Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,271
- 2,400
Kwa mizengwe inayoendelea huko CCM kile kinachoenda kutendeka mwakani, ni wazi kwamba kuna maandalizi kabambe ya kuvuruga tena upinzani nchini. Namuona mwanadiplomasia mashuhuri 'akitoswa' na chama chake katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Nawaona CCM wanavyosuka tena mpango wa huyu nguli kuangukia upinzani na hatimaye kuwania kupewa rungu la kupeperusha bendera ya UKAWA. Nawaona baadhi ya wanaukawa wanavyotamani hili litokee, lakini nawaona wanaukawa makini wakisema safari hii ni BIG NO!
Jaribio la kuipasua CCM lililofanyika miaka kadhaa iliyopita lilifanikiwa angalau kwa asilimia nyingi. Palikosekana tu nguvu ya ziada kumalizia mpasuko huo. Hivyo jitihada ziendelee kufanyika kuona ni namna gani CCM inadhoofishwa kimikakati lakini upinzani ukihakikisha kuwa hawazibi tena tundu la panya kwa keki. Ni hayo tu kwa sasa
Sent using Jamii Forums mobile app