CHADEMA: Matamanio ya IGP Sirro anayosema amejifunza Rwanda kuhusu Polisi kuingia Misikitini na Makanisani na kuandaa mitaala ni kinyume na Katiba

Huu ndio utofauti wa CCM na CHADEMA. CHADEMA kila anayeongea hutoa hoja zenye uzito na mantiki.

Siro huko aliko atakuwa amepata shule ambayo hakuitarajia. Na hakika si Siro wala polisi yeyote atakayeenda msikitini au kanisani eti kwenda kuangalia mitaala.
 
Kwanza Kabisa nichukue muda kidogo kumshukuru Mwenyezi Mungu , mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuamka salama , sema Amina .

Baada ya utangulizi huo wa kiroho nafurahi kukufahamisha kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo 14/9/2021 kitafanya Mkutano wake na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za makao makuu yake , Kinondoni mtaa wa Ufipa , Nje ya Jiji la DSM , Kuanzia saa 6 kamili mchana .

Wote mnakaribishwa huku mkiombwa kufuata sheria za dunia za kujikinga na Corona

----- HOTUBA----

View attachment 1937579
Naibu katibu Mkuu Bara, Benson Kigaila

Imeonekana kwa Jeshi la Polisi na kwa Kamanda Sirro ni kitu cha kawaida kabisa kuvunja sheria na Katiba."

Wiki iliyopita IGP ametoka Rwanda akaongea na vyombo vya habari akawa anaeleza mambo ambayo amesema kuwa amejifunza Rwanda. Kwamba Jeshi la Polisi linapitia kuona kwenye Madrasa na Sunday School wanafundisha nini?

Sirro anataka kwenye Madrasa badala kufundusha neno la Mungu wafundishe uzalendo, anataka kwenye makanisa badala ya kufundisha neno la Mungu kwa watu wa Kipaimara, Komunyo ya kwanza na Ubatizo wafundishe uzalendo.

Sirro anasema ameambiwa na polisi wa Rwanda, Hajatuambia kama aliwauliza wale polisi wa Rwanda kwamba Katiba yao inasemaje, hajatuambia kama sheria ya Rwanda inasemaje kuhusiana na hilo suala.

Sisi Tanzania siyo nchi iliyozaliwa leo, Tanzania siyo nchi kama walivyoanza kuifanya kina Sirro kwamba ni nchi inayokwenda kwa maelekezo na matamko, Tanzania ni nchi yenye katiba pamoja na ubovu wake.

Katiba ya mwaka 1977 pamoja na mapungufu yake na ubovu wake lakini ipo Katiba, sheria zetu pamoja na mapungufu yake lakini tuna sheria. Katiba inasema ibara 26 (1) 'Kila mtu ana wajibu wa kutii Katiba hii na kufuata sheria za JMT'. Inamuwajibisha kila mtu pamoja Sirro.

Ibara ya 26 (2) inasema kila Mtanzania ana wajibu kwa taratibu zilizowekwa kuhakikisha Katiba hii inahifadhiwa na kulindwa. Kwa maana hiyo kila mmoja anawajibu wa kulinda Katiba.

Matamanio ya Sirro anayosema amejifunza Rwanda anataka sasa Jeshi la Polisi lianze kuingia Misikitini na Kanisani liweze kuandaa mitaala ya Makanisa na Misikiti wafundishe nini, ni kinyume na Katiba.

Ibara ya 19 (2) inasema 'katika kueneza dini au katika kuendesha ibada majukumu hayo yatafanywa nje ya mamlaka ya kiserekali maana yake mamlaka ya kuendesha ibada, malaka ya kueneza dini hayataingiliwa na Serikali.

Ibara 19 (3) inasema 'kuingilia uendeshaji wa dini maana yake kutavuruga umoja wa kitaifa kutahatarisha maadili ya jamii na amani ya jamii'. Maana yake Sirro anachokutangaza anahatarisha umoja wa kitaifa, anavuruga amani ya nchi na anavuruga maadili ya taifa.

Siyo Sirro wala Rais, wala mtu yoyote mwenye mamlaka ya kuvunja Katiba wala Sheria. Makosa yoyote yanayoshitakika mahakamani ni makosa yanayokiuka Sheria na Katiba. Ukifanya kitendo chochote ambacho kinakiuka sheria zilizopo, hicho kitendo kinaitwa kosa.

Ukiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi ambaye anavunja sheria anajenga polisi ya namna gani?, Ukiwa na mkuu wa Jeshi la Polisi ambaye hasimamii utekelezaji wa sheria badala yake anavunja Katiba anajenga Jeshi la Polisi la namna gani?

Kama Polisi wanavunja sheria hawawi wahalifu? Kama mimi au Mwanahabari akivunja Sheria anakamatwa kwamba ni muhalifu kwanini Sirro anayevunja Sheria na Jeshi lake la Polisi wasiwe wahalifu namba moja.

Wito wetu kama chama kwa Vyombo vya Habari, Taasisi za dini, Vyama vya Siasa, mashirika yasiyo ya kiserekali na Watanzania kwa ujumla, kwamba kwa pamoja tusimame ili kuweza kuhakikisha Katiba na Sheria zilizopo zinalindwa na watawala waliopo.

Wito wetu, tusimame pamoja kuwataka mamlaka ya uteuzi wa IGP, IGP aondolewe. Anaharibu Polisi, anakifanya Jeshi la Polisi kiwe chombo cha kuvunja Sheria badala ya kulinda Sheria. Kama mamlaka ya uteuzi wa Sirro wataona vema Sirro aendelee tutatangaza mgogoro na Sirro.

Sisi kama sheria hazifuatwi tutawaambia dunia nzima kwamba Tanzania sheria hazifuatwi. Tukisema hivyo wanasema siyo uzalendo, uzalendo siyo kunyamazia maovu. Muovu namba moja ni yule ambaye hafuati sheria na Katiba.

Wanaozuia Wawekezaji wasije ni wale akina Sirro wanaokiuka Sheria, wanaovunja Katiba. Siyo Chadema wanaosema Sirro anavunja Katiba. Sisi kama Watanzia ni wajibu wetu kupinga kwa nguvu zote uvunjaji wa sheria na ukiukaji wa Katiba.

Sirro anasema watu wakionekana wanaviashiria vya ugaidi, hivi ugaidi una viashiria gani?, unaweza kumwona mtu ukasema huyu anaviashiria vya ugaidi? Sirro anataka kujifanya kama Nabii/Mtabiri, kwamba anaweza kukutana na watu wanavyotembea akasema wewe unaviashiria vya ugaidi.

Sheria siyo koti, Sirro anataka kulifanya Sheria ni koti. Kaenda kwa Kagame kaona IGP wa Kagame amevaa koti zuri na yeye anataka avae koti hilo hilo bila kujali mwili wake upoje, linaweza likambana au kumpwaya na hili limembana tayari, Kwa sababu amekurupikia.

Chanzo: CHADEMA Tanzania
Mtu anayevunja katiba na sheria za nchi kwa makusudi hafai ni lazima kutangaza mgogoro nae hamna namna
 
Inakuwaje chama bila Mwenyekiti wala Makamu wake?!
inamaana Chadema ni kampuni ya Mbowe?!
aise!! hapo tumeliwa!
ifike mahali uongozi uliopo uwaeleze wananchama hatma ya chama kwa sasa bila mwenyekiti wala Makamu kama kweli Chadema ni chama cha wananchi na sio mali ya kikundi cha watu wachache!!

Nilidhani ungefurahi kuwa mpinzani wako sasa hana uongozi na haeleweki. Badala yake inakuuma sana kuona hata hakuna wanaotilia shaka hatma ya chama.

Nikukumbushe hili - itikadi huwa sio swala la kiongozi tu. Buddha, Mtume Mohamad, Yesu Kristu na hata OBL hawako tena lakini walichoacha kimesimama!!
 
Nilidhani ungefurahi kuwa mpinzani wako sasa hana uongozi na haeleweki. Badala yake inakuuma sana kuona hata hakuna wanaotilia shaka hatma ya chama.

Nikukumbushe hili - itikadi huwa sio swala la kiongozi tu. Buddha, Mtume Mohamad, Yesu Kristu na hata OBL hawako tena lakini walichoacha kimesimama!!
Swadakta
 
Aiiiseeeeee!

SIRRO alikwenda Rwanda kujifunza njia za kuwakandamiza wapinzani kama polisi wa huko walivyofanikiwa kuwafanyia wapinzani wa Rwanda?

Maana ya ziara ile kumbe ilikuwa ni nzito kiasi hiki!
Kaenda kujifunza maovu ya wa italahamwe. Kamanda ni mtu hatari sana.

Umri alionao hata miaka 10 mbele hafikishi. Badala atengeneze na Mungu anazidi kuwa mtu wa Ibilisi.
 
Back
Top Bottom