CHADEMA, Mbunge Msigwa wa Iringa atoa misaada kwa Hospitali Mpya

Tatizo wabunge wetu wanashindwa kutofautisha "uongozi" na "ufadhili".
Na hii ndo inazidi kulemaza wananchi wabaki kuwa watu wa kuletewa tu.

Kwa hapo sioni tofauti kati ya mbunge Msigwa na Mohamed dewji wa Singida.

Wewe ndo unashindwa kutofautisha kati ya kiongozi na mbunge,je hujui kwamba mbunge ni kiongozi? Katika nafasi ipi? Kwa kuwa tunajua jf hatutakiwi kupinga kwa matusi napenda nikuambie kwamba wewe unapenda kupewa vijisendi,watu wa IR Kwa sasa [VIFUNYA YI CCM]maana wamegundua kwamba maendeleo ni kutatua karaha zilizodumu miaka nenda rudi.PIA HAWA JAMAA WANAHISTORIA MOJA WAKISEMA BASI MAANA YAKE BASI,NI HERI WAJITUNDIKE.Mkwavinyika!
 
Tatizo wabunge wetu wanashindwa kutofautisha "uongozi" na "ufadhili".
Na hii ndo inazidi kulemaza wananchi wabaki kuwa watu wa kuletewa tu.

Kwa hapo sioni tofauti kati ya mbunge Msigwa na Mohamed dewji wa Singida.


Afadhali huyu kafadhili vitanda vitavyolaliwa na wote, ccm,cdm,tlp, nccr, vipi hao wengine wanaofadhili tshirt na ubwabwa?
Na kumbuka hawana serikali hawa, pamoja na kuwapigia kelele wanaoendesha serikali bado wameweka pamba masikioni.
Hebu jiulize, ni wabunge wangapi au viongozi wangapi wanapewa misaada kwa project za wanachi na haziwafikii?
 
Kazi bora CDM, na wapambanaji wote...huduma na maisha bora ya wapiga kura ndio mtaji wa siasa bora na utendaji bora wa kuwajibika...tuachane na Wana-Magamba wa kijani wamebakia kufilisi nchi na kutoa utetezi eti 'hali ya uchumi wa dunia ni mbaya kwa ujumla' ndio maana maisha ya wananchi yanazidi kudhoofika, wakati wao matumbo yanazidi kwenda pembeni na kujijengea utajiri kifisadi?

Nenda Msigwa, nenda CDM, tulikomboe taifa, tunyanyue maisha ya watanzania...! Pamoja Daima!
 
Afadhali huyu kafadhili vitanda vitavyolaliwa na wote, ccm,cdm,tlp, nccr, vipi hao wengine wanaofadhili tshirt na ubwabwa?
Na kumbuka hawana serikali hawa, pamoja na kuwapigia kelele wanaoendesha serikali bado wameweka pamba masikioni.
Hebu jiulize, ni wabunge wangapi au viongozi wangapi wanapewa misaada kwa project za wanachi na haziwafikii?

Umesema vema ndugu yangu. Kuna watu wanaandika proposal za miradi kwa ajili ya wananchi lakini ikishatiki wanayeyushia kwao
tu. Naungana na wote waliopengeza juhudi za mbunge wetu msigwa kwani hata kama wengine watasema ni takrima lakini mi naona bora takrima inayopelekea maendeleo kuliko zile za misosi na 10,000 kama alivyosema kwenye hotuba yake. Bravo Pastor, Piga Kazi kwa kwenda mbele. Angalia maeneo mengine yenye kugusa jamii yetu uchangie na huko. Hatuwezi kusubiri serikali kufanya kila kitu. Wanaoweza kuchangia maendeleo kama Mh Msigwa wafanye hivyo kwa maendeleo yetu. Kama CCM watakuwa wameguswa wafanye na wao mambo makubwa ili wanasiasa wakishindana kwa mtindo huo muda si mrefu kero zitakuwa zime pungua sana
Bless you Mh Msigwa
 
Tatizo wabunge wetu wanashindwa kutofautisha "uongozi" na "ufadhili".
Na hii ndo inazidi kulemaza wananchi wabaki kuwa watu wa kuletewa tu.

Kwa hapo sioni tofauti kati ya mbunge Msigwa na Mohamed dewji wa Singida.

hata huku ketwu wapo, kijiba cha roho na utakesha sana, kesha mpaka mchana ila makamanda wanasimama hivyo siku zote
 
Kangalage myaaa!!gendelage uludodifu ulukafu luladenyeka!!Inguluvi inyaluhala ikutange bee...mele ta liwoko la ishukurani beee!avamama vatatige luhulo...kisa kwigaya figonelo....Piga kazi Mwanangu Msigwa!icheki na stand ya Mlandege!simamia na barabara...toa mambo ambayo ni tangible!achana na bishoo,tozi nyangema Vangimembe Wily Lukuvi!amekalia kukupga majungu wakati jimbo lake masikini wa kutupwa!Isiman hakuna maji,wanapokunywa punda ndo watu wanachota,maji ya makorongoni...huduma za afya mbovu Isimani kote!nilienda kumcheki jamaa yangu kijiji kimoja Migoli Jimbo la Ismani...maji shda tupu!ebu Msigwa Piga kaz uipe uhai CHADEMA IRINGA!...Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema akubariki sana!
 
Ni Msigwa na R.T.C.O. Hata hivyo migomo na maandamano vimewachelewesha sana, sasa ndiyo wameanza kufanya siasa.
 
Mh. Msigwa umetenda vema...HONGERA
Wasiwasi wangu ni kuhusu chanzo cha fedha hizo ni mshahara wako
au kuna wafadhili...But all in all hilo ni jambo zuri...kwakuwa wewe pia ni Diwani
tafadhali shughulikia barabara za katikati ya Manispaa zina mashimo mengi yanazidi kupanuka
kila siku.....pia mfumo wa maegesho ni wa hovyo sana katikati ya manispaa hasa mbele ya CRDB bank, stendi ya Miyomboni
Karibu na MR, na NSSF... anzeni kama manispaa ya Ilala anayepaki hovyo gari lake alipe
faini kuongezea manispaa mapato...maafisa afya wafanye kazi ipasavyo kwani nyumba za wageni hasa
za katikati ya mji ni chafu zina mende....Aibu nyingine ni mpaka leo mnatoa vibali vya ujenzi wa vibanda na nyumba
ndogo za kawaida za kuishi katikati kabisa ya mji lini IRINGA itakuwa jiji kwa hali hii???

Nilifikiri unaakili ulivyoanza kuongele ishu ya parking ndo nikagundua matatizo ya IQ
 
Nimefurahishwa na kazi hiyo.
Na hiyo ndio moja ya kazi za Kibunge, anunue, aombe au hata Kama katokea muhisani akamkabidhi nae akakabidhi kwa walengwa, basi hiyo ni faraja na mapenzi kwa Kiongozi Kama Mch Msigwa.
 
Lazima itoke hongera kwakila mpenda maendeleo wa nchi hii,kwanza umetoa somo kuwa tujiulize tunaifanyia nini Tanzania kabla ya kuuliza itakufanyia nini.Umeonyesha njia atakayebeza mdomo ni demokrasia hulipii kodi ya kuongea na hasa ukizingatia mdomo ni nyumba ya maneno.Mwanakwaya mh. Martha Mlata uliyemponda sana mchungaji na leo ponda tena.Kupanga ni kuchagua,huwezi kukurupuka akahidi utatekeleza kila kitu,kwanza lazima tuwe na vipau mbele,nini tufanye na kwa wakati gani.Hongera sana Mh. Msigwa
 
Hongera mh. Msigwa na msaada ulioutoa ni imani yangu utaandaliwa utaratibu wa wananchi wengine kutoa michango yao kwani suala la maendeleo ni letu sote.
 
tatizo wabunge wetu wanashindwa kutofautisha "uongozi" na "ufadhili".
Na hii ndo inazidi kulemaza wananchi wabaki kuwa watu wa kuletewa tu.

Kwa hapo sioni tofauti kati ya mbunge msigwa na mohamed dewji wa singida.

kutokuona utofauti kwako ni ujinga ulonao kitaaluma,hv ulishawahi kuona kiongozi asiyewasaidia wananchi wake hapa duniani?hata baba wa taifa kuna wakati alihmiza na wakati aliwaletea wananchi vifaa vya kazi,sasa ww ucchoelewa nn!
 
Mh.msigwa unastahili pongezi za kipekee umeonesha njia njema kuwa muda si kigezo bali nia thabiti na uzalendo wa kweli.hongera sana kamanda!!
 
Viva msigwa! I real proud u to be my representative mjengoni! Niko kifua mbele siyo kama magamba kila siku wamefisadi hela za umma yaani wanakela sana

Peoples powerrrrrrrr

But tukukumbushe ile ahadi ya kututafutia hati za nyumba sisi ambao tulijenga bila kufuata mipango miji maeneo ya mwangata, kihesa, kiondombi na ferimo do it jembe langu
 
Mbunge wa Iringa mjini kupitia Chadema ametoa msaa wa thamani ya sh 50 milioni ikiwa ni pamoja na vitanda 30 kwa hospitali mpya ya wilaya ya Iringa ikiwa ni sehemu ya ahadi zake kwa wapiga na wananchi wa jimbo hilo.

Source: wapo redio
 
Back
Top Bottom