CHADEMA, Mkienda vijijini msivae ki mgambomgambo. Wanakijiji wanaogopa MAGWANDA kuliko MAGAMBA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Mkienda vijijini msivae ki mgambomgambo. Wanakijiji wanaogopa MAGWANDA kuliko MAGAMBA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Dec 10, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tangu ulipoingia mfumo huu wa vyama vingi nchini. Wananchi wengi wasio na elimu hasa vijijini walipandikizwa imani kuwa vyama vingi husababisha vita. Ndio maana kumekuwa na wimbi la mabadiliko mijini kuliko vijijini ambako kuna wapiga kura wa kweli wengi zaidi. Wengi wa wananchi vijijini wanachukulia uvaaji wa CDM kama dalili za kuwepo kwa jeshi lisilo rasmi nchini. MAGWANDA yanawatisha na kuwajengea hofu kuwa, pengine chama hicho kina dalili za ushari. Nawasihi makamanda wa CDM kuwa, wakati umekaribia sana kwa maana hiyo wajaribu kubuni mbinu itakayowapatia wafuasi wengi hasa kutoka vijijini. Kwa kweli MAGWANDA ya makamanda yanatishia sana amani. Hebu yavueni mwende kwa wafuasi wenu mkiwa mmetinga suti.
   
 2. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwani mavazi yanafanana na matendo ccm wanavaa suti huku wanaiba pia wanatumia police kuuwa watu sijawahi kusikia cdm wameuwa mtu
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo Wassira na Mizengo hata wakivaa kama Papa huwa hawaachi kumtisha mwanangu anapowaona kwa TV.
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Sio wanavijiji wa leo, hata wao wameamka, wanajua jinsi magamba wanavyowaibia na wanajua magwanda ni kwa ajili ya kung'oa magamba na kuleta ukombozi wa kweli. So Chadema nendeni vijijini na magwanda yenu.
   
 5. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ha ha ha..JF ni burudani tosha
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kweli unachosema ni ushauri wa ujenzi, wanavijiji wanaweza kudhani kodi ya kichwa imerudi...
   
 7. M

  Mughwira Senior Member

  #7
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2008
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Usidhalilishe waTZ wanavijiji gani unaowazungumzia ambao hawezi kutofautisha? CDM wanakubalika sana vijijini fanya utafiti kidogo kabla ya kuweka upupu hapa.
   
 8. j

  janejean Member

  #8
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kweli, wanavijiji siku hizi wanajitambua. Na kama hauamini, angalia Rais amewai kurushiwa mawe msafara wake vijijini
  na mikoani. lakini wa mjini wanakubali kukaa foleni masaa hadi manne kusubiri waheshimiwa wapite. wavijijini hawaogopi kuliko wamjini. Labda wavue wakiwa wanahutubia mwembe yanga au jangwani!!!
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,278
  Likes Received: 19,430
  Trophy Points: 280
  hii point mtaipuuza lakini inaweza kuwa ina effect kubwa sana .....hivi kweli chadema kuna wanasaikoligi wanaoenda na kusoma watu hasa huko vijijini juu ya chama chao?
   
 10. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #10
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sio upupu, huo ndio ukweli. Nimepita vijiji vingi tofauti na unayodhani. Nimefanya kazi huko pia, watu bado wana fikra mgando. Huo ndio ukweli! Huwezi amini mpaka sasa kuna wazee wanaamini Nyerere bado yupo hai. Au kwa sababu ushazoea maharagwe ya mjini mambo hayo hujawahi kuyasikia. Nyie mafuasi ya CDM sijui akili zenu zikoje!
   
 11. M

  Mughwira Senior Member

  #11
  Dec 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2008
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kijiji gani ulipita au ulifanyakazi kiweke hapa, wewe unaleta mambo ya kufikirika, au hisia zako zinavyokutuma ndo unafikiri watu wote wa Vijijini wako hivyo.
   
 12. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  OMG., Mwita25 hivi zimo kweli ww., duh kama umenifanya hadi nimepaliwa na mate..:poa:poa:poa
   
 13. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #13
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nenda na magwanda yako huku huko Ipande, Muhanga, Kanamalenga, sasilo, Sasajali, Kinangali, London huko Manyoni milimani kama watakuelewa. Nenda Kubi, Makanda, Lamaiti na hayo magawanda yako kama watakuelewa. Nenda Mpwapwa ndani huko Godegode, Mgoma, Mzogole, Mima kama watakuelewa. Tatizo lako wewe kwa akili yako ndogo kama mbegu ya pera unadhani vijiji ni vile vilivyopitiwa na barabara kuu tu.
   
Loading...