CHADEMA, mkichukua mkopo wa gari mil 90, hamna tofauti na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, mkichukua mkopo wa gari mil 90, hamna tofauti na CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uswe, Feb 15, 2011.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nimesikia ule utaratibu wa kukopeshana mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kununua magari ya kifahari unaendelea, kama kuna wakati wa kuwaonyesha watanzania njia kwa vitendo ni sasa, hata kama ni mkopo hiyo ni sumu, nasubiri kwa hamu kusikia chadema wanaamua nini katika hili. kama wakikubali hizo mil 90 kila mmoja eti kwa kununulia magari, basi A, B na C yote ni majibu sahihi, i mean CCM, CUF na CHADEMA hamna tofauti
   
 2. b

  binti ashura Senior Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wabunge wetu wanakopa magari ya mamilioni mengi ili wakianza kukatwa mikopo wajiongezee mishahara kwa kuona pesa wanazozipanta ndogo. nchi hii haya tutafika tu!.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Chadema ndio Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Chadema ndio wameunda Baraza la Mawaziri kivuli, Chadema kimepigiwa kura nyingi na watanzania kama chama imara na mkombozi wa wanyonge, Chadema kama chama imara kimekataa kushirikiana na vyama vingine sababu wanataka waunde Upinzani imara Tanzania. cha ajabu zaidi Wabunge wote wa Chadema wameishalipwa kila mmoja milioni 90, baada ya kupokea pesa eti wanashanganzwa na hatua ya Rais Kikwete kuweka (BAJAJI) kama moja ya vipaumbele vyake, Wananchi wa Tanzania waliowapa kura wanataka wapewe maelezo ya hizo pesa za Wabunge jinsi watakavyozitumia hata kama ni mkopo, milioni 90 ni pesa nyingi kwa gari ya Mbunge
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Huu ni mkopo katika maana kwamba fedha yote itarudishwa,sioni tatizo liko wapi.

  Si wote wanao kopa hizo 90,000,000.00 wanaishia kununua hayo magari mazito kama akili ya mbunge inafanya kazi vizuri only 30,000,000.00 inatosha kununu gari zito jipya la 4 wheel.

  Huu ni mkopo labda uniambie si mkpo na hakuna mbunge mwenye mpango wa kurudisha fedha hiyo.

   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Lini ulifahamu kuwa watu wanakimbilia siasa ili kuwasaidia wanyonge? walalahio? watu wa kawaida?
  Huelewi kuwa kwa TZ siasa ndio short cut ya kuganga njaa?

  Halafu CCM ni magwiji wa mikakati ya kuwachakachua hata wale wachache ambao wanaonekana ni watu safi...njia moja wapo ndio hiyo.Niambie nchi yenye shida ya kila kitu kuanzia umeme, maji, barabara, mahospitali na zahanati nk leo wana pesa za kumwaga kama hizo kwa wabunge!!!
  TZ mkuu ni zaidi ya tuijuavyo!
   
 6. U

  Uswe JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Madela inaonekana hujui finances inavofanya kazi, hata kama ni mkopo bado ni tatizo, kwani wale wanafunzi wa chuo si huwa wanapewa mikopo, kwa nini wote wasipewe 100% kwani si watarudisha, tatizo liko wapi? milioni tisini kwa kila mbunge ni zaidi ya 3.2bn, hakuna kitu kingine cha maana cha kufanya na hizi pesa (ambazo ni kodi yako na yangu) zaidi ya kumkopesha mbunge? hii haijakaa vizuri, kwa kuchukua hizi wabunge wa chadema wametusaliti
   
 7. Davesto

  Davesto JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 60
  **** all tz politicians
   
 8. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  CDM hawatengenezi sera, wao wanaongozwa na sera za ccm ambazo zinatoa hizo mil 90. Hizo pesa ni za kukopeshwa, na tayari zilishatengwa kwa ajili ya kazi hiyo, hata wakizikataa hizo fedha zitaenda wapi? Je zitarudi hazina? au zitabaki ofisi ya bunge? kwa kuwa si chadema ambao wanadhamana ya kuzitunza hizo fedha,tunauhakika gani kuwa hazitaishia mikononi mwa watu?

  Kukataa hizo fedha si suluhisho,hakutasaidia chochote, Lakini tujue kuwa hizo fedha hawajapewa chadema kama chama,bali mbunge kama mwakilishi wa wananchi, hivyo sidhani kama kuna mamlaka yoyote ambayo CDM kama chama kinaweza kufanya juu ya suala la mbunge kama mwakilishi wa wananchi, bali ni mbunge mwenyewe aamue.

  Naunga mkono kwamba hizo pesa ni nyingi sana kwa mazingira yetu ya kiuchumi, Lakini kwa wabunge wa chadema kukataa itakuwa siasa za kitoto, na tusiwalaumu maana wao hawana maamuzi ya kisera katika serikali.
   
 9. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hili nalo ni Neno, tena la maana
   
 10. U

  Uswe JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  my take, Ni lazima kuongoza kwa vitendo!
   
Loading...