CHADEMA, Mbunge Msigwa wa Iringa atoa misaada kwa Hospitali Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, Mbunge Msigwa wa Iringa atoa misaada kwa Hospitali Mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Feb 16, 2012.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,154
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  February 16, 2012

  MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MCHUNGAJI MSIGWA AWAZIBA MIDOMU CCM ,AKABIDHI VITANDA VYA MAMILIONI YA SHILINGI

  [​IMG]Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kulia akikabidhi vitu mbali mbali leo kwa ajili ya Hospitali ya Manispaa ya Iringa Mjini kwa kaimu meya wa Manispaa ya Iringa Vitor Mushi mwenye shati la kijani katikati
  [​IMG]Wananchi wakishusha vitanda katika malori leo vitanda ambavyo ni msaada kutoka kwa mbunge Msigwa
  [​IMG]Sehemu ya vitanda vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa leo
  [​IMG][​IMG][​IMG]Hii ndio Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa ambayo mbunge Msigwa amekabidhi vitanda vya kisasa itaanza kutoa huduma jumatatu wiki ijayo
  [​IMG][​IMG]Vitanda vya kisasa vikiwa vimeshushwa katika lori kwa ajili ya matumizi ya Hospitali ya Manispaa ya Iringa
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]Baiskeli kwa ajili ya walemavu na wagonjwa watakaofika kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo
  [​IMG]Mbunge Msigwa akionyesha jinsi ya kuseti vitanda hivyo kwa umeme
  [​IMG]Kaimu mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa diwani wa kata ya Mtwivila Victor Mushi (CCM) akishukuru kwa msaada huo kutoka kwa mbunge Msigwa (Chadema)
  [​IMG]Umati wa wananchi waliofika kushuhudia zoezi hilo nyeti
  [​IMG]MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amekabidhi vitanda vya kisasa 30 pamoja na magodoro yake kwa ajili ya kusaidia kulalia wagonjwa na Baiskeli za walemavu (Wheel chairs) 19 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 50 na kuwapongeza wabunge waliomtangulia akiwemo Monica Mbega (CCM) kwa kazi nzuri.

  Akikabidhi msaada huo leo kwa kaimu meya wa Manispaa ya Iringa Victor Mushi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa iliyopo eneo la Frelimo mjini hapa ,mbunge Msigwa alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo kama njia ya kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuboresha huduma za afya.

  Hivyo alisema kuwa kwa upande wake ataendelea kufanya mambo ya kimaendeleo zaidi badala ya kutoa fedha za kula kwa mwananchi mmoja mmoja japo ambalo halitasaidia kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo la Iringa mjini.

  "Kiukweli kama rafiki zangu ninao wengi sana na leo hii nikaamua kugawa fedha shilingi 10,000 kwa kila rafiki yangu kama sehemu ya ahsante kwa kunichagua nitakuwa siwasaidii na njia sahihi ya kuwasaidia rafiki zangu na wapiga kura wangu ni kuwasogezea maendeleo kama hivi....hivi vitanda leo vitatumiwa na wana Chadema, CCM ,CUF ,TLP ,NCCR Mageuzi na wanachama wa vyama vyote na wasio na chama ambapo ni jambo la msingi zaidi kuliko kuwa mbunge wa kugawa fedha za kula...kweli wananchi wangu naomba mnisamehe kama nitawakwaza kwa kufanya shughuli za kimaendeleo"alisisitiza mbunge Msigwa.

  Hata hivyo alisema kuwa si kwamba amekuwa akichangia shughuli za kimaendeleo kwa kutumia uwezo na maamuzi yake pekee bali amekuwa akifanya hivyo kwa kuzingatia zaidi mawazo na maagizo ya wananchi waliomchagua kupitia ofisi yake na mikutano mbali mbali ya hadhara aliyopata kuifanya kabla ya baada ya vikao vya bunge na mabaraza ya Halmashauri ya Manispaa.

  "Katika mazingira hayo jukumu la mbunge na diwani makini si kuwapoza wananchi kwa kuwapa vijisenti na vizawadi vya kula leo na kumalizika leo ,au kuwadanganya kwamba naweza kuwaletea maendeleo kwa kutumia mshahara wangu wa ubunge ambao sote tunajua kuwa hautoshelezi watu wa jimbo hili ,bali ni kuhudhuria kwenye vikao hivi na kuhakikisha kuwa vinapitisha maamuzi na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo yenu ...nashukuru kwa kunielewa kwani wajibu wangu kikatiba ni kuishauri na kuibana serikali kwa manufaa ya maendeleo yetu"

  Mbunge Msigwa alisema kuwa mbali ya kukabidhi msaada huo katika Hospitali hiyo ya wilaya ya Iringa mjini kama njia ya kupunguza msongamano katika Hospitali ya mkoa wa Iringa bado amekuwa mbele kuchangia shughuli mbali mbali zikiwemo za michezo na kuona kuwa ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni zinatimizwa kwa wakati ikiwemo ahadi ya kuchangia shilingi milioni 12 kila mwaka kutoka katika familia yake kwa ajili kusaidia watu wenye matatizo .

  Akielezea juu ya msaada huo alisema kuwa kila kitanda kimoja kinagharimu zaidi ya shilingi milioni 1.5 wakati baiskeli kila moja ni zaidi ya shilingi 700,000 pamoja na vikabati vya kuhifadhiwa vifaa vya wagonjwa katika mawodi na kuwa msaada huo ameupata kupitia wahisani wake R.T.C.O japo alisema hakupenda sana kutumia kutafuta sifa kwa msaada huo kwa kuweka thamani ya fedha kama ambavyo wanasiasa wengine wanavyofanya.

  Pia alitaka wananchi wa jimbo la Iringa mjini mbali ya kusubiri kusaidia na serikali kwa kila jambo bado wanaweza kujitolea kusaidia huduma za afya ,elimu na maendeleo mengine katika maeneo yao na kuwa ofisi yake kuanzia sasa itafanya kazi ya kupokea misaada na michango mbali mbali kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya jimbo la Iringa mjini.

  Kwa upande kaimu meya wa Mnaispaa ya Iringa diwani wa kata ya Mtwivila Victor Mushi (CCM) mbali ya kumpongeza mbunge Msigwa kwa msaada huo mkubwa bado alitaka vifaa hivyo kutunzwa zaidi ili kuweza kuendelea kusaidia katika Hospitali hiyo .

  Huku kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza matatizo ya akina mama wajawazito ambao wamekuwa wakipata shida na kuwa tukio hilo la kukabidhi vitendea kazi katika Hospitali hiyo ni tukio la kupongezwa na kuwa katika shughuli za kimaendeleo wanasiasa wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuharakisha maendeleo badala ya kuingiza mivutano ya kisiasa isiyo na tija katika maendeleo ya wananchi

  Huku wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakiwemo wana CCM na wanachama wa vyama vya upinzani wamepongeza jitihada za mbunge wao Msigwa kwa msaada huo na kutaka wabunge wa CCM kuiga mfano huo katika kuchangia maendeleo badala ya kutoa takrima kwa wapiga kura.

  John Kalinga ni mwana CCM mkazi wa Frelimo amesema kuwa wengi walikuwa wakishindwa kumuelewa mbunge Msigwa ila sasa wamemtambua vema kuwa ni mbunge wa kazi katika jimbo hilo na kuwa jitihada hizo zinaweza kuja kuwa mwiba kwa CCM kulichukua jimbo hilo kutokana na mambo ambayo anayafanya kuwa makubwa zaidi ukilinganisha na yale ya CCM.

  Huku Sarah Sanga mwana TLP amepongeza jitihada hizo na kutaka wana CCM kuacha kuelekeza mashambulizi kwa mbunge Msigwa badala ya kuelekeza mashambulizi ya kimaendeleo kwa wananchi
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,154
  Likes Received: 1,245
  Trophy Points: 280
  Natamani wabunge wa CCM wangekuwa na Moyo kama huo tungekuwa mbali sana hebu fikiria miaka 50 ya Uhuru. Lakini jamaa ni mabingwa wa kutoa ubwabwa na mavazi ya njano na kijani wakati wa kampeni tu.

  Lakini badala ya kutoa ndo wanataka kujiongezea posho tu.

  Magale Shibuda John upo? Hebu na wewe wape Demo kidogo hapo Maswa ili ku neutralise mambo ya posho.
   
 3. m

  moshingi JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Msigwa umetenda vema...HONGERA
  Wasiwasi wangu ni kuhusu chanzo cha fedha hizo ni mshahara wako
  au kuna wafadhili...But all in all hilo ni jambo zuri...kwakuwa wewe pia ni Diwani
  tafadhali shughulikia barabara za katikati ya Manispaa zina mashimo mengi yanazidi kupanuka
  kila siku.....pia mfumo wa maegesho ni wa hovyo sana katikati ya manispaa hasa mbele ya CRDB bank, stendi ya Miyomboni
  Karibu na MR, na NSSF... anzeni kama manispaa ya Ilala anayepaki hovyo gari lake alipe
  faini kuongezea manispaa mapato...maafisa afya wafanye kazi ipasavyo kwani nyumba za wageni hasa
  za katikati ya mji ni chafu zina mende....Aibu nyingine ni mpaka leo mnatoa vibali vya ujenzi wa vibanda na nyumba
  ndogo za kawaida za kuishi katikati kabisa ya mji lini IRINGA itakuwa jiji kwa hali hii???
   
 4. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu Msigwa kanigusa sana, ndani ya muda mfupi wa utumishi wake kahanza kufanya mambo makubwa, viva Msigwa, hakika wewe ni mbunge wa vitendo.
   
 5. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tatizo wabunge wetu wanashindwa kutofautisha "uongozi" na "ufadhili".
  Na hii ndo inazidi kulemaza wananchi wabaki kuwa watu wa kuletewa tu.

  Kwa hapo sioni tofauti kati ya mbunge Msigwa na Mohamed dewji wa Singida.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hongera msigwa nimeipenda sana hii!
   
 7. m

  mtukwao12 Senior Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 112
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  namkubarigi sana huyu jamaa...sema tu anachanganya dini na siasa...
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongera wana Iringa kwa kupata mbunge makini
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kazi nzuri mh mbunge waache ccm walilie posho ili kufidia gap la mikopo ya kununulia kura.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mhhh hiyo niliyo bold hiyo... mweee au ulitaka kuandika KAYANZA maana jina limewakaa kweli watanzania hili
   
 11. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  vitanda vya kisasa kabisa hivyo hata aghakani havipo
   
 12. M

  Muggssy Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani kuchanganya dini na siasa dhambi we vipi? ina maana wanasiasa hawatakiwi kua na dini kama kingunge Ngobale Mwiru ambaye anapayuka tu siku hizi au kwakua yeye ni mchungaji basi hapaswi kua mwana siasa? be analystic bwana!!! Kwamaana hiyo wanaopaswa kua kwenye siasa ni pegans tu au ? naomba unijibu
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  vitanda vya umeme? huyu jamaa wa ukweli aisee ccm hawezi poteza pesa yake yote hio angeenda kujenga huko lushoto kama kina mkapa
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  haya ndio mambo tunayotaka kusikia kila siku.....
   
 15. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,088
  Likes Received: 10,447
  Trophy Points: 280
  hongera mh. Msigwa umenigusa sana God bless you.
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Kafanya jambo la msingi ila nimeona vitanda vimeandikwa maneno "Kwa niaba ya Mbunge Msigwa na R.T.C.O" ni vyema tukajuzwa pia hawa R.T.C.O ni kina nani na wamechangia nini katika hivi vifaa.
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pamoja na yote Mheshimiwa P.Msigwa angalia na barabara ya Kihesa inayoenda Chuo kikuu Tumaini, inatisha ni mbovu ina mashimo wakati wa mvua ni hatari, kuna siku nilikua kwenye Taxi natoka Miyomboni kwenda Tumaini University mvua ilikua inanyesha maji yakawa yanatiririka barabarani, tulikanyaga msumari tairi ikapusuka, nashukuru tulikuwa kwenye mwendo mdogo sana... Tupia macho kwenye barabara
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ni jambo la kuigwa alilofanya mbunge Msigwa sasa ni wazi CDM mwalimu wa maendeleo.
   
 19. BORNCV

  BORNCV JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mambo ndio hayo ameshasema R.T.C.O ndio wahisani walioshiriki kwenye msaada huo sasa wewe unataka nini?
  Mambo mazuri haya gafla changia mawazo yako kuimarisha maisha ya wana Iringa sio kulalamika tu.
  Wote tuseme PEOPLES POWER!
   
 20. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Thanks Msigwa may the lord bless u
   
Loading...