CHADEMA Mkishinda 2015 bado mtaacha kuwe na vyama vya upinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Mkishinda 2015 bado mtaacha kuwe na vyama vya upinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Aug 29, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Ni hoja tu maana nguvu inayotumika ni sahihi kwa ajili ya kushinda shida ni kuwa sio nguvu ya hoja ila ni hoja ya nguvu hasa hasa ukizingatia kauli mbiu ya "PP". Historia inaonyesha chama chochote kikiboronga haijalishi ni chama gani na kilikuwa maarufu kiasi gani, watakikataa tu! Nani alijua CCM itakuwa na upinzani huu wa sasa? Hata kama upinzani wenyewe una mapungufu, lakini unakishikisha adamu CCM.

  Wasiwasi wangu uko kwa viongozi na jinsi watu wanavyopokea hamasa zao, inaonekana nguvu inayotumika ni ya mwili zaidi kuliko hoj na mipangotunayoitarajia, ikiwemo kurushiana kashfa na matusi (nasema hivi kwakuwa CCM nao wameingina kwenye mtego wa kurushiana vijembe). Kuna hatari wakiiingia madarakani wakahamasisha chuki hii hii na kutaka chama kilichokuwa madarakani kiteswe au kiadhibiwe au hata kifutwe.

  Ni vema kuyasema haya kabla hayajatokea, kuliko kusubiri. Nasubiri busara zenu kwenye kuchangia mada hii.
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Sidhani kam utakuwa fair kusema kuwa jamaa wanatumia mwili kuliko hoja.Sidhani kama kuna anayeweza tumia mwili against ccm na kushinda, kwani wana kila kitu.Hata nguvu ya umma ina hitaji mvuto na ushawishi.Ingawa umeonyesha kuwa umeona uwezekano mkubwa CCM kuondoka.

  Lakini kuhusu hilo la kuacha upinzani sidhani kama unamaanisha CDM kuna mashaka.KWA KAULI YA SUGU ALIPOMPASUKIA LIVE MP NA MH RAIS KUWA MWENDO WA CDM SI UPEPO BALI NI KIMBUNGA KINACHOELEKEA KUING`OA CCM 2015,NA TATIZO LAO NI KUWA HAWATAPENDA WAFIKE PALE WAKIWA NA MPINZANI LEGELEGE KWANI HAWATAPATA CHANGAMOTO.

  Unachoshindwa tambua ni kwamba CCM watajikuta wakipata kipindi kigumu bila hata kulipizwa kisasi.CCM wana watu walioliibia taifa, waliovunja haki za binadamu, etc.sasa lazima hawa watu washitakiwe,ili warudishe hela ndugu yangu, na wengine wawajibishwe.Tatizo litakuwa ccm ikiondokewa na hao watu wanaotuhumiwa watabaki salama?Kwa watu waovu watajificha ktik kisingizio kuwa wanalipizwa kisasi(na ndio hata wewe unawakilisha hapa),ila sivyo.

  Mimi nilidhani muda huu CCM wangekuwa wakifanya maandalizi ya kuwa mbadala kuliko ya kubaki.ili wajue jinsi ya kusurvive nje ya hizi tabia za mikakati ya urais, kwa vile ccm imekuwa ikiamini kuwa mteule wao automatically anaenda kuwa rais.Sasa mitazamo itakuwa tofauti CCM itakapokuwa katika mazingira ya kutokuwa na hakika ya kutoa rais.Watu watapunguza kasi ya kujiwekeza katika ccm kwa gharama kubwa.kwani baadaye watakuwa na wakati mgumu wa kujiwekeza kwa wapiga kura waliogawanyika.mara nyingi nimesema kuwa kwa mwenye akili ,kugombe akupitia ccm ni too much risk.Hela zitolewazo, na makeke mengine,halafu kuja katik game na upinzani bila hakika ya kushida ni biashara kichaa.Next election litadhibitika hili kwa wabunge wa ccm watakaosimama ns watoto wadogo wa cdm wasio hata na nyumba ya kuishi,sijui kama mabomu yatatosha kubadili ushindi.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Vyama vya upinzani vitakuwepo ila UFISADI hautaruhusiwa, mafisadi wajiandae kusepa
   
 4. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwani uwepo wa vyama vya upinzani ni sera ya chama?
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hii hoja inatakiwa iwekwe baada ya chadema kuongoza serikali.
  Manake hii ni sawa nakusema eti mwanamke akiolewa anazaa?
   
 6. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,216
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Vitakuwepo tena vitaimarishwa zaidi
   
 7. a

  alfazulu JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 735
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM au chama kingine chochote iwapo hakitafuata taratibu za sheria za vyama za siasa lazima wachukuliwe hatua, na ka ma serikali itayoingia madarakani 2015, itakuwa na utashi wa kuwashughulikia wana ccm waliovyunja sheria za nchi na kuliingizia taifa hasara, nitawaunga mkono saana tu. Lazima tufike mahala tuwe na serikali inayoheshimu sheria za nchi na kuzisimamia. nakama ktk kutekeleza majukumu yake CCM wataingia humo then well n good, wakati huo kutakuwa hakuna aliye juu ya sheria zaidi ya sheria yenyewe. So hilo lisi tafsiriwe kama nia mbaya ya kulipiza kisasi hasa na wana CCM.
   
Loading...