Ndikwega
R I P
- Feb 1, 2012
- 5,979
- 5,524
Nawapongeza saana CHADEMA kwa Juhudi zenu binafsi katika kutetea wananchi wanyonge wa Taifa hili Tanzania. Yoote haya tunayashuhudia sababu ni Juhudi zenu.
Mnapambana na Chama Kikongwe CCM, wenzenu wengi mliyoanza nao safari ya Ukombozi wa Kifikra pale 1992 walishajikatia tamaa na hakuna ndoto tena ya kushika dola.
Ninyi pamoja na kuwa na Rasilimali kidogo yaani Pesa na Vitega uchumi kulinganisha CCM ambao muda mwingine wanatumia hata rasilimali za serikali bado mmekaza na kudhihirisha hili kuwa mnaogopwa na CCM ndiyo maana vitisho haviishi juu yenu kila uchao kwa kutumia vyombo vya dola.
Jifunzeni kwa Wenzenu Afrika Kusini hakika wameiweza ANC hivyo hakuna kuvunjika moyo na Vitisho vya Watawala hawa wasiyoitakia mema nchi yetu.
Ninachowaomba Viongozi wa Chadema igeni mfano wa Lissu, katika swala la kusimamia Kweli. Katika Ukombozi wowote lazima pawe na maumivu, wachache wataumia kwa faida ya wengi!
Niwatakie mapambano mema, mkikaa kimya kwa udhalimu huu hakika mtakuwa hakuna haja ya kuitwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Mungu awatangulie katika Mapambano yenu ya kumsaidia Mnyonge wa Tanzania asiye na Sauti ili muwe Sauti yake.