CHADEMA mlisusa acheni nongwa dhidi ya Halima Mdee na wenzake

Kwa sababu walishavuliwa uanachama wao ndani ya CHADEMA. Hata pale walipokata rufaa dhidi ya kuvuliwa kwao uanachama basi wanatambua kuwa wao si wanachama tena wa CHADEMA mpaka pale watakapoweza kuzishinda rufaa zao na hatimaye kurejeshewa tena uanachama wao.
Hao kushinda rufaa zao ili warudishiwe uanachama ni sawa na kuniambia mimi njiunge na ccm.
 
Ndugu zangu,

Chadema walisisia matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 wakaahidi kutoshiriki uchaguzi wowote siku zijazo..
Uko sahihi.

Halima na wenzake ni Wabunge wa viti maalum wa Chama cha Mapinduzi.

Mwambie Spika Ndugai arekebishe taarifa za Kibunge ili Chadema isiwasakame.

Tatizo hapa ni lile la kuendelea kutamka kuwa Halima Mdee na wenzake ni Wabunge wa Chadema, wakati dunia inajua kuwa Chadema walitamka kutoutambua Uchafuzi Mkuu uliopita.
 
Chadema walisema uchaguzi wa 2020 ulikuwa batili, sasa kuwaandama wabunge 19 wa chama chao wenyewe na kuwaacha wale wengine wa chama twawala wanaonyesha hawana mtazamo mpana wa kisiasa na kuishia kujikita kwenye siasa za matukio, mihemuko, wivu huku wakiwaacha ccm wakiendelea kujivinjari kana kwamba hawana mpinzani serious...
Uelewa wako kwenye jambo hili watia shaka sana, ndugu.

Hebu kaa ujiulize kwa nini waingizwe huko bungeni kwa jina la CHADEMA?

Wangekuwa wameingia huko kivyaovyao hakuna ambae angehangaika nao, labda wa kwenu huko lumumba.
 
Uelewa wako kwenye jambo hili watia shaka sana, ndugu.
Hebu kaa ujiulize kwa nini waingizwe huko bungeni kwa jina la CHADEMA?
Wangekuwa wameingia huko kivyaovyao hakuna ambae angehangaika nao, labda wa kwenu huko lumumba.
Kwani chadema wana jipya lipi hadi jina lao lisitumike kuwaingiza wabunge.....kuna uchaguzi wowote mkuu walishashinda nafasi ya urais, au akishakaa mbowe hapo tayari manona mna rais...
 
Kwani chadema wana jipya lipi hadi jina lao lisitumike kuwaingiza wabunge.....kuna uchaguzi wowote mkuu walishashinda nafasi ya urais, au akishakaa mbowe hapo tayari manona mna rais...
Utakapoelewa itakusaidia
 
..Halima Mdee na wenzake watafutiwe utaratibu mwingine wa kuingia bungeni.

..utaratibu uliotumika awali sio sahihi kwasababu Chadema imewakana na kuwatimua uanachama.
 
Ndugu zangu,

Chadema walisisia matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 wakaahidi kutoshiriki uchaguzi wowote siku zijazo.

Ingekuwa busara waendelee na shughuli nyingine waachane na siasa kwani masharti yao hayakutimizwa.Sio lazima Chadema kushiriki chochote,kitendo chao kuwasakama akina Halima Mdee ni nongwa na husda.

Ukisusa susa kweli acha kutazama nyuma.
Tumia akili kidogo unapoandika mbona povu linakutoka ,sasa hivi ni serikal ya awamu ya 6 tulia sindano ya nchi 6 ikuingie tukujue.
 
Back
Top Bottom