JOYOPAPASI
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 250
- 408
*CHADEMA MLIPOPELEKA MBOGA NDIYO MFUATE CHAKULA*
Nimeona Malalamiko ya CHADEMA wakiitaka Serikali iwaeleze kwanini hawakupewa nafasi ya kuingia ndani ya Uwanja wa Uhurru kuungana na Watanzania wengine kumuenzi kipenzi chao *Rais Mstaafu Benjamini Mkapa.*
Mwalimu Nyerere alishawahi kusema kiongozi mzuri ni yule anayeheshimu mamlaka iliyopo madarakani, hakuna asiyefahamu hata mtoto wa darasa la 3 anayefundishwa somo la Uraia anaambiwa kiongozi Mkuu wa Nchi ni Rais na si mwingine.
Kuna sababu bilioni za kuamini, CHADEMA hawakuwa na nia dhati ya kushiriki maombolezo ya Rais Mstaafu Mkapa kama *wanavyojishaua* sasa hivi bali lengo lao lilikuwa ni kupata huruma ya kisiasa.
Taratibu, muongozo na maadili ya viongozi wa Umma, sehemu ambayo Mkuu wa Nchi anakuwepo kiitifaki yeye ndiye mtu wa mwisho kufika kwenye eneo hilo na baada ya kufika yeye tukio ndiyo linaanza, wanaokuja baada yake wanaruhusiwa kuingia kwenye eneo la tukio kama raia wa Kawaida, haijalishi nafasi yake ndani ya Serikali au nje ya Serikali, CHADEMA hawalijui hili ndiyo maana walifika baada ya Mkuu wa Nchi, Waligoma kukaguliwa, walisababisha fujo wakati kulikuwa na viongozi wa Mataifa mengine.
Kituko hiki cha CHADEMA leo kimeonesha *Ombwe kubwa la kiuongozi* lililopo ndani ya chama hicho, walitaka kulitumia tukio la huzuni kujinufaisha kisiasa, baada ya kuona jana Watanzania waliwagomea Uwanja wa Ndege na wakaji kuta wao wanachama wao Uchwara.
CHADEMA wameumbuka sana na watanzania wameshawajua kama hawa watu wanashindwa kuheshimu Mamlaka ya viongozi wa Umma wataweza kuwaongoza Watanzania ambao watawapigia kura Oktoba 28, unagundua hawana uwezo wa kuwatumikia Watanzania, *chaguo pekee lililobaki ni John Pombe Magufuli.*
Waswahili wanasema *kurukaruka kwa Maharage ndiyo kuiva kwake,* CHADEMA wamekosa sera na ajenda za kuwaambia wananchi kwenye Uchaguzi ujao, hivyo wameanza visanga na vitimbwi kama watoto wa kambo, niwaambie mtakula mlipopeleka mboga tukutane kwenye box.