CHADEMA, mmeisoma hii? Wanasema uchaguzi ni maandalizi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, mmeisoma hii? Wanasema uchaguzi ni maandalizi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Oct 21, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hebu chadema na wapinzani kiujumla msikilizeni huyu jamaa acheni kucheza ama kuchezeshwa ngoma msiyoijua...jamaa anajiita OMBUDSMAN anasema hivi:


  Hao wote mama Kilango na mama Simba walikuwa hawafai. Lakini kwa vile suala la EL linazungumzwa kila mara penye chaguzi hizi za ndani ya CCM nirudie haya hapa:

  Watz ni wavivu wa kufanya hata utafiti mdogo tu kama hii habari ya EL. Sikilizeni enyi msioona mbali:-


  1. Kwamba EL si msafi halipingiki. Nape yuko sahihi kusema hivyo lakini pia ni kichekesho kuwa yeye na Katibu Mkuu walipiga 'U turn' ya ajabu kukana ultimatum ya zile siku 90 ambazo EL na wenzake walipaswa kujiengua wenyewe kusafisha chama. Nape na wenzake wamezidiwa kete na kuonekana chochote wanachokiongea sasa kuwa hakina ukweli kwa sababu it is ironically useme mtu si msafi na kweye CC mumpitishe hadi kugombea uNEC na hakuna mahala mmemjadili na kumchukulia hatua kichama. Hayo yataonekana kuwa majungu.

  2. Utafiti wangu unanionyesha kuwa EL kamwe hataweza kupitishwa jina lake kuwa mgombea maana CCM si wajinga mnavyodhani. Kwa sasa, jina lake linatumika ili msiwafikirie wenzake ambao hamuwasemi na katika hao atatajwa mmoja na ndipo mtashangilia (mazingaombwe ya Mwanakijiji) kuwa EL amekomolewa kumbe ndivyo ilivyopangwa. Ni hivi EL hana ugomvi na Rais Kikwete wala Membe wala Migiro. Na hata siku moja hutamsikia Rais wetu wala Membe akisema hayo wazi wazi. Hawa wako pamoja sana na ndio maana ya kuwa na mikakati ya muda mrefu na ambayo huwezi kuipredict kiurahisi kama wenzetu wa CHADEMA wanavyotake political risks bila kuzichambua.

  3. EL yeye hana shida ataendelea kula pension kama Ex-Premier na atakuwa ndani ya NEC, ndani ya CC na Mbuge wa huko kwao kwa hivyo yuko safe & liquid kona zote. Na atakuwa Mweyekiti Kamati ya Bunge na Bodi zenye mashiko ya posho, haitaji Urais. Sana sana wakiona hata mmepumbazika kwa kumhurumia eti jina lake kutopitishwa kwenye Urais basi Rais ajaye kwa kuwa ni mtu wake anampa uWaziri wa nguvu basi mnabaki kung'ang'aa macho kuwa kaonewa kumbe ndivyo ilipangwa!

  4. Kosa kubwa linalofanywa na upizani ni hili.
  Kwanza hamko wamoja kwa hiyo hata kwenye fair ground ikipigwa kura leo wale wasioipenda CCM wanagawanyika kati ya CHADEMA, CUF, NCCR n.k wakati wapenzi wa CCM wao watafia hapo hapo hasa WATAKAPOONA KUWA JINA LA ANAYEPEPERUSHA BENDERA YAO SI Mh. E. LOWASSA ALIYEWAUMIZA WENGI KWENYE CHAGUZI ZA NDANI BALI NI MWINGINE MSAFI ( MIGIRO, MAGUFURI, MEMBE etc) jambo ambalo si kwa sababu za mnyukano bali mpango wa muda mrefu.

  Pili uchaguzi wa kumpata rais ni wa nchi yote kila kitongoji na si maeneo machache tu ya nchi. Uchaguzi Mkuu ni zaidi ya political rally za M4C mkoa fulani au kanda fulani. Unahitajika kuwa na watu wengi kila kitongoji nchi nzima ambao wanaushawishi kwa wengine na pia kuwasimamisha wagombea Ubunge kote nchini kila kitongoji kama wafanyavyo CCM. Sasa angalia CCM imepanua wigo wa ujumbe wa NEC toka mkoa hadi kila wilaya TZ nzima na hao wanaochaguliwa wanaushawishi fulani wa ama kiuiwezo au hata kifedha na pia wana marafiki wao na ndugu zao ambo ndio watawapigia debe CCM (Kimya kimya au kwa uwazi). Chaguzi za CCM Mikoani na za Jumuiya zake UVCCM, Wazazi na UWT ni mtandao tosha ambao unafanya hata CHADEMA na CUF humu wanajadili habari za mama Simba vs mama Malecela bila kujijua mpaka wanasahahu kuwa kuwa BAWACHA au baraza la wanawake wa CUF n.k.

  Swali ni kuwa mbona hatuoni maandalizi ya namna hii ya mfumo wa kutafuta wawakilishi wa jumuiya za vyama vingine vya upinzani katika mtandao mpana kama huu wa CCM Tanzania nzima (haijalishi kuwa hata kama wa CCM pia una mapungufu lakini unaibua ushindani mkubwa sana).

  5. Sikiliza CHADEMA, hakuna ubishi Dr. Slaa ni jembe na anapendwa lakini uchaguzi ni maandalizi ya kuwa na mtandao wa kupata watu wengi (Bara na Visiwani) wawakilishi watakaomsaidia nchi yote kuwashawishi watu wengine waone kuwa kweli huyu akipewa kuongoza nchi kama Rais basi si kwamba itakuwa yake na kakundi kake kadogo kwa Mbowe, Lissu, Mnyika, Mdee bali kwamba kuna watu wengi kila kitindoji Tz yote wenye uwezo kuendesha Wizara zote na Mikoa yote bila kutikisika.

  6. Mwisho, ni bayana pia kuwa hata thread za Zitto na mikwara mbuzi yake ya kuutaka Urais ni kanya boya akitegemea kuzua tafrani CHADEMA maana anatumika. Tunashukuru kuwa hilo limejulika kwa wengi sasa maana amepwaya na ataishia kuwa looser tu kwa kuwatumikia mabwana wawili na kamwe hatasimamishwa na CCM (hata akihama leo CHADEMA) kuwa mgombea na wala hakuna mgombea binafsi anayeweza kupita kuwa rais leo Tanzania; demokrasia yetu haijafikia hatua hiyo hata Marekani bado!

  EL si mgombea urais, anawaandalia watu wake makao ili naye aendelee kufurahia utukufu wa mtandao wake. WaTz hatupendi kujishughulisha na kuchambua kwa undani mambo ya juzi na kesho bali ya leo tu!!!

  Mfano, leo Mh. ShyR Banji ametaka kutwangana na Mh. mama Simba kwenye uchaguzi wa UWT. Hivyo atakuwa na hasira naye na pia EL kwamba ndiye alikuwa sponsor wa mama Simba lakini kesho atasimamishwa mama Rose Migiro, msomi na hana tuhuma na Banji atakuwa wa kwanza kumpigia hata kampeni Tz yote kwa jina la kumkomoa EL hahahahahahahahahah!!!


  Sitaki kusikia mtu akilialia baada ya uchaguzi mkuu (2015) kuwa tumeibiwa kura!!!! Mtu anajiibia kura yeye mwenyewe kuanzia sasa kutegemeana na mfumo wa maandalizi yake.

  Ombudsman, niko huru na niko tayari kutoa msaada wa kweli kwa ajili ya maendeleo ya nchi yangu Tanzania

  EXTRACTED FROM HERE
   
 2. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,099
  Likes Received: 11,248
  Trophy Points: 280
  2010 mlipata kura ngap? Na mkaiba ngap? Ndo kazi ya huo mtandao wa EL kuiba kura?
   
 3. m

  mliberali JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 2,885
  Likes Received: 1,517
  Trophy Points: 280
  leo kim umenifurahisha
   
 4. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Uchambuzi mzuri sana na wakufanyiwa kazi! Lakini huo mfumo wa CCM ni mkongwe sana, na umejengwa kwa rasilimali za umma since mfumo wa chama kimoja. Lakini haliondoi ukweli kuwa CHADEMA tunahitaji mtandao wa nchi nzima ili kushinda urais!
   
 5. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  huna lolote!! ndani ya chama cha mapinduzi hakuna mwenye kufikiri logically kihivyo. haiwezekani mtu atumie mamilioni ya shilingi ili ampishe mwingine na ambae hajatumia chochote.hayo ni matamanio yako lakini ccm hakuna mtu mwenye hiyo busara.kama kweli kuna mwenye busara na hekima ungeona jinsi wanavyo yashughulikia matatizo ya kidini yaliyo jitokeza. KIFUPI CCM WAMEPOTEZA MVUTO, WATEGEMEE WIZI WA KURA KWA KUSAIDIANA TISS WAOGA NA WANAO TOKA FAMILIA MASIKINI.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yote tisa. Migiro anapwaya tena sana tu.
   
 7. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  MIGIRO akiwa rais nahamia JAMHURI YA WATU HURU YA ZANZIBAR maana itakuwa ni kuudhihaki URAIS n IKULU yetu.
   
 8. Mbonica VJ

  Mbonica VJ Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 27, 2012
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hayo ni mawazo yako kakaa
   
 9. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...huo mfumo(mtandao) wa CCM ni mfumo mkongwe sana na uendeshaji wake ni wa ki-analogy zaidi,kitu ambacha hakiendani na mazingira ya sasa hivyo Chadema hawana sababu ya kutishika na wingi wa hao makada wa CCM...hiki ni kizazi cha digital ambacho kinaji-set chenyewe na ambacho Chadema inaushawishi mkubwa sio kma CCM inavyohitaji kuwa na watu wengi wa kugawa kanganga,kofia,tshet na rushwa...mimi nadhani Chadema hinaitaji watu wemye sifa za uongozi,watu wenye mtazamo yakinifu, weredi wa mambo,wabunifu,makini na waliotayari kujitoa kwaajili ya kuikombo nchi,wanaweza kuwa watu wachache tu wakafanya kazi vizuri ya kuliongoza hili taifa kwa kuweka mfumo raisi wa utawara kwa kuitumia tekonlojia ya kisasa...hiyo mipango dhalimu ya hao mafisadi(EL na wenzake) imeishashidwa kabla hata haijafanyika kwani watanzania sasa wanamjua adui anayekwamisha maendeleo yao ni UFISADI unaofanywa na watawala wa serikali ya CCM...
   
 10. n

  ng'witunja Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo uko nje ya mstari hasa unaposema wawakilishi wa ccm ni wenye ushawishi, kwa maana siku hizi uchaguzi wa ccm hakuna kushindana sera tena! M4C ni kiboko kwa maana hapo wananchi wanapata elimu na kujitambua hivyo CCM itaanguka mweleka wa ajabu (hata wenyewe wanajua ndo maana wanapiga vita M4C). Wewe umefikiri vizuri lakini CCM wao wanafikiri watz ni wale wale wa miaka 1947, hiki ni kizazi kingine kabisa hata hao waliokuwepo enzi hizo wameelimishwa sana kupitia utandawazi.
   
 11. k

  kim jong un JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  uko sahihi CCM wote mawazo mgando hawawezi kuwa na arrangment nzuri. Nnachokubali EL na kikwete hawana ugomvi kabisa
   
 12. Mura Weito

  Mura Weito Member

  #12
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwisho wa siku EL atawafanya ccm kama samson alivyo wafanya wafilipi baada ya kugundua kuwa nywele zimeota kichwani lakini macho hayapo so akona hakuna raha ya kuendelea kuishi. ataangusha nguzo zote za ccm ili wote wafie humohumo ndani ya ccm.Ni mtazamo tu!!!
   
 13. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Too much assumption to make it true.
   
 14. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  mkuu watanzania wanaichukia ccm na si mtu flani,angalia wanachama wengi wa ccm mfano Magufuri si kwamba ni mbaya bali
   
 15. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  tatizo ni chama na hata asimame nani jina ccm ni tatzo hata zaidi ya m2 mmojammoja,mwisho wa yote hapa ni kuiondoa ccm
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  lakini mbona hamjibu hoja za msingi za maundishi,hivi iko wapi "uwt" ya chadema,mbona haisikiki,je iko hai?iko wapi ya cuf na nccr..pengine tuanzie hapo badala ya kukurupuka na kumjadili mlete hoja badala ya alichokiandika
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Tatizo letu tunataka kusolve simulteneous equations kwa kutumia jia ileile wakati kuna approach zaidi ya mbili kwa wanamahesabu watanielewa.Usiwalazimishe CDM watumie approach ya ccm.Mbona wao ccm hatujamsikia katibu mkuu wa UVCCM akizunguka mikoani kama anavyofanya HECHE wa chadema???? kwani anachofanya heche hakina impact ktk siasa za tz hasa kuhusu kuimarisha chama na kupata umaarufu???
  CDM tunawaona walivyopbadilisha siasa za Tanzania leo ukielekea mrogoro njiani unakutana na bendera za cdm barabarani tofauti na zamani, hayo ni mabadiliko makubwa kisiasa, ili uweze kupata juhudi za ccm laZIMA uzingatie haya ili kujua kati ya wawili na ni zaidi????
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu hapa.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Oct 22, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  I thought so.
   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kaka jumuia za chama ni muhimu sana kuwa nazo,naungana na wewe heche na genge lake wanajitahidi sana lakini hawatoshi,inabidi kuwe na jumuiya zingine chamani hasa ya kina mama ziwe hai,hii itasaidia pia kupata trust kwa wapiga kura wa jinsia ya kina mama ambao ndio mtaji wa ccm na ndio wengi.

  Kuhusu suala la bendera kuwa nyingi,si hoja,kuna wakati ukiafiri njiani kuelekea mikoani cuf na ccm walikua wanashindani kwa bendera,yani cuf walikua na bendera almost kila kijiji..acheni ukaidi imarisheni jumuiya ya kina mama angalau ili ifanye kazi kama ya vijana,hiyo ndio mihimili.
   
Loading...