CHADEMA, mkono mtupu haulambwi!

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,655
Hakika ni kweli mkono mtupu haulambwi hii ina maana gani kwa cdm? Chadema ijiandae kwa next election kwa hali na mali iweze kuchukua dola.Chadema iliweza kunadi sera zake kwa uzuri na ufasaha lakini chama cha kijani kilitumia serikali za mitaa kupata ushindi ambao hata hivyo si halali. Haingii akilini uchaguzi wa jimbo moja uchukue zaidi ya masaa 36 kukamilisha la hasha lazima kuna mchezo uliofanyika ndugu zetu wa vijijini wanatakiwa kupewa elimu zaidi ya uchaguzi kwani vijijini wanadhani ccm ndo mungu wao hivyo basi cdm kuanzia sasa ijichimbie vijijini.
 
Nilijua tu maana safu nzima ya Chama cha Kijani kimejikita huko, huko sishangai kwa haya yaliyotokea huko!
 
Ni kipimo kizuri cha ukuaji wa chama (cdm) kwan mwaka jana ktk jimbo hilohilo na uchaguzi hakikutoa ushindani wa karibu kwa deep green (ccm).

vilevile inaongeza (chochea) madai ya katiba mpya as well as tume huru ya uchaguzi
 
Kuna somo la kujifunza hapa, kwanza: media houses zijifunze kulipoti ukweli unaooonekana on the groud na si fikira binafsi- tulio mbali na igunga tulidanganywa kuwa mikutano ya ccm haikuwa na watu bali chadema ilifunika, nahisi tulikuwa tunadnaganywa. Kuna memba wa JF alipost kuwa mgombea wa chadema amekata tamaa- members walitamani kumlalua humu janvini- this was misleading. We need to be real ili tuwe na mikakati sahihi ya kuelimisha jamii.
Hakika ni kweli mkono mtupu haulambwi hii ina maana gani kwa cdm? Chadema ijiandae kwa next election kwa hali na mali iweze kuchukua dola.Chadema iliweza kunadi sera zake kwa uzuri na ufasaha lakini chama cha kijani kilitumia serikali za mitaa kupata ushindi ambao hata hivyo si halali. Haingii akilini uchaguzi wa jimbo moja uchukue zaidi ya masaa 36 kukamilisha la hasha lazima kuna mchezo uliofanyika ndugu zetu wa vijijini wanatakiwa kupewa elimu zaidi ya uchaguzi kwani vijijini wanadhani ccm ndo mungu wao hivyo basi cdm kuanzia sasa ijichimbie vijijini.
 
We thank GOD uchaguzi umeisha na tunaamini umoja wa wana Igunga na Watanzania kwa ujumla utarudia tena na hautaathiriwa na itikadi zetu za Kisiasa au Kidini
 
Nashukuru kila ninapopita maneno ya wizi wa kura ndo yanayotawakla 100% lazima tujipongeze kwa hatua ya kugundua hilo! Ipo siku haki itatawala!
 
na hao watu wa kijani wajue ipo siku itakula kwao kwani watu wanaelimika na walishachoshwa na siasa uchwara za kijani.
 
Kuna somo la kujifunza hapa, kwanza: media houses zijifunze kulipoti ukweli unaooonekana on the groud na si fikira binafsi- tulio mbali na igunga tulidanganywa kuwa mikutano ya ccm haikuwa na watu bali chadema ilifunika, nahisi tulikuwa tunadnaganywa. Kuna memba wa JF alipost kuwa mgombea wa chadema amekata tamaa- members walitamani kumlalua humu janvini- this was misleading. We need to be real ili tuwe na mikakati sahihi ya kuelimisha jamii.

Tuna mengi tu ya kujifunza. Binafsi nimegundua kuwa jamvi limevamiwa na watu wasiostahili kabisa kuwa humu. Wanatoa habari za uongo, uzushi na wakati mwingine za udaku! Tunapoteza muda kujadili habari ya kutunga au ya udaku.
Nashindwa kushauri nini cha kufanya sababu sifahamu wanachokifanya mods kabla ya kuweka jukwaani posts za watu. Wamekuwa wakisema wanazipitia lakini thread nyingi zimewaprove wrong! Bado natafakari lakini ni vizuri tukaliangalia hili wote kama tunapenda jukwaa lilete maana yake!
 
tutafanikiwa tukianza mtandao wa 'database' tu vinginevyo itatulazimu kuingia msituni.
 
Tuna mengi tu ya kujifunza. Binafsi nimegundua kuwa jamvi limevamiwa na watu wasiostahili kabisa kuwa humu. Wanatoa habari za uongo, uzushi na wakati mwingine za udaku! Tunapoteza muda kujadili habari ya kutunga au ya udaku.
Nashindwa kushauri nini cha kufanya sababu sifahamu wanachokifanya mods kabla ya kuweka jukwaani posts za watu. Wamekuwa wakisema wanazipitia lakini thread nyingi zimewaprove wrong! Bado natafakari lakini ni vizuri tukaliangalia hili wote kama tunapenda jukwaa lilete maana yake!

Ushabiki na unazi umetangulizwa mbele na kuwapa watu matumaini kupita kiasi. tuache ushabiki tuseme ukweli ohh Chadema imeteka igunga sijui ohh tusidanganyane jamani.
 
JAMANI NIMEKIMBIA CCM SABABU NAAMIN KUBAKI CCM NI KUJIIBIA SASA NAUNGANA NA WENZANGU WA CHADEMA WENYE MAPENZ MEMA NA NCHI HII,NINATARAJIA KWENDA KUSHUGHULIKIA KADI YA UANACHAMA KUANZIA KESHO,NIPOKEEN WAZALENDO WENZANGU WA CHADEMA ,pia naomba msamaha kwan uchaguz wa mwaka jana nilikuwa mmoja wapo niliyemuongezea huyu tapeli mkuu wa nch hi(kiwete).
 
Kuna somo la kujifunza hapa, kwanza: media houses zijifunze kulipoti ukweli unaooonekana on the groud na si fikira binafsi- tulio mbali na igunga tulidanganywa kuwa mikutano ya ccm haikuwa na watu bali chadema ilifunika, nahisi tulikuwa tunadnaganywa. Kuna memba wa JF alipost kuwa mgombea wa chadema amekata tamaa- members walitamani kumlalua humu janvini- this was misleading. We need to be real ili tuwe na mikakati sahihi ya kuelimisha jamii.
Ee bwana umenena. Members wengi wa Jf tunajua ni wafuasi wa cdm. Huwa hawapendo kuambiwa ukweli. Wanashabikia sana unazi tu na mambo yasiyo na msingi. Umuhimu wa chama pinzani si katika umahiri wa matusi. Ukipna hivo basi wengine tunajua kwamba hapa hakuna wanachama bali wahuni tu ambao hata kura hawapigi
 
Wana Igunga walikua wanataka posho na misosi sasa CDM wanapeleka sera tupu ndiomana wameshidwa na chama cha kijan kilichogawa posho na misosi
 
...Unachosema ni kweli lakini ndio tatizo kubwa linalowakubwa watanzania wengi. Kutokana na umasikini uliokithiri mtu akionyeshwa sahani ya wali na T-shirt au Sh. 5,000 anabadirika kabisa bila kujua kwamba kupozwa kwa njaa yake kwa muda mfupi kutapelekea yeye kuathirika zaidi mbeleni. Kwanza ni matusi chama kuweka sahani za wali jukwaani kwenye kampeni. Nini maana yake kuwa nyie kuleni wali then mtusikilize..........!!! Mbaya sana.
 
Back
Top Bottom