na CCM. Kwamba Rais bora sasa anaweza kutoka nje ya CCM. CCM hawakuzoea vita ya urais ipiganiwe kwenye vyama vingine na magazeti yakajaza habari na nchi ikatetemeka. Sasa, wameona. Hivyo, mimi vita hii ni nzuri tu kwa CHADEMA.


  Ninaamini ubunge ndiyo sijui itakuwaje. Mwaka 2010 CHADEMA ilishindwa kusimamisha wabunge kwenye baadhi ya majimbo. Sasa kama urais umeshaanza kugombewa leo basi ubunge ndani ya CHADEMA sasa hivi ni gharama kuliko mahala popote. Gharama kwa maana ya kwamba kama unataka kugombea kupitia CHADEMA basi inawezekana mwaka huu ni wa mwisho kwako na ninaamini kufikia January 2013 nafasi za ubunge zitakoseana ndani ya CHADEMA.

  Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba wao ni chama pendwa. Sasa kila mmoja anaona wazi mgombea urais kupitia CHADEMA ni mtu wa muhimu katika nchi hii. Kila mmoja anataka kugombea kupitia CHADEMA.

  CHADEMA sasa lzima mjifunze kukubali ambayo hamkutarajia. Hayo ni pamoja na kujitokeza kwa wengi kuomba uanachama na uongozi. Lakini pia mkubali kwamba maadam mnapendwa na wananchi na mna asilimia kubwa ya kuchukua dola basi mzoee sasa hali ya sasa. Wagombea urais ndani ya CHADEMA watakuwa ni hot cake na jamii inawamulika. Wagombea ubunge au udiwani mambo ni yaleyale.

  Cha msingi mjikite kiasi kwamba hasira za wagombea kukosa kuteuliwa zikiharibu chama. Hiki mnatakiwa kujiandaa nacho. Lakini msibweteke kwamba watu wataach kuonyesha spiration wakati CHADEMA ni chama pendwa na kila mmoja anakiangalia kwa jicho la 2015.


  Kila la heri CHADEMA, ndiyo ukubwa huo.
   
 2. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0

  I'm thrilled with your explanations!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hata mimi, ingawa siko Simplistic:-
   
 4. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  vurugu kama hizo zinatafsir mbalmbal,ao viongoz baadh wanatamaa ya madaraka sawa,ila muweke mbelemaslah yetu wananchi
   
Loading...