manywangari jean malonkwa
Senior Member
- Mar 17, 2016
- 193
- 188
Tangu aingie madarakani Dactari John Pombe Magufuli amekuwa akipambana na watu wanaoitwa mafisadi kwa mtindo unaoitwa kutumbua majipu.
Swala hilo limempa credit sana kwa wananchi walio wengi, na limenoga zaidi pale alipowapa nafasi ya kumtumbua moja wa wanaoitwa majipu tena wakiwa juu ya daraja la kisasa, utawambia mini tena hawa watu kuhusu Magufuli.
Kwa upande mwingine upinzani(CHADEMA) wamekuwa wakipinga swala hili. Hoja yao ni kwamba utumbuaji majipu sio suluhu la matatizo ya watanzania Bali ajielekeze kwenye mikakati ya kiuchumi itakayowakwamua wananchi badala ya kuendelea kutumbua majipu.
Hoja yao inaweza ikawa na mashiko lkn kuna hiki kitu wanakisahau. Huyu shetani kwa jina la ufisadi wao ndo walimtengeneza, wakatumia media kumsambaza, wakawaaminisha watanzania kuwa adui wa maendeleo yao ni ufisadi na mafisadi.
Wakaenda mbali zaidi kwa kutoa majina ya vinara wa mafisadi pale mwembeyanga kwa kutumia mile walichokiita "the list of shame", baada ya hapo wananchi wakaanza kuwaamini wakawaunga mkono ktk kumtengeneza hiyo shetani, wakaandamana pamoja nanyi.
CHADEMA ikaanza kuwa kanisa la watu wengi hadi leo watanzania wanachojua adui yao ni ufisadi na mafisadi.
Mheshimiwa pombe ambaye ni mwanasiasa kama ilivyo kwa Mbowe, Lisu na Zitto naye ameiona fulsa hiyo iliyotumiwa na CHADEMA kufika hapo ilipo. Magufuli naye sasa anajiimarisha kwa kumtumia shetani huyo mliyemtengeneza na kumtumia kufika hapo, ndio mlimtengeneza!! sio nyie mliosema Lowassa na genge lake ni mafisadi lkn akaja kuwa mpeperusha bendera wenu.
Sasa anachokifanya anapambana na hiyo shetani, anatumia media kama mlivyofanya na ameenda mbali zaidi kwa kuwauliza wenyewe amtumbue au amuache shetani unadhani watajibu nini" mtumbue" eboo.
Sasa wananchi wanatembea kifua mbele yule shetani wetu sasa amepata FIBA, kila anayejaribu kukosoa wananchi wanatamani nae atumbuliwe hata kama sio jipu( shetani, ufisadi) maana wanaamini anawacheleshea maendeleo.
Ushauri wenu kwa CHADEMA kuweni making na namna mnavofanya ukosoaji kwa magufuli, vinginevyo anaweza kuwapoteza maana raia wamekolea hawaambiwi kitu kama walivokolea wkt mkimtengeneza huyu shetani.
Kuwaambia tena kuwa aliyesababisha muwe masikini kuwa sio huyu shetani hapo mnaweza kuwa mko sahihi hawatawaelewa ukizingatia shetani mmowapo kati ya wale kumi mmeshamsajiri kwenu.
Hawa wadanganyika wanaweza kuwapa kidogo kabisa maana nawaona wanamatatizo ya kupoteza kumbukumbu ndo maana shetani wa miaka hiyo aligeuka malaika ndani ya miezi mitatu naamini walikuwa wamesahau tayari.