CHADEMA, mmeisoma hii? Wanasema uchaguzi ni maandalizi!

chadema mnaikumbuka hii kitu?naona kama mmeanza kuicheza ngoma ya ccm kwa wiki takribani mbili mpaka leo ni maongezi ya vikao vya ccm vilivyokipatia viongozi chama hicho chini ya jk kama mwenyekiti,hakuna anaemzungumzia slaa,zitto wala uchaguzi wa viongozi wa chadema,watu wako busy na kina lowassa,mwigulu,karume na jk
 
Tatizo letu tunataka kusolve simulteneous equations kwa kutumia jia ileile wakati kuna approach zaidi ya mbili kwa wanamahesabu watanielewa.Usiwalazimishe CDM watumie approach ya ccm.Mbona wao ccm hatujamsikia katibu mkuu wa UVCCM akizunguka mikoani kama anavyofanya HECHE wa chadema???? kwani anachofanya heche hakina impact ktk siasa za tz hasa kuhusu kuimarisha chama na kupata umaarufu???
CDM tunawaona walivyopbadilisha siasa za Tanzania leo ukielekea mrogoro njiani unakutana na bendera za cdm barabarani tofauti na zamani, hayo ni mabadiliko makubwa kisiasa, ili uweze kupata juhudi za ccm laZIMA uzingatie haya ili kujua kati ya wawili na ni zaidi????

CDM ni lazima ijenge mtandao kuanzia ngazi ya familia, shina nk. CCM inajua inadi kamili ya wanachama na wafuasi wake kila mtaa/kijiji lakini CDM inategemea zaidi kampeni za jukwaani bila kua na uhakika wa kura za kuaminika.
 
MIGIRO akiwa rais nahamia JAMHURI YA WATU HURU YA ZANZIBAR maana itakuwa ni kuudhihaki URAIS n IKULU yetu.

Lakini uje kuwa kwa CCM kumuweka Migiro watakuwa very strategic ikizingatiwa kuwa wapiga kura wengi huwa ni wanawake. Wataweka tofauti zao pembeni na kumuunga mkono
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa CDM wanahitaji mtandao unaoanzia ngazi ya chini kabisa kama wanataka kuwa washindi katika chaguzi zijazo. Wanahitaji mkakati maalum utakaoshawishi kila kundi katika jamii kama wanawake, vijana n.k. Hii bado haipo CDM. Tunataka kuona ile effort kama ya Nyololo inaendelea. Kufungua matawi kila kijiji na kuwa na uwakilishi wa jumuia katika ngazi hiyo. Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014 utatoa taswira kama hilo limetendeka. Bila hivyo CDM watakuwa wanaota ushindi ambao hawataupata.
 
4. Kosa kubwa linalofanywa na upizani ni hili.
Kwanza hamko wamoja kwa hiyo hata kwenye fair ground ikipigwa kura leo wale wasioipenda CCM wanagawanyika kati ya CHADEMA, CUF, NCCR n.k...

Hoja kuhusu upinzani umegawanyika, Chadema so far hawana haja ya kuungana na vyama vingine kwani ukiangalia hata matokeo ya kura za urais hata tukikubali kwamba matokeo ya urais yalichukuliwa, bado in over 80% ya mikoa ya Tanzania (bara) Chadema ilikuwa haina haja ya kuungana na vyama vingine vya upinzani - yani chama kilichoshika nafasi ya tatu na ya nne; Kwa mfano, hata katika maeneo kadhaa ambayo CCM ilishinda kwa margin kubwa mfano 65% ya Kura aidha za Urais au Ubunge, katika mengi ya maeneo haya, Chadema ilipata sio chini ya 30% ya kura zote huku vyama vya upinzani vilivyvobakia vikigawana 5% ya kura; Sasa coalition ya Chadema na vyama vingine hapa ni ya nini?

Chadema inahitaji kuendea wananchi wenye vitambulisho vya kupiga kura wasio na uanachama wa chama chochote cha siasa; Ifikapo 2015,Tanzania itakuwa na wapiga kura kati ya milioni 21 na milioni 22; CCM ina wanachama sio zaidi ya milioni tano ambayo ni chini ya 25% ya wapiga kura Tanzania nzima, which means operesheni vua gamba vaa gwanda haitakuwa na maana zaidi ya operesheni wanachama wapiga kura wapya bila ya kujali kama wanachukua kadi za Chadema au lah; Hiyo ndio moja ya siri za ushindi kwa chadema, lakini vile vile CCM 2015;
 
chadema mnaikumbuka hii kitu?naona kama mmeanza kuicheza ngoja ya ccm kwa wiki takribani mbili mpaka leo ni maongezi ya vikao vya ccm vilivyokipatia viongozi chama hicho chini ya jk kama mwenyekiti,hakuna anaemzungumzia slaa,zitto wala uchaguzi wa viongozi wa chadema,watu wako busy na kina lowassa,mwigulu,karume na jk
KIM KARDASH, ungekuwa unachukua time kidogo tu kufikiri kabla ya kuandika, hungekuwa unajidhalilisha kwa michango ya kipuuzi kama hii isiyo na kichwa wala miguu. Lazima uelewe kuwa katika wiki hizo mbili unazoziongelea CCM walikuwa kwenye pilika pilika za uchaguzi, sasa naomba uzingatie haya;

  1. CCM ni chama tawala.
  2. Mwenyekiti wa CCM ndiye Raisi wa Tanzania.
  3. Raisi ndiye Kiongozi Mkuu wa serikali.
  4. Viongozi wote wa juu wa serikali wako CCM.
  5. Serikali yoooote kuhamia Dodoma.
KIM KARDASH, swali kwako...kwa nini unaona ajabu maongezi kujikita katika Uchaguzi ndani ya chama kinachounda serikali? Kwa nini wakati kama huu wewe ushangae kwa Watanzania kufuatilia mazingaombwe yanayofanyika ndani ya CCM? Kwa nini huwezi kuchukua hata dakika moja kujiuliza imekuwakuwaje hata taratibu za upigaji kura ndani ya chama chako zibadilishwe ili kumnusuru kiongozi dhaifu aliyeshindwa kukiongoza na badala yake uwarukie wasiohusika? Kwa nini mtu ukishajiita mwana CCM, unakuwa hivi? Wakati wote ni kushangilia upuuzi tu na ujinga! Come on, grow up, una zaidi ya mwaka ndani ya JF lakini bado unatambaa tu kama kiwete!
 
CDM ni lazima ijenge mtandao kuanzia ngazi ya familia, shina nk. CCM inajua inadi kamili ya wanachama na wafuasi wake kila mtaa/kijiji lakini CDM inategemea zaidi kampeni za jukwaani bila kua na uhakika wa kura za kuaminika.

chadema wanaitegemea jf,na wanaichukulia jf kama ndio sampling ya uhakika kupima jinsi wanavyokubalika,ndio mana wanafeli sana kila zinapokuja chaguzi za jumla,rejea uchaguzi wa serikali za mitaa walivyofanya vibaya na hakuna aliyewajibika wala kuulizwa kwanini chama kinafanya vibaya huko site ilhali kwenye jf kinaonekana kama kinakubalika sana
 
KIM KARDASH, ungekuwa unachukua time kidogo tu kufikiri kabla ya kuandika, hungekuwa unajidhalilisha kwa michango ya kipuuzi kama hii isiyo na kichwa wala miguu. Lazima uelewe kuwa katika wiki hizo mbili unazoziongelea CCM walikuwa kwenye pilika pilika za uchaguzi, sasa naomba uzingatie haya;

  1. CCM ni chama tawala.
  2. Mwenyekiti wa CCM ndiye Raisi wa Tanzania.
  3. Raisi ndiye Kiongozi Mkuu wa serikali.
  4. Viongozi wote wa juu wa serikali wako CCM.
  5. Serikali yoooote kuhamia Dodoma.
KIM KARDASH, swali kwako...kwa nini unaona ajabu maongezi kujikita katika Uchaguzi ndani ya chama kinachounda serikali? Kwa nini wakati kama huu wewe ushangae kwa Watanzania kufuatilia mazingaombwe yanayofanyika ndani ya CCM? Kwa nini huwezi kuchukua hata dakika moja kujiuliza imekuwakuwaje hata taratibu za upigaji kura ndani ya chama chako zibadilishwe ili kumnusuru kiongozi dhaifu aliyeshindwa kukiongoza na badala yake uwarukie wasiohusika? Kwa nini mtu ukishajiita mwana CCM, unakuwa hivi? Wakati wote ni kushangilia upuuzi tu na ujinga! Come on, grow up, una zaidi ya mwaka ndani ya JF lakini bado unatambaa tu kama kiwete!

Acha ushenzi wako wewe,kuwa kwangu na zaidi ya mwaka mmoja humu has nothing to do with you,jibu hoja acha vioja,wagombea wa chadema kwanini wanafichwa ama wanajificha ilhali wana chadema wanafanya kazi ya kujitolea kuwanadi wagombea wa ccm na kuwapa umaarufu mpaka ikifika siku mtu kapitishwa na ccm kugombea urais anakua tayari mashuhuri huku yule wa upinzani anakua kama underground alieibuka tu,rejea uchaguzi uliomuingiza jk madarakani kwa mara ya kwanza,unakumbuka umaarufu wa jk ambao wapinzani pia walishiriki kwa namna moja ama nyingine kumpa umaarufu kutokana na kujikita kuwajadili wanaotajwa tajwa kugombea kwa tikiti ya ccm ulivyomsaidia jk?yani inafika mahali utaona wanachama wa vyama vya upinzani wanakua nao na wagombea wao wanaowashabikia kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea urais kwa tikiti ya ccm!

unashangaa taratibu za upigaji kura kubadilika ndani ya ccm lakini kutokana na kuzidiwa na mapenzi kupita kiasi unashindwa kushangaa jinsi demokrasia ambavyo imekua ikibakwa ndani ya chama kinachojiita cha kidemokrasia mchana kweupe hadharani,rejea issue ya zitto kuzuiliwa kugombea na genge la mzee mtei,rejea chacha wangwe kuandamwa na wana chama cha kidemokrasia kutoka kilimanjaro mpaka kufikwa na mauti.
 
nime kupata lakini kwa mtazamo wako inaonesha kuwa una hitaji vyama vya upinzania vifuate mfumo wa chama tawala.je vyama vya upinzani haviwezi kuwa na mifumo yake au mwendo ndiyo uleule wa kukopi na kupesti?
 
mfumo wa vyama vya upinzani umeprove kuwa failure,huo ndio ukweli,thats why for years now since tuingie kwenye multi-party system mafanikio yamekuwepo lakini si ya kuridhisha ukilinganisha na wenzetu waliotuzunguka,mfano malawi,zambia na hata kenya na kwingineko afrika ambako tumeshuhudia vyama vikongwe vikipoteza umaarufu na kuondoshwa madarakani na vyama vya upinzani,na kote huko wengi wa waliofanikiwa ni wale waliotoka kwenye vyama tawala na kuadopt mfumo wa chama tawala.Hakuna njia ya mkato,ni lazima tuwe na mifumo inayoanzia kwenye mashina huko sio kwenye miji mikubwa tu then utegemee matokeo,otherwise tutaishika uchawi tume ya uchaguzi kila baada ya chaguzi!
 
Back
Top Bottom