Uchaguzi 2020 CHADEMA mkimsimamisha Lissu najiunga na chama chenu

Nikiangalia mwenendo wa kampeni unavyo endelea kwa kweli sijutii maamuzi yangu.
Kwanza nafurahishwa na jinsi Lissu anavyo mwaga Sera kwa ukweli na hadhi ya Presidential person tofauti na mgombea wa chama changu cha zamani asiyejua hata anataka kusema nini zaidi ya kuji contradict tuu.
Nimeshuhudia wanaccm wengi sana ninaofahamiana nao wakiwa wane KATA SHAURI KUACHANA NA DHAMBI YA CCM
Mkuu noana mgombea wa chama Chako cha zamani amebaki kutukana njia nzima kama mlevi wa gongo
 
Sera za Chadema in nzuri na pengine zinazidi za ccm. Hilo hata marehemu baba wa Taifa aliliona na kulitambua.
Tatizo lao walikuwa hawajapata MTU sahihi.

Walijidanganya kuwa Dr Slaa alikuwa mtu makini lakini ukweli yule hakuwa kama walivyo kuwa wanamdhania, mtu yeyote anayeiacha huduma ya kanisa au msikiti na kuja siasani ni wa kumuangalia mara mbili utajuwa tuu ni mpenda ya dunia na sio mkweli.

Kwa Lowassa ndio usiseme kabisa, it was a big mistake. Lakini Lissu nadhani anamuacha mbali sana mgombea wetu wa CCM.
Hata wao wanajua wanakaza shingo tu
 
Sera za chadema zilisifiwa pia na Nyerere, RIP. Wakati anafanya hivyo mwaka 1995 chama kikuu kilikuwa NCCR- mageuzi chini ya Lyatonga Mrema, Marando, Sengogo, Lamwai, Selasini, nk. Hivyo kama unamuheshimu Nyerere lazima utaheshimu na maoni yake pia.
 
Umechina Memba yuko humu toka long. Hizi sio Id fake mlizotumwa mataga
Hao ni wagumu kukubali ukweli. Ona mpaka bosi wao anapagawa jukwaani utadhani anafika kileleni?
Bado ndani ya siku hizi zilizobaki atapiga kelele "Nileteeni Lisuuu, nileteeni Lisuu" hadi watamnyang'anya mic wakijua tayari!
(Ona hapo chini clip )

Wakati nafanya maamuzi haya sikujua kama mawazo yangu yalikuwa ndani ya mamilioni ya washabiki wa CCM wengine. Lakini majuzi nikiwa kwenye shughuli zangu Kahama nilichoshuhudia kwa macho na kusikia kwa masikio yangu tena nikiwa sijagusa ka bottle ka jioni nikajiambia SASA BASI TENA CCM, imekwisha! Kama wapo wanaccm waliobaki huko ni wale waajiriwa kwa maana ya ajira ya Chama au paid vuvuzelas.

 
Back
Top Bottom