Uchaguzi 2020 CHADEMA mkisema mtatoa Huduma za Afya bure, naomba mjibu hoja zifuatazo

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,884
Nimeona CHADEMA ikijinadi kuwa ndani ya siku mia moja watahakikisha huduma za afya inatolewa bure kwa kushirikiana na taasisi binafsi. Kwangu hili itakuwa jambo jema kwa watu zaidi ya watu millioni 60 watapewa huduma bure kabisa bila kuchangia chochote.

Lakini nina mashaka na ahadi hii
1. Kwanza CHADEMA na wapinzani mmekataa kuwa Tanzania siyo nchi yenye uchumi wa kati. Kwa mantiki hiyo Tanzania bado ni nchi maskini hivyo Huduma bure za Afya ni ahadi ya uongo.

2. Ni mbinu gani mtatumia ndani ya siku mia moja kuifanya nchi iwe tajiri kiasi cha kufanya huduma za afya iwe bure?

3. Nchi kama Marekani, England, na nchi tajiri duniani hakunaga huduma bure za afya. Na kama itakuwepo lazima kuwa na udhibiti wa rapid population growth maana unawezaje kutoa huduma bure za afya kwa kinamama wanaojifungua kila mwaka?

4. Hivi unaposema utatoa huduma bure za afya uanaelewa kweli ulisemalo? Hivi unaelewa kuwa gharama za huduma ya afya ni kubwa kuanzia mwanafunzi anapoanza masomo ya huduma za afya, vifaa Tiba na madawa?

5.Unaposema utatoa huduma bure za afya hebu tuambie Tanzania kuna, viwanda vingapi vya madawa na vifaa tiba? India, China etc kuna viwanda vingi vya madawa na vifaa tiba, je kwao huduma za afya ni bure?

7. Mpaka sasa watoa huduma za afya wanapata shida kwa upande wa NHIF maana gharama zao ni ndogo, makato makubwa, kiasi cha kuathiri uendeshaji Bora wa huduma za afya huko private hospitals. Sasa ukisema utashorikiana na private sector kutoa huduma za afya si ndiyo itakuwa hovyo kabisa?

8. Ziko huduma unaweza kutoa bure lakini siyo huduma za afya. Huduma bure mashuleni is possible because you need black board, chaki na mishahara ya wafanyakazi. Daftari, vitabu, penseli, pen mzazi ananunua mwenyewe.

9. Wapinzani mnalalamikia wafanyakazi na wafanyabiasha kulipa kodi sasa mtatumia mbinu gani kukuza uchumi?

10. Mnapinga miradi mikubwa iliyoanzishwa na awamu ya tano na mkiingia Ikulu nihakika mtaifuta. Mradi mkubwa wa ujenzi wa bwawa la umeme, mradi wa train wa mwendo kasi, mradi wa ndege etc. Ni miradi inayotupeleka uchumi wa kati na baadae kutuwezesha kutoa bure Baadhi ya huduma. Sasa miradi hiyo yote mnaiponda, kwenu haina tija mtaipiga chini. Sasa kwanini Mnatoa ahadi za uongo kuwa utatoa huduma bure za afya?

11. Makinikia mnasema siyo ya kwetu, mnalalamikia ukuta wa Mererani, mnasema serikali isifanye biashara sasa mimi nashindwa kuelewa hiyo huduma ya afya itakayotolewa bure itakuwa na kubera gani.

Karibuni kwa majibu ya hoja zangu na siyo kwa matusi na mihemko!
 
Kwanza Hoja yako huna utafiti. Mi nilitegemea useme huduma hyo ya afya ulivyopiga hesabu ni trilion ngp kwa mwaka, kiasi ambacho hatuna labda. Pili huduma bure za afy n kwa hosptls za serikal kama mtu ataenda prvt hyo ni yeye mwenyewe mfn.elimu bure kwa msng na sec. Haihusu prvt schls ila kwa vyuo vipo ambavyo serikal inatoa mkopo.

Hiyo miradi mikubwa unayoisema je kuna mahal wamesema wataifuta? Au ni mhemko wako? Kinachogomba sio miradi tu ni wapi inafanywa, huwez kuacha kujenga uwanja ama soko la kimataifa Kahama ukaenda kujenga butiama lazma miradi iwe kwa faida sio maonyesho. Miradi iendelee ila mzunguko uwepo wa fedha.

Uchumi wa kati unaosemwa aliuelezea kikwete kwenye msiba wa Mkapa. Kwa sasa mtanzania anauwezo wa kupata dola 1100 kwa mwaka ila lengo lilikuwa iwe 3300 mwaka 2020 hivyo tumefka kiupandeupande
 
Kwanza Hoja yako huna utafiti. Mi nilitegemea useme huduma hyo ya afya ulivyopiga hesabu ni trilion ngp kwa mwaka, kiasi ambacho hatuna labda. Pili huduma bure za afy n kwa hosptls za serikal kama mtu ataenda prvt hyo ni yeye mwenyewe mfn.elimu bure kwa msng na sec. Haihusu prvt schls ila kwa vyuo vipo ambavyo serikal inatoa mkopo. Hyo miradi mikubwa unayoisema je kuna mahal wamesema wataifuta?...
Bado kwenye suala la huduma za afya bure ni impossible mkuu. Hata bila kufanya research kwa undani, face validity ya hii sera inajieleza kuwa anataka kura tu
 
Lissu amesema kila Mtanzania atakua na Bima ya afya ya bei nafuu na ataichangia. Si wote tutaumwa kwa pamoja hii inamaana pesa za wazima zitatibu wagonjwa.
hiyo hata obama marekani alishindwa nchi tajiri itakuwa kwa huyu kibaraka wa mabeberu wameshamdanganya wamemtosa hata kampeni hawamsaidii
 
Ccm inaaminisha watu kuwa Bima ya Afya maana yake ni huduma za Afya bure.....kwa bahati mbaya sana hii notion ipo kwa Watanzania wengi sana, unakuta mtu anafanya forgery atibiwe kwa BIMA kubwa then akawe refunded, sasa si umejiibia mwenyewe?

Bila ya Afya haimaanishi bure, ni pesa yako, ni akiba yako! Hakuna huduma za afya bure don't mislead people. Huu upupu kadanganyaneni kwenye yale magroup yenu ya CCM
 
Kwanza Hoja yako huna utafiti. Mi nilitegemea useme huduma hyo ya afya ulivyopiga hesabu ni trilion ngp kwa mwaka, kiasi ambacho hatuna labda. Pili huduma bure za afy n kwa hosptls za serikal kama mtu ataenda prvt hyo ni yeye mwenyewe mfn.elimu bure kwa msng na sec. Haihusu prvt schls ila kwa vyuo vipo ambavyo serikal inatoa mkopo...

Lb7 ana nini cha kusema zaidi ya kuimba nyimbo za mapambio?
 
Back
Top Bottom