fasiliteta
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 2,165
- 3,655
Habari za muda huu wakuu.
Bila kuwachosha niende moja kwa moja katika maudhui ya uzi huu.
Hivi karibuni tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia kwa kinachoitwa democracy katika chama kikuu cha upinzani Tanzania (CHADEMA) kupitia chaguzi zake mbalimbali hasa hizi nafasi za uenyekiti.
Kiukweli ni hatua nzuri sana katika ustawi wa democracy nchini pale chama kinapojali maoni/mapendekezo/Machaguo ya wanachama na wananchi wao.
Nipende kutoa pongezi kwa dhati kabisa kwa chama hiki huku nikitazama nafasi ya mwenyekiti wa chama ngazi ya Taifa ambapo Mh. Mbowe anagombea kwa awamu ya nne katika historia ya chama hicho.
Huku mtaani watu wamekuwa na maoni tofauti katika hii nafasi nyeti kwa chama huku wakiendelea kujiuliza sana hili suala linawezekanaje kwa mwenyekiti kugombea tena licha ya kuhodhi madaraka ya uenyekiti muda mrefu?
Majibu ya wanachama husika yamekuwa ni mengi sana huku wakijitapa kuwa Mh.mbowe ndiye mtu sahihi na aendelee kuwavusha daraja kutokana na kukitendea haki kiti chake kwa muda aliokaa hivyo hawaoni haja ya kutafuta mbadala zaidi ya yeye kuendelea kukitumikia chama kwa nafasi hiyo.
Sisi kama wananchi hatuna shaka na hilo kutokana na baadhi ya sababu hizo. Zaidi tumejifunza kitu kumbe uwezekano wa democracy kutumika pindi tu mtu anapofanya vizuri na hivyo kupewa nafasi ya kuongoza mihula zaidi ya miwili kama wengine tulivyojiaminisha ndio mihula ya kiuongozi kidemokrasia inawezekana.
Swali kwenu wana CHADEMA je wale walioona mazuri ya Rais wao mchapakazi Mh.Dr John Pombe Magufuli walikuwa sahihi kudai aongezewe muda wa kukaa madarakani kwa kutumia democracy hiyo hiyo mnayoifanya kwa sasa ndani ya Chama?
Je, kuna ubaya tukamuomba Mheshimiwa Rais naye aendelee kuchapa kazi kwa vipindi vingi zaidi baada ya kuona matunda yake kwa muda mfupi?
Je! CHADEMA sasa wamegundua Democracy inaishi na si ya kubezwa?Maana kumbe yawezekana kama alivyoweza na anavyoendelea kuweza Mh. Mbowe.
Mwisho niwaombe CHADEMA na wanachama wake, kuna kipengele katika democracy kinaelezea nguvu ya POLITICAL TOLERANCE au kiswahili UVUMILIVU KATIKA NYANJA ZA SIASA.
Nyinyi mmeweza sasa na bila shaka mnaenda kumsimika Mh. Mbowe kwa muhula wa nne.
Muda ukifika kwa wengine basi mnyamaze kimya na muache DEMOCRACY iendelee kuishi.
Msumeno hukata pote pote, ni zamu yenu sasa na zamu yao ikifika basi ndio Democracy hiyo wajomba.