CHADEMA, Mgogoro wa Ruzuku mikoani ni bomu la kulipuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Mgogoro wa Ruzuku mikoani ni bomu la kulipuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Jun 11, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nimewahi kulizungumza hili juu ya muelekeo wa CDM hasa katika ngazi za mikoa juu ya mgawanyo wa ruzuku.Wengi wakapuuza na wengine kunikejeli eti ''magamba'', kama ilivyozoeleka humu kwa wapambe wasiotizama mbele kuna nini!.

  Kinachosambaratisha vyama vya siasa hapa Tz kwa sehemu kubwa huwa ni migogoro ya mgawanyo wa mapato (ruzuku) kutoka juu hadi ngazi ya shina ama kata.

  Ruzuku hii inapaswa kuelekezwa kwa kiasi kikubwa huko kwenye wanachama ili kuwezesha uhamasishaji (usafiri,ofisi,na vitendea kazi vingine)na si fungu kubwa kubakia headoffice ambako shughuli kuu ni paper works na si field hapa pana posho za vikao visivyokwisha pamoja na mishahara.

  Kumeanza kuzuka manung'uniko juu ya jinsi gani hali inavyotajwa kuwa bado haijatengamaa kimapato ndani ya chama,wakati ruzuku inayotolewa sasa ni kubwa kuliko ya vipindi vyote vilivyopita vya uhai wa chama. Mikoani na wilayani imekuwa pangu pakavu,ntilie mchuzi huku headoffice watu wananawili tu.

  Hii hali inajenga vishawishi kuwa ndani ya chama kuna wateule,na watwaliwa na wengi kuanza kumkumbuka Marehemu Chacha Wangwe kwa kupambana juu ya mgao wa ruzuku mikoani. Hizi pesa kidogo zisipotazamwa itakuwa kiini kikubwa cha kusambaratisha hiki chama. Wimbi la kuanza kukimbia kwa baadhi ya viongozi wa CDM ni dalili tosha ya muelekeo wa chama hiki yaani kufa, kwani ni mapema mno toka uchaguzi uishe.

  Viongozi wengi wa wilayani wamekuwa na manung'uniko yasiyo kwisha na pengine kuanza kubwabwaja na kusababisha tusio husika kupata nyeti hizi.CDM hakuna uzalendo pasipo na uzalendo. Huwezi kusema hali mbaya chini huku juu mnalipana na mambo yenu yanasongo eti ndipo chama kinaimalika. Mtaendekeza huu utaratibu wa uhamasishaji kufanywa na wabunge na viongozi waandamizi mpaka lini?.

  Hawa wabunge wana majimbo yao na wanahitajika kuwatumikia wananchi wao pia. Kukosa umakini juu ya hili watajikuta wanapoteza pia nafasi zao, hii na maana ya kwamba wananchi ambao ni wanaCDM na wasio na chama ila wapiga kura hawatokuelewa mwaka 2015 kuwa hukuwapatia maendeleo kwa sababu ulikuwa Namtumbo katika shughuli za chama.

  Kuondoa masahibu haya Chadema ifikirie kupunguza pia marupurupu ya viongozi waandamizi ili kuelekeza nguvu chini. Najua itakuwa shida sana hasa Wabunge kuizira posho ya vikao. Hapa ndipo hali itachafuka zaidi kwani kila mmoja atakunja mkono wake na hata safari za Wabunge katika maandamano zitapungua. Nadhani tunatambua kuwa wamekuwa wakidai wanajigharamikia wenyewe katika ziara.

  Uwepo wa posho hizi kwa CDM ilikuwa msaada mkubwa kama wangejua jinsi ya kuzitumia,cha ajabu Zitto kaongoza kuwatia kitanzi huku yeye akijua namna gani atasurvive. Hili suala la Uzalendo wake linanipa mashaka kwani ni muda mrefu amekuwa akizipokea labda ni bora zaidi akajisahihisha na kurudisha hata zile alizokwisha chukua.

  Hili si la kwangu ni la wabunge wenyewe wa CDM kuamua kunyoa ama kusuka.Ila tutambue kipato kikipungua ndani ndipo ugonvi huanzia na hatimaye kutengana. CDM itambue kuwa hawa viongozi wa chini wasipo tizamwa vizuri ili kuboresha utendaji wao, watapukutika kama inavyoanza kutokea.

  Hii support ya vijana kutoka vyuoni haina tija kwa sasa. Wengi mbali na ushabiki hawako tayari kujivika nafasi hizo zisizo na kipato cha kukidhi maisha yao. Wengi wanakimbilia kutafuta ajira zenye kipato kulingana na vyeti vyao. Hii ni sahihi kama uongozi ndani ya CDM hakuna mshahara ama haukidhi nitaishije kwa maana ya kupata rizki yangu (ugali) kila siku huku nikiendesha shughuli za chama? DR. Slaa bila mshahara ama posho hata yeye angeishirizia kukata tamaa.

  Haya ni maoni yangu,mimi si Mwana CDM wala shabiki wa chama chochote na hii hainizuii kukikosoa CDM wala CCM au CUF. Ukiwa mtazamaji mara nyingi ni rahisi kutambua makosa ya kila mmoja uwanjani na hata ya refa mwenyewe.
   
 2. M

  MPG JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kijana wa NAPE yupo kazini ,haya baba hongera naona unafikiria kwa kutumia makamasi badala ya ubongo,haya nenda ofisi za CCM ukachukue posho kwa kazi uliotumwa ya kuja kuleta upuuzi wako.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Apolycaripto, mtazamo wako uko huru kabisa na ni mchango madhubuti kwa wahusika kama wana macho ya kusoma, akili ya kuelewa, masikio ya kusikia na mikono ya kutenda.
   
 4. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  noted, lazima wajirekebishe haraka, ofisi za wilaya zitengeneze bajeti zao na ziwe allocated mapato ya ruzuku kutokana na mission zao na ziwe audited mara kwa mara, na chadema waweke wazi mgawanyo wa matumizi ya RUZUKU unless otherwise hatutawaelewa kama ccm
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Binafsi ningeshauri viongozi wakuu wa CHADEMA wasipuuzie haya yaliyoandikwa. Ni vizuri Head office wawe na mawasiliano ya karibu kabisa na kuwaelimisha walio mikoni juu ya matumizi ya ruzuku. CCM wanatumia hii hoja ruzuku kueneza sumu mikoani na wasiwasi wangu ni kwamba hata kama hakuna ukweli lakini in the absence of information basi hii inaweza kuwa the 'weakest link' kwa CHADEMA.
   
 6. M

  MPG JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulishaomba kupewa mgawnyo wa RUZUKU katika mikoa ukanyimwa kuambiwa,CHADEMA wamefanya mikutano hivi karibuni waliweka wazi,then dr katika kufanya makongamano na wanafunzi wa vyuo vikuu mikoa mbarimbari kama IRINGA,alieleza kila kitu mgawanyo wa hayo mapato na jimbo lenye kupata RUZUKU kubwa ni UBUNGO,Sasa sijui unataka kipi kingine
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Jibu hoja na si utumbo.
  Oo Nape yupo kazini, Nape Yupo kazini
  Wizi mtupu
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ina maana chadema ile sera ya majimbo hawaitekelezi kwa vitendo mambo mambo yako tooo centralised??????

  Laini vyovyote vile dar itabaki kuwa dar. hata CCM CUF na hata serikali yenyewe ndo ilivyo. Ndo maana ya neno makao makuu.


  kwani kila mkoa unapata kiasi gani kama ruzuku kwa ajili ya kujiendesha???? ebu tupe data japo mgao wa mikoa au wilaya kama tano.
   
 9. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni hoja nzuri japo aliyeanzisha ameileta kimagambamagamba, mimi ninacho jua hakuna hujuma yoyote na kwa ofisi hizo za mikoani ila la msingi ni ilo taarifa ni kitu muhimu sana, nawaombeni viongozi wa huko mikoani na wilayani msimpe nafasi ibilisi, vuteni subira CDM ufisadi ni mwiko mukiona mambo ni kama hayaendi sawa basi kutakuwa na vipaumbele vingine the na ilo litafuata
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Haya sio masuala ya kusubiri kujibiwa toka makao Makuu. Kila jimbo linapata ruzuku sawa sawa na mchango wake katika uchaguzi Mkuu wa Okotoba 2010. Ruzuku hizi zimeanza kutolewa tangu Januari 2011. Kama kuna jimbo ambalo halipati ruzuku basi ni ama hawajafungua akaunit (pesa yao ipo tu makao makuu) au Uongozi wa kikatiba haujapatikana i.e kuna viongozi wa muda. Zaidi ya hapo hizo ni porojo tu
   
 11. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Katiba ya Chadema inatoa mamlaka makubwa kwa Majimbo (ya uchaguzi) na huko ndiko kwenye nafasi ya mtunza Hazina. Kikatiba ruzuku inatakiwa kuelekezwa huko na ndivyo inavyofanyika, kwa kila jimbo kupata kulingana na mchango wake katika matokeo ya uchaguzi mkuu.
   
 12. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena! Ila ukweli ni kwamba kama kuna jimbo halina rurzuku basi ni kwa sababu hakuna uongozi wa kikatiba au jimbo husika halijawasilisha akaunti makao Makuu. Ila fedha za Majimbo yote zipo tangu Januari 2011. Tusipotoshe umma kwa maslahi binafsi
   
 13. j

  jnuswe JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,271
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  tunashukuru mkuu kwa kuliweka sawa hilo, maana magamba wamekosa hoja ,wanaweza kutumia mwanya huo kwa wasio jua utaratibu wa ruzuku hizo
   
 14. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Mimi nilikuwa Katibu wa Jimbo mojawapo so najua ninachokisema hapa. Na wakiendelea kuleta porojo hapa watutajie jimbo gani halipati hizo pesa na sisi tutaweka hapa stahili za jimbo husika kulingana na mgawao toka makao makuu
   
 15. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  MPG usiichukulie cdm kama Wakristo na Fumbo la Utatu Mtakatifu lisilohojiwa, na wala usiwafikirie viongozi wa cdm katika ngazi za Umalaika kwamba hawawezi kupitiwa na mambo ktk mipango na utendaji. Bali kama unataka kuwa wa msaada kwa cdm fanyia kazi au fikisha changamoto, maoni na mapendekezo kwa wahusika. Pia jitahidi kujiweka huru na ushabiki unaoweza kuifanya akili yako na utashi zana butu. Hii ndiyo hali inayowafanya hata Vipanga/intellectuals wa ccm kuonekana vilaza.
   
 16. M

  MPG JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hufatilii, CHADEMA wamefanya mikutano yao hivi karibuni,moja ya sehemu hiyo ni nyanda ya juu kusini, na walieleza yote,na katika kufanya vikao na wanafunzi wa vyuo vikuu vya IRINGA DR alitoa mchanganyuo wote wa mapato unavyogawiwa na aliyesoma huo mchanganyuo ni BWANA BENSON nadhani unamfahamu na jimbo linalopata RUZUKU kubwa ni UBUNGO, na walitoa sababu ya kupata RUZUKU Kubwa.

  Na swala la ofisi za mikoani wameshaanza kulifanyia kazi, tatizo lililokuwa linawakumba ni kwamba wapangishaji walikuwa wakitishwa na Serikali kuwapangisha CHADEMA kwenye majengo yaliyo bora kwa hiyo kwasasa CHADEMA kwa mchakato wa ofisi za mikoani kuwa na ofisi bora wanafanya kwa siri kubwa, mfano IRINGA mwanzo walipata OFISI kubwa na bora lakini mpangishaji alikuja kutishia na watu wa Usalama wa TAIFA ambao wengi wao ni CCM kwa hiyo huyo mtu akaogopa,ila kwa habari nzuri kwa hapa IRINGA CHADEMA watahamia kwenye Jengo bora mwezi wa Nane huyo mpangaji nayee ni mpiganaji mwenzetu kwahiyo haiogopi Serikali ya CCM.

  ANGALIZO JIFUNZE KUFATILIA NA KUULIZA
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani tatizo hapa ni mawasiliano. Kwa muda mrefu wanaJF wamekuwa wanashauri kitengo cha mawasiliano chadema kiimarishwe. Sijui kuna nini lakini wamekuwa wagumu sana. Website yao haitumiki kama ipasavyo. Kama wametengeza formula ya kutoa ruzuku wa kila Mkoa kinawashinda nini kuweka hizo taarifa kwenye website yao? Kwa sasa hivi kila mbunge wa chadema anaokena kukazania kutoa taarifa kivyake, facebook twitter, blogs lakini hakuna effective communication system ya chama kama KIKUNDI.
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,698
  Trophy Points: 280
  wewe ndo unajibu utumbo, kama nae hayupo kazini thibitisha. Hujui kilichomsukuma hadi kusema nape yupo kazini
   
 19. M

  MPG JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekujibu vizuri angalia hapo chini mchanganyuo
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Fungu kubwa la Ruzuku linakwenda kwenye maandamano ya Chadema, karibu wabunge wote huwa wanashiriki na kila baada ya maandamano kuna posho wanagawana viongozi wakuu pamoja na wabunge, bado kuna malazi na chakula kwa wastani kila maandamano makadilio ni 50 Milioni, na wastani wa maandamano yanafanyika kwa mwezi mara mbili, sasa hapo unadhani mikoani watapata nini
   
Loading...