CHADEMA mkijipanga vizuri mnaweza ipindua ACT Wazalendo visiwani Zanzibar

Cathelin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,071
3,992
Ukweli ni kwamba Wazanzibar Sasa wanaona the way ACT Wazalendo alivyo,, hana tofauti na CCM.

CHADEMA mkiwekeza Zanzibar,,mkaubiri haki,, na matatizo pamoja na suruhisho la muungano mta-win Sana Zanzibar.

Kumbuka last year, speech moja ya Lissu uko Pemba, ilifanya wazanzibari wamchague sana Lissu. Kitendo Cha ACT Wazalendo kuwa wanafiki na kukumbatia uovu wa CCM, kimepunguza imani kwa wazanzibari.

CHADEMA nenda Zanzibar mtakuwa Giant party Kama uku bara.

IMG_20210920_124631.jpg
 
Chadema hawana mipango ya muda mrefu wanawexa kuanza na huu mchakato wa kuichukua Zanzibar ila wakatoka relini rais akichukua likizo ya mwezi Zanzibar. Wakaanza jadili kuhusu likizo huko Clubhouse na Space wakimaliza wanalala wanasahau ajenda ya mwanzo ilikua ni nini
 
CCM ndo Wana mipango??
 
Usiwapote
Ukweli ni kwamba Wazanzibar Sasa wanaona the way ACT Wazalendo alivyo,, hana tofauti na CCM.

CHADEMA mkiwekeza Zanzibar,,mkaubiri haki,, na matatizo pamoja na suruhisho la muungano mta-win Sana Zanzibar.

Kumbuka last year, speech moja ya Lissu uko Pemba, ilifanya wazanzibari wamchague sana Lissu. Kitendo Cha ACT Wazalendo kuwa wanafiki na kukumbatia uovu wa CCM, kimepunguza imani kwa wazanzibari.

CHADEMA nenda Zanzibar mtakuwa Giant party Kama uku bara.

View attachment 1971884
Usiwadanganye wenzako

Act -wazalendo wanatumia diplomatic kuikomboa Zanzibar
Chadema wanatumia force kuikomboa Tanganyika

Kila moja hana mpango na eneo la mwenzake kwasababu hakuna aneamini katika Muungano
 
Chadema haina wanasiasa watulivu wenye kutafakari bila jaziba .

Siasa za Zanzibar hazihitaji unafiki kama unaofanywa na vijana wa Chadema wanaotokea bara. ACT imebebwa na Vijana wa CUF waliokua wamejenga siasa za itikadi sio unafiki wa kutafuta maslahi.

Kwanza Zanzibar hakuna kufukuzana fukuzana kwenye siasa na misimamo yao ya kuipinga CCM .
Huku bara wanasiasa ni wafanya biashara wasaka vyeo.

Nikimkumbuka Nasari, Jobu Lusinde, Lijuakali, Katambi, Mwita, Mdee, Bulaya n.k. naogopa sana siasa za Bara.

Zanzibar ni tofauti sana. Zito Kabwe ni mjanja sana na ni akili kubwa sana anayoutumia kutafuta opportunity za kisiasa.
Chadema ina vijana wenye akili sana lakini wana dharau kila MTU .
Huu ni usomi wa kijinga na ndio unaowaharibu waafrika.
Waafrika wa zamani waliosoma walikua wapumbavu na ndio waliolivuruga bara letu na kulifanya liwe nyuma pamoja na kuwa na wasomi wengi wenye akili za vyeti.
Msomi maki ni yule anayepata elimu yake kwa kuwatumia wasiosoma. Ukitaka ujue masisha ya watu wa vijijini lazima ujishushe uishi kama wao. Watakueleza kila kitu.
Leo hii wasomi wa kizungu wanajua maisha ya waafrika na mila zao kuliko wasomi wetu wa leo.
Hata Twiga kule mikumi anavyozaa , tunapata taarifa zake toka kwa wazungu huko ulaya mana wanatumia muda wao kuwasoma wanyama na kila kiumbe. Waafrika akisha kuwa na digri moja au mbili basi hataki hata kukaa kwenye kijiwe cha wauza kahawa na kupiga nao stori ya maisha ya kawaida. Utawakuta wasomi wetu muda wote wapo kwenye baa wanalewa na kuongelea mambo ya madili na wanawake tuu. Wakiwa wanasiasa ndio hivyo hivyo hata vyeo wanapeana kwa rushwa ya ngono na kwenye ulevi.

Zanzibar hali ni Tofauti kabisa kwani wale wasioipenda CCM ,hawsipendi kwa itikadi na kwa matendo maovu yanayofanywa na CCM. Huku bara ,Leo Msomi kama Ally Happy alikua Mpinzani mkubwa na mhamasishaji maandamano alipokua chuoni lakini baada ya kupata fursa ndani ya CCM akageukana na kuwa adui mkubwa wa wakosoaji wakati Sera kandamizi alizokua anazipinga ni zile zile.
Polepole ,Kabudi, Bashiru n.k. Watu kama hawa hawapo Kule Zanzibar.

Na hata Mama Samia ni tofauti sana na Waovu wa Bara waliokua wanawaza kuwa kama miungu kwenye jamii kwa kujilimbikizia Mali na kuwa na madaraka makubwa na kuogopwa kama miungu.
Dini yao pia inasababisha kuwa na siasa za tofauti na bara.
Ubinafsi umewajaa wabara bila kujali vyama vyao.

Zito kabwa aliwapa Wazanzibari uongozi wa Chama cha ACT kwa adilimia kubwa sana jambo ambalo Chadema hawawezi.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Chadema hawana mipango ya muda mrefu wanawexa kuanza na huu mchakato wa kuichukua Zanzibar ila wakatoka relini rais akichukua likizo ya mwezi Zanzibar. Wakaanza jadili kuhusu likizo huko Clubhouse na Space wakimaliza wanalala wanasahau ajenda ya mwanzo ilikua ni nini
Hawana mpango mrefu? Unadhani chama kiliwezaje kuwa na msingi kuanzia Kinondoni hadi Buhigwe huko?? Mbowe alifanya sourcing ya watu wenye influence na potential ile 2004-06 na ndio imefikisha chama hapa.

Kuhusu Space na clubhouse hiyo ni part ya long term strategy yaani CHADEMA digital inayohusisha kutumia nguvu ya mitandao kuinfluence masuala ya chama. So kma mikutano hairuhusiwi lakini clubhouse ya CHADEMA ina wasikilizaji zaidi ya elfu 2 kila siku unadhani sio platform nzuri?? Hasa miaka hii ya digital?

Lissu mikutano yake watu walikaribishana na kuhamasishana kwa whatsapp/FB Messenger maana hta media zilikua hazitoi updates zozote!!

Mtu anayedhihaki matumizi ya teknolojia karne ya 21 ni embicile!!
 
Unajidanganya Mzee..

Lisu hakupata kura kwa Sera zake, Bali kupigiwa chapuo na hao ACT ikiongozwa na Maalim (Mungu amlaze mahala pema)
 
Back
Top Bottom