Chadema mjipongeze kwa kuwa chama kikuu cha upinzani, ni hatua nzuri.

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
Kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania, ni kama ushindi kwa chama hiki cha CHADEMA na kwao ni hatua nzuri kimafanikio katika siasa.

Hatua hii waliyopo CHADEMA kwa sasa imeshakaliwa na vyama kadhaa vya upinzani huko nyuma, lakini vilishindwa kuhimili mikiki miki ya kiushindani na kujikuta vikipoteza mvuto wake kisiasa.

CHADEMA jitahidini sana maana ushindani katika hatua hiyo ya kubaki kuwa chama kikuu cha upinzani sio mwepesi. Maana CUF, NCCR na TLP kila kimoja kinapigana kurudi katika hiyo nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani.

Rai yangu kwa CHADEMA, huku CCM hatuna shaka na kukubalika kwetu hasa na watu wa vijijini, kukubalika huku kuna tuhakikishia kubaki madarakani kwa karne, kutokana na hilo basi, CHADEMA jitahidini muendelee kuwa chama kikuu cha upinzani, ndiyo ushindi wenu huo.
 
kuwa chama kikuu cha upinzani tanzania, ni kama ushindi kwa chama hiki cha chadema na kwao ni hatua nzuri kimafanikio katika siasa.

Hatua hii waliyopo chadema kwa sasa imeshakaliwa na vyama kadhaa vya upinzani huko nyuma, lakini vilishindwa kuhimili mikiki miki ya kiushindani na kujikuta vikipoteza mvuto wake kisiasa.

Chadema jitahidini sana maana ushindani katika hatua hiyo ya kubaki kuwa chama kikuu cha upinzani sio mwepesi. Maana cuf, nccr na tlp navyo vinapigana kufika katika hiyo ya kuwa vyama vikuu vya upinzani.

Rai yangu kwa chadema, huku ccm hatuna shaka na kukubalika kwetu hasa na watu wa vijijini, kukubalika huku kuna tuhakikishia kubaki madarakani kwa karne, kutokana na hilo basi, chadema jitahidini muendelee kuwa chama kikuu cha upinzani, ndiyo ushindi wenu huo.

hicho ki-machine cha kutengeneza, kupiga, na kuhesabu kura kiko kwako nini.....!!!!!
 
hicho ki-machine cha kutengeneza, kupiga, na kuhesabu kura kiko kwako nini.....!!!!!

Hatuna haja ya kimashine chochote kile, sera zetu, itikadi ya CCM na malengo ya CCM ndio yana fanya wananchi wawe na imani na matumaini kwa CCM kuliko vyama vingine vya siasa.
 
Unavyohangaika mpaka nakuonea huruma.

Molemo, nimekwambia CCM hatuna shaka na umaarufu na kukubalika kwetu.

Wewe ndie utulii, na kikubwa ni matokeo yatakayo yatangazwa katika chaguzi ndogo zinazo endelea, msubiri na mtulie kupigwa za uso.
 
Last edited by a moderator:
Anahangaika huyu! Amekalia cha wana Arusha nini?

Deshmo, jipongezeni jamani, nafasi mliyo ifikia ya kuwa chama kikuu cha upinzani si haba, ila tu kazaneni maana CUF et al nao wanataka kuchukua nafasi hiyo hiyo.
 
Last edited by a moderator:
Hatuna haja ya kimashine chochote kile, sera zetu, itikadi ya CCM na malengo ya CCM ndio yana fanya wananchi wawe na imani na matumaini kwa CCM kuliko vyama vingine vya siasa.

WanaCCM tuambiane ukweli "Ni hatari sana maskini anapochoshwa na kusema namwachia mungu, kwani chochote chaweza kutokea, NI tofauti na matajiri ambao hutumia pesa kunusuru hali." Unajisikiaje kuendelea kusema sera ndizo zinazoendelea kukiweka chama madarakani hali ya kuwa unasikia kila kona CCM wanakamatwa wakigawa rushwa na kununua kadi za wapiga kura?. Kwa kuwa huo ndio mtaji wa Chama Nadhani njia nzuru ya kukomesha hizo rushwa ni wananchi kujichukulia sheria mikononi kuwa kila atakayekamatwa akigawa rushwa / kununua kadi iwe ndio mwisho wake LA SIVYO rushwa ihalalishwe na iwe ni moja ya zana katika kushinda chaguzi. Wengine tuendelee kusikilizia nini hitimisho la Matajiri watoa rushwa na Maskini waliochoshwa na uduni wa maisha huku wakidanganishiwa rushwa.
Inakera sana unapoambiwa Serikali inapinga rushwa huku wao ndio wanaongoza kutoa rushwa.
 
HAWEZI KUWA DAKTARI KILAZA NAMNA HII MIMI NNKATAA HUYU NI KILAZA WA CCM TU KAMA KILAZA WENGINE HAMNA DAKTARI mwenye akili za ajabu namna hii...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom