CHADEMA, Mbunge Msigwa wa Iringa atoa misaada kwa Hospitali Mpya

Jamani sie tulidanganywa eti tukichagua upinzani wataleta vita sasa mbona waliojaribu wanafaidi matunda uuuuwiiii 2015 njoo haraka.
 
Inguluvi ikutangage mvina ugendelage ludodi ndayiyo. Umemfunika mbunge aliyepita ambaye alikaa miaka mitano bila kuifanyia chochote Iringa. mpaka tukafike mwaka 2015 Iringa yetu itakua imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. tuwekee ratiba ya kukuona ofisin nina changamoto nyingi sana za manispaa yetu ya Iringa nataka nije tujadili tuone ni jinsi gani tunaweza kushirikiana kuzikabili.
All the best mbunge wangu
 
Tatizo wabunge wetu wanashindwa kutofautisha "uongozi" na "ufadhili".
Na hii ndo inazidi kulemaza wananchi wabaki kuwa watu wa kuletewa tu.

Kwa hapo sioni tofauti kati ya mbunge Msigwa na Mohamed dewji wa Singida.

Kuna watu wananitukana kwa hii post.
Na hili ndo tatizo la watu wanojifanya "mashabiki wa chadema". Wanataka kila mtu aseme: "safi chadema, hongera sana, tunachukua nchi kesho....." ukimuuliza how? hana cha kujibu.

Laiti wangalijua kuwa uchadema wangu unawazidi wao kwa kiasi gani, nadhani wangalikaa kimya kabisa.

Yote kwa yote:
Chama hakitafanikiwa kwa misifa tu, hata pale pasipostahili. Vinginevyo nachelea kusema sioni tofauti kati ya ccm ubwabwa na pro-chadema wa aina hii.
 
Mh. Msigwa umetenda vema...HONGERA
Wasiwasi wangu ni kuhusu chanzo cha fedha hizo ni mshahara wako
au kuna wafadhili...But all in all hilo ni jambo zuri...kwakuwa wewe pia ni Diwani
tafadhali shughulikia barabara za katikati ya Manispaa zina mashimo mengi yanazidi kupanuka
kila siku.....pia mfumo wa maegesho ni wa hovyo sana katikati ya manispaa hasa mbele ya CRDB bank, stendi ya Miyomboni
Karibu na MR, na NSSF... anzeni kama manispaa ya Ilala anayepaki hovyo gari lake alipe
faini kuongezea manispaa mapato...maafisa afya wafanye kazi ipasavyo kwani nyumba za wageni hasa
za katikati ya mji ni chafu zina mende....Aibu nyingine ni mpaka leo mnatoa vibali vya ujenzi wa vibanda na nyumba
ndogo za kawaida za kuishi katikati kabisa ya mji lini IRINGA itakuwa jiji kwa hali hii???

nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, ila pia, Msigwa tafuteni namna ile stand ya daladala za kuelekea Ilala na Mkwawa pale MR haipaswi kuwepo pale, hadhi na sura ya manispaa inapotea. Tafuteni eneo jingine walau maeneo ya Stand kuu. Pili, madereva wa bodaboda wamekuwa wakilalamika kuwa polisi wanawakataza kufanya biashara zao wkt wa mchana na badala yake wafanye wkt wa usiku tu.. Hebu litizame hili, kwakuwa bodaboda zimekuwa zikiwanyanyua vijana wengi kiuchumi hapa nchini, sasa kwanini manispaa yako iwe nyuma kwa hili. Na inasemekana kuwa chama cha wamiliki wa daladala na Taxi ndio waliotengeneza zengwe hilo kwa kuhofia ushindani wa kibiashara.
 
Asee nasikitika sana nchi hii itaendelea lini sijui.nahoji sasa? 01 )sikatai jambo alofanya msigwa ni jema sana lakini hivi kwann anunue vitanda vya kichina 1,500,000/= wakati angeweza kuwapa ajira maselemala na kuleta tija kwa bei ya 200000 wachonge 6 kwa bei hiyo ,najua vya wagonjwa ni tofauti na kawaida ila wakipewa vigezo wanaweza.02 ) yeye ni mfadhili au kiongozi ?03) familia yake itatoa 12million ,from where for wat ? Je asingepata ubunge asinge fanya hivo.04 )hiyo pesa ni aliyoipata kwa miradi yake au ziada ya posho na mishahara wanayojilipwa kuzidi mahitaji halisi.kuna haja ya kubadili mtazamo wa ubunge kuwa mbunge ni mwanchi makini ambaye tumemthibitisha kwa sera na maisha yake kiasi cha kumwamini atuwakilishe kugawana keki ya nchi bungeni sio kutupa misaada ya pesa yetu.viongezwe vigezo hivi :01) awe ameushinda umasikini kaya yake kwa kishindo ,huwezi shindwa kulea familia yako ukalea jimbo.02) kabla hajaapishwa tra na bodi maalum ikague mali zake.
 
USHAURI KWA MHE MSIGWA.

1. Jaribu kufanya siasa kidogo.
Hii ninamaanisha kuwa, umekuwa ukiwaeleza wananchi wa iringa ukweli ulio wazi, jambo ambalo wamekujengea mtizamo hasi na wanajuta kwanini walikuchagua.
Sababu kuu, ni kuwa umekuwa ukiwapa majibu kwa lugha ya ukali yenye maneno makali, (japo ndio ukweli halisi) lakini kwa mtazamo wangu haukijengi chama chako bali unakibomoa. Acha dharau, tumia maneno yenye matumaini na hata kama unamkatalia mtu jambo fulani kuna lugha nzuri hasa ya kisiasa ambayo mtu anaridhika au anafarijika kukutana na mbunge wake badala ya kuchukia au kujilaumu kukutana na mbunge wake tena wa CHADEMA.

2. Jaribu kuwa karibu na makundi mbalimbali hasa kina mama na vijana.
Kwa sasa akina mama wengi wanakuchukia mbaya. Sababu wanazotoa ni kuwa hutaki kusikiliza shida zao, kumbuka walikupigia kura nyingi sana wkt wa uchaguzi 2010. Pia uwe na tabia ya kukutana na vijana mara kwa mara na uwaletee mawazo na mipango mbalimbali yenye fursa za ajira ili kuwakombo walau hata kuwaonyesha njia. Kumbuka vijana hawa ndio waliokuwa wakikuchangia shs 200-500 ili upate mafuta yakufanyia kampeni. Majibu ya shortcut ambayo umekuwa ukiwajibu yanawaumiza na wameanza kukuchukia na kujutia kwanini walikuchagua. Njoo huku chini kaa nao, watakuelewa na mwisho wa siku CHADEMA kitaimarika hapa mkoani iringa.

3. Jaribu kutatua mgogoro baina yako na Gervas Kalolo na Abuu Majeki.
Hawa jamaa kamwe hutawasahau katika ubunge wako. Walikusaidia sana katika kampeni. Leo hii unawasema vibaya tena kwa wapiga kura wako ambao wanatambua mchango wao kwenye ubunge wako. Umekuwa ukipita mitaani na kuwasema vibaya mfno. eti Abuu Majeki hajui kusoma wala kuandika, eti Gervas kalolo anasumbuliwa tu na maradhi. Plz kila binadamu anamapungufu yake lakini sio lazima kuyaweka hadharani hasa watu muhimu kwako kama hawa jamaa .
4. Kwenye uchaguzi ndani ya chama, 2012 usigombee.
Kiukweli kwa nafasi yako tu ya ubunge achilia mbali uenyekiti wa wilaya, CHADEMA imeanza kupoteza mvuto na matumaini, na sababu kubwa ni wewe (msigwa)..
 
Heeee....... Kumbe Si hasa ???????
Mwacheni afanye kazi, msijipendekeze kwake.
mara VIVA CDM, mara pipoz pawa!!!!!!! Inahusu nini ?
amehangaika yeye, katafuta mwenyewe, msijibehedue kwake.
Comarade, fanya kazi.!!!
BIG UP !
 
Saaafi! mpiganaji saidia jimbo lako, magamba walilitelekeza kwa muda mrefu!!!!
 
hongera sana Msigwa...pia hongera ziwaendee wana iringa wote kwa kumuona na kumchagua..haya ndo matokeo ya kuchagua watu makini...
 
Back
Top Bottom