CHADEMA mawazo mapya Kwa wakati muafaka!! CCM Wililin Chip | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mawazo mapya Kwa wakati muafaka!! CCM Wililin Chip

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasimba G, Mar 17, 2012.

 1. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  WaAfrocaribean na watu wenye asili ya Africa wanaokaa nchi za ulaya na America huwa wanaamini kuwa wazungu waliwatawala kwa kutumia wililin chip, yaani mtu mweusi alikuwa analazimishwa kuamini kuwa yeye hafai kitu mbele ya mtu mweupe, hata kama mtu mweupe mwenyewe ni hamnazo.

  WaAfrocaribean na watu wusi wa pembezoni walipigana dhidi ya wililin chip na kushinda ndio kisa cha kushindwa biashara ya utumwa na udhalilishaji mwingine juu ya watu weusi, hivyo walishinda vita ambayo adui aliteka mawazo na kuwaambia wao si kitu!

  Wililin chip kwa watanzania ni hiki chama CCM! Wako watu pamoja na kudhalilishwa bado hujiona si kitu na pia huambiwa nyie si kitu nao huamini, Hivi utabambikiwa kesi na baada ya kufungwa unatoka gerezani na kusema CCM number one? Wililin chip!

  Utaambiwa kanunue dawa harafu ukipona unasema CCM number one! Wililn chip!

  Utachaguliwa kiongozi ambaye una uhakika hana uwezo na ukampigia kura na kumshangilia wakati unajua kiongozi mwenyewe ****! Wililn chip

  Hebu tujikomboe na ujinga ambao watawala wetu, wanatuwekea vichwani mwetu na tushinde huu utumwa kama watu weusi wa pembezoni walivyo pambana na wanaendelea kupambana mpaka leo hii, viongozi wa CCM wa leo hii ni kama wakoloni hebu tuitoe wililin chip na tuwe huru kifikra kwa kuikataa CCM!

  Nawasilisha
   
Loading...