CHADEMA mlifunika kombe WAZANZIBARI WAMELIFUNUA. Kazi kwelikweli.

Lazima tuelewe kuwa nchi mbili ndizo zilifanya muungano yaani Tanganyika na Zanzibar so hapa the issue ni kwamba muungano uvunjwe then kila watu wawe na serikali yao sie tubaki Tanganyika na wao Zanzibar then basi tukae chini tena ili tuwekeane mikataba ya muungano kama vile Europeen Union then kutakuwa na serikali ya Muungano kwa maana hiyo kutakuwa na serikali 3 ile ya Muungano,Zanzibar na serikali ya Tanganyika.
 
Zanzibar MAFUTA hakuna tusidanganyane, na mtakuja shangaa mkikuta mafuta yamepatikana bara, na hayo mafuta ya Zanzibar yanaposadikiwa ni mpakani na Tanga, na kuna uwezekano mkubwa ni upande wa BARA.
Ni bora hivyo iwe hayako, ndio salama yao.
Umeona wapi katika Afrika hii, ambapo kuna rasilimali na wenyeji wanafaidika nazo?
Angalia mafuta ya Angola na Equatorial Huinea kwa mfano, mafuta yananufaisha tabaka tawala.
Tusiende mbali, hapa hapa Tanganyika, maeneo yenye madini ndiyo yanayoongoza kwa umasikini, magonjwa na uharibifu wa mazingira.

Tusijidanganye Wadanganyika (in this case, Wazanzibari wasijidanganye kwa utajiri wa mafuta.

Kuhusu Muungano, kama viongozi wa sasa wana akili na wanaona mbali, njia pekee iliyobakia ya kuuokoa ni kuunda serikali tatu, vyenginevyo utavunjika kabisa. Ni ama serikali tatu au kuuvunja, hakuna option nyengine.
 
Wananchi wa zanzibar wamesalitiwa na wabunge wao kwa sababu ya unafiki, hivi si mnakumbuka wabunge wa cuf na ccm walivyoungana kumtukana tundu lissu? Wanafiki wana sifa moja, kwamba wakihaidi hawatimizi! Cuf waliahidi kudai serikali tatu, yako wapi madai yao? Wameshirikiana na ccm wamesahau!
 
...Mi naona bora wasepe watanganyika tuko poa kabisa.
ila watakuja kulia na kusaga fizi!!. dhambi kubwa kabisa ya utengano mhiiiiiiiiiiii......


Hili suala la Muungano si Wazenji tu ambao waliwahi kulilalamikia na kutaka uvunjike. Hata Watanganyika waliwahi kufanya hivyo mathalani wale wabunge 55 ambao walitaka serikali ya Tanganyika irejeshwe wakaishia kusambaratishwa na Nyerere. Lakini pia baadhi ya vyama vya upinzani viliwahi kupata umaarufu mkubwa kwa kukumbatia ajenda ya kupatikana kwa serikali ya Tanganyika. Mfano ni mchungaji Mtikila ambaye muda wote amekuwa makini kabisa kuhusu suala hili (soma kiambatanisho). Kuna wakati kulikuwa na harakati za kufikisha suala hili Umoja wa Mataifa (mpaka maombi rasmi yalikabidhiwa kwa Katibu Mkuu), ilikuwa mshikemshike a aina yake.
Ukizingatia kwa makini utaona kuwa Wazanzibar ndio wakoloni huku Tanganyika na wala si Watanganyika huko Zenji kama inavyodaiwa. Hebu fikiria kidogo tu kuwa masuala mengi si ya Muungano. Hata hivyo ili bajeti ya yale ambayo si ya Muungano ipite inabidi yajadiliwe na wabunge wa Zanzibar ambao hawana maslahi yoyote nayo (huo si ukoloni?). Tena hata kwenye baraza la mawaziri, wazenji hushiriki kujadili mambo ambayo hayaihusu Zanzibar hata kwa chembe, tena kwa gharama za Tanganyika, sijui tuwaiteje? Wadanaganyika kwa kweli ni watu wema ajabu. Sasa ni zamu yao
 

Attachments

  • DHANA YA.docx
    30.7 KB · Views: 91
Ondoa mafuta (nishati) katika mambo ya muungano kama wanavyoomba wazanzibari waonje huo moto kwanza.
 
Kwani ukinya lazima tunye sote! waache wala tende na haluwa wanye sisi tunatema mate tunasonga mbele upo hapo?
 
Back
Top Bottom