CHADEMA mlisusa acheni nongwa dhidi ya Halima Mdee na wenzake

Huyu mwanamke hua hana hoja anaandikaga takataka tu. Very useless.
 
Mbona mnataka kupachika wengine?
..Halima Mdee na wenzake watafutiwe utaratibu mwingine wa kuingia bungeni.

..utaratibu uliotumika awali sio sahihi kwasababu Chadema imewakana na kuwatimua uanachama.
 
Mkuu, kwani Halima Mdee na hao wenzake 18 maarufu kama COVID 19 bado ni wanachama wa CDM?
Wawe wana Chadema wasiwe wana Chadema, tunachojua sisi ni Wabunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema.
 
wangekuwa sahihi wangefungua japo kesi moja kupinga matokeo ya uchaguzi hata japo Kwa wabunge.
Huoni kama hao Chadema wako sahihi kwa sababu hawakutoa baraka zao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za nchi?

Kama ungejiongeza, basi ungemshauri bosi wako Ndugai atangaze hadharani ya kwamba hao wabunge, wapo bungeni kwa nguvu yake! Na siyo ya chama chao na ambacho hakiwatambui.
 
Ndugu zangu,

Chadema walisisia matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 wakaahidi kutoshiriki uchaguzi wowote siku zijazo.

Ingekuwa busara waendelee na shughuli nyingine waachane na siasa kwani masharti yao hayakutimizwa.Sio lazima Chadema kushiriki chochote,kitendo chao kuwasakama akina Halima Mdee ni nongwa na husda.

Ukisusa susa kweli acha kutazama nyuma.
Asante Wakudada, baeleze baelewe, ukisusa, sie twala. Kina Halima ni mashujaa!.
P
 
Back
Top Bottom