CHADEMA Mkoa wa Arusha-Taarifa kwa Umma,kumbukumbu ya January 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Mkoa wa Arusha-Taarifa kwa Umma,kumbukumbu ya January 5

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nanyaro Ephata, Jan 4, 2012.

 1. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  TAARIFA KWA UMMA: KUMBUKUMBU YA TAREHE 5 JANUARI
  04 JANUARI 2012.
  Ndugu wananchi na wakazi wa Arusha.
  Tarehe 5 Januari ni siku ya kumbukumbu ya maana sana katika chama chetu kwenye mkoa wetu na halmashauri ya jiji letu la Arusha.

  Tarehe 5 Januari mwaka 2011 ulifanyika mkutano mkubwa ambao ulikuwa umebeba ujumbe wenye madai ya wananchi kuhusu ukiukwaji wa demokrasia katika suala la uchaguzi wa UMEYA katika jiji la Arusha. Wakazi wa Arusha walijitokeza kwa wingi kwa sababu walikuwa wameelewa nini hasa kilikuwa kinalalamikiwa.

  Kwa yote yaliyotokea mwaka mmoja umepita sasa, chama kinawapa pole makamanda wote na kuwataka tujipe moyo kwa safari ya ukombozi tuliyoianza. Sote tufahamu kuwa iko siku tena sio muda mrefu wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla tutafaidi matunda ya rasilimali zetu nyingi ambazo kwa ujumla wake iwapo zitasimamiwa vizuri kwa haki na usawa hatupaswi kuitwa maskini.

  Tarehe 5 Januari, CHADEMA tulipaza sauti zetu tukiwa na madai ya msingi sana ambayo yanabeba maisha ya wakazi wa Arusha. Suala la uchaguzi wa MEYA wa jiji la Arusha ambao ulichakachuliwa kwa uwazi, makusudi na aibu kwa waliotenda. Bado madai ya wakazi wa Arusha na chama kwa ujumla yanabaki pale pale kuwa hatumtambui MEYA wa CCM aliyechaguliwa kwa mazingira yasiyo ya haki.
  Kwa vile suala la maandamano lipo mahakamani, hatutalizungumzia, tunasubiri haki na sheria vichukue mkondo wake katika kuamua kuhusu suala hilo.

  Sambamba na hili, tunawapongeza wakazi wa Arusha kwa ujasiri na umahiri wao katika kupigania na kusimamia bila woga masuala ya msingi. Ujasiri huu ndio unaopelekea wakazi wa Arusha kutokubali kunyanyaswa hasa inapokuja kwenye masuala muhimu ya haki za binadamu.

  Kwa wakati wote hali ya Arusha katika uhalisi imeendelea kuwa ya amani na utulivu na watu wamekuwa wakifanya shughuli zao kama kawaida licha makada wa chama tawala CCM na baadhi ya viongozi wa serikali kutoa maneno yenye utata kwa kuizungumzia hali ya kisiasa kwa sura ya kukejeli demokrasia na haki za watu.

  Tunaendelea kuwasihi wakazi wa Arusha waendelee kuwa majasiri, waendelee kuwa wachapakazi na kuwa tufanye kazi kwa kujituma kwa maendeleo yetu na ya watoto wetu.

  Mwaka wa 2012 uwe ni mwaka wa kitofauti katika kuifanya Arusha yetu kwa kuleta na kufikia mabadiliko chanya ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na zaidi sana kushughulikia kwa dhati suala la ajira kwa wasio na ajira.

  Amani Golugwa
  KATIBU WA CHADEMA MKOA WA ARUS
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tupo Pamoja sana! Nguvu ya umma
   
 3. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,786
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  hukukumbuka wala kutaja waliopoteza maisha!
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  pamoja sana
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi yale maandamano yalizaa tija yeyote? Au kufukuzwa madiwani ndio ilikuwa lengo?
   
 6. kajwa

  kajwa Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante....
  Na mapambano yataendelea..!
   
 7. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wewe unaonaje yalizaa au hyakuzaa?
   
 8. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Tutafanya mkutano wa hadhara NMC kuanzia saa tisa mchana
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Nguvu ya Umma wabunge 23?
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Huo mkutano mnawakumbuka kina nani? Kwa nini hizo pesa za maandalizi ya mkutano pamoja na posho mtakazopeana msiwape familia za wale waliopoteza maisha?
   
 11. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wngapi wanatosha kuwa nguvu ya umma?je tume ya uchaguzi ni huru?palikuwa na ushindani linganifu?
   
 12. s

  sakafu Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni fujo zenu
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbaka kieleweke!
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Fafanua mkuu,hapa JF tunajadiliana kwa hoja!karibu sana JF!
   
 15. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  saa ya ukombozi ni sasa,kuna haja kubwa sana kuwakumbuka mashujaa wa demokrasia makini toka demokrasia mgando
   
 16. N

  Nyota Njema Senior Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukio la Arusha linapaswa kulaaniwa na kila mpenda haki nchini, na kumbukumbu yake ni muhimu ili wote wanaofikiri kuwa kumwaga damu za wanaharakati ndiyo njia ya kung'ang'ania madaraka wazidi kuona aibu na kuacha ushenzi wao. CHADEMA inapaswa kuifanya siku hii kuwa muhimu kwa ajiri ya kuwakumbuka wenzetu waliojali zaidi maslahi ya Taifa kuliko hata uhai wao. Ole wao walioua Arusha, siku zao zinahesabika!
   
 17. L

  Luiz JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vzur kesho mkpitsha japo mchango ili tukawakarm ndugu na kuwatembelea ni vzur zaid, pamoja sana makamanda
   
 18. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Na rais aliechaguliwa na watu milioni 5 kati ya milioni 40+?
   
 19. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  Hivi nguvu ya umma iliyom-baka Gadafi ilikuwa na wabunge wangapi vile?
   
 20. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Thax kwa taarifa nzuri! Peoples power tupo pamoja!
   
Loading...