CHADEMA masalia mliobaki shikamaneni ili chama kisiwafie haraka kiasi hiki

Albert Einstein

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
384
560
CHADEMA MASALIA MLIOBAKI SHIKAMANENI MKOMAE KIUME.

Ingawa ni kazi ngumu kwa namna mlivyokaukwa na midomo na kwa namna mlivyopatwa na mawazo kwa mdororo wa chama chenu alichowahi kukipaisha Dk Slaa mpaka wanaCCM wakawa wanaogopa kuvaa sare zao hadharani, kwamba leo mmekimbiwa na wandani wenu kama vile ni mnaugua maradhi ya ukoma.

Pamoja na haya yote sasa amueni moja ama mkomae mpaka 2020 mkivunje chama chenu baada ya kumalizia muhula wenu wa ubunge. Lakini ninachokiona ni ugumu wa kuweza kuiinua tena Chadema kutoka hapo ilipolala na kuimarika tena, utakuwa ni kwa muujiza wa mwenyezi Mungu peke yake hilo linaweza kutokea labda mliobaki yaani nyie wabunge MASALIA mjiorganize muasisi chama kingine kipya cha siasa lakini hiyo CDM imuda si mrefu itapelekwa wodi moja na NCCR-Mageuzi na CUF.

La mwisho na la muhimu tuzidi kumuombea mwanasheria mwandamizi wa CDM mhe.Tundu Lisu aimarike zaidi ili pengo lake lizibwe na kusiwe na singizio lolote
 
Back
Top Bottom