Chadema mikutano ya nini?

Zhu

Senior Member
Sep 26, 2010
184
24
Uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kutekeleza ahadi tulizo ahidiwa. Si mda tena wa kampeni wala propaganda. Watanzania bwana. Badala ya kuchapa kazi we use a lot of time discussing problems rather than solution. Jf mnasemaje.
 
Kinachokufanya uulize ndicho kinachopelekea chadema kufanya mikutano, mbili chadema ni chama cha siasa kipo kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, tatu uchaguzi uliomalizika kama ulivyosema una kasoro nyingi kwa maslahi yako na taifa kwa ujumla chadema lazima iwaele watanzania nini kinaendelea nini kifanyike, nne chadema ina amini katika nguvu ya umma people's power, tano kazi unayodai ifanyike baada ya uchaguzi kufanyika haikuanza leo -tuhitaji mijadala ya kuwafanya waliolazimisha utawala masultani na walioteuliwa na sultani wawajibike kwa wananchi sio kwa maslahi ya sultani. Kama wewe ni raia mzalendo utakubaliana nami kuna haja ya mikutano na ni kwa kuhofia kuumbuliwa na kuingiza michanga vitumbua vya masultani wanapiga vita mikutano kinyume na katiba.

Nategema kwa majibu haya altitude yako imebadilika kama hujatumwa na sultani na kwamba utahudhuria mikutano -ukizingatia kuwa siyo watanzania wote wana access na jamii forum kuhabalishwa kama wewe, kwnini usifanye kazi badala yake unakodolea macho jf? Vivyohicyo ndio watanzania wengine wanahitaji mikutano.
 
Wee Zhu unafahamu kazi ya siasa. Chama cha siasa ni kupiga siasa mchana na usiku. Kama CDM wakikaa kimya basi ndiyo mwisho wa siku tutaanza kusikia wanaambiwa na vyama vya musimu. Kama chama cha siasa lazima watafute agenda itakayo wapeleka kwa wananchi ili waonekane wanafanya kazi. Hivi sasa CDM ndiyo agenda zao hizo wameweka wazi. Nafikiri kwetu sisi hapo ndipo tunapata maendeleo.
 
kwa hiyo unashauri kwamba uchaguzi umekiwsha ofisi za vyama vya sisa pia zifungwe!
 
Uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kutekeleza ahadi tulizo ahidiwa. Si mda tena wa kampeni wala propaganda. Watanzania bwana. Badala ya kuchapa kazi we use a lot of time discussing problems rather than solution. Jf mnasemaje.

Is this not MS????????????
 
Achana na hawa wachumia tumbo wa CCM a.k.a Chaka Chua Matokeo. Wao huwa uwakilishi wao uko bungeni na sijui huwa wanatumwa na nani huko! Wajinga hawa hata hawaelewi kwa nini lazima kuwe na mikutano hata ikiwezekana kila siku. Hiyo ndiyo kazi. CCM wamezoea wakishachanguliwa hao kwenye mashangingi hadi 2015 utaona wanakuja mbio mbio. Kama si hivyo sasa hivi utasikia wameanza zile kelele zao kwamba kuna watu wameanza kunyemelea majimbo yao. Hovyoooooooooooo
 
Mwanzo na JM mlisema vyama vya upinzani ni vya msimu tu sasa leo hii mnaona vinaendelea na kutokuwa vya msimu tena. Hapo ndio viroho vinawauma lakini Nini maana ya Chama cha Siasa? au mlitaka kundelea na dharau zenu kuwa Vyama vya upinzani ni vya wakati wa uchaguzi tuu?

Mtatia akili ukimuamsha aliyelala ujue unausingizi wa kulala wewe!
 
Uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kutekeleza ahadi tulizo ahidiwa. Si mda tena wa kampeni wala propaganda. Watanzania bwana. Badala ya kuchapa kazi we use a lot of time discussing problems rather than solution. Jf mnasemaje.

Unadhani kazi ya mwanasiasa ipo wakati wa uchaguzi tu? Akiacha siasa akafanye nini kama siyo kukutana na wananchi wake wapange mipango ya maendeleo.

Zhuzhu mafisadi wanakulipa ngapi kwa kila thread unayo toa?
 
Uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kutekeleza ahadi tulizo ahidiwa. Si mda tena wa kampeni wala propaganda. Watanzania bwana. Badala ya kuchapa kazi we use a lot of time discussing problems rather than solution. Jf mnasemaje.
Hujui majukumu ya chama cha siasa au unajifanya kuwa huyajui, kwenye maisha ya siasa kila dakika ni siasa, siasa haina likizo hata huo utekelezaji unaousema ni siasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom