CHADEMA mambo ya meya wa Arusha inatosha, shughulikieni masuala ya kitaifa sasa

Ccm shughulikeni na matatizo ya wanainchi sio kujivua magamba tumechoka huku hayatusaidii magamba yenu.
 
Tokea kukamilika kwa uchaguzi mkuu wa 2010, viongozi wa CDM wamekuwa very busy kuhangaika na uchaguzi wa meya wa arusha tuu, hali hii imeanza kutukatisha tamaa sisi wapenzi na washabiki wa CDM kwa kuwa hivi sasa taifa linakabiliwa na matatizo kibao kupanda kwa gharama za maisha, kushuka kwa thamani ya shilingi yetu na hivi karibuni Seikali kushindwa kutimiza majukumu ya kifedha. Aidha watendaji mbali mbali serikali na taasisi na mshiriki ya umaa waliowekwa kimkakati katia asasi hizo wamefungulia ufisadi wa kutisha kwa kufuja fedha za ummma kama kwamba dunia na Tanzania ndio inafikai kikomo.

Che kushungaza wakati haya yote yakitokea viongozi wa CDM hawaonekani kujishughulisha kutaka kuleta mabadiliko katika matatizo haya badala yake kila siku ni uchaguzi wa meya Arusha. Halafu wanatutaka tuandamane nchi nzima kwa ajili hiyo.

Sio ombi tena tunawataka viongozi wetu wawaachie wat wa Arusha mamabo yao na waanze mara moja kushughulikia kero zinazotusumbua kama Taifa. Na huyo anayejiita Ndg Heche tokea achaguliwe kushika wadhifa wa Uenyekiti wa BAVICHA hatujamuaona kuja mitaani kuimarisha chama leo anatutaka kupitia vyombo vya habari tukaandamane tena kwa sababu zisizo na msingi wowote.

CDM tifani acheni kufikiria ndani ya boksi tu, tokeni ndani ya boksi muone hali halisi nje ikoje; ama sivyo mtkuja kujikuta mko peke yenu. Waulizeni akina Mrema, Lipumba n.k

watanabe,
Mawazo yako ni kielelezo cha uvivu wa kufikiri na kutafiti .
I.Chama gani zaidi ya Chadema kimezunguka zaidi ya mikoa 13 na majimbo yote ya mikoa hiyo tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana?
2. Mbona huelezi kwanini JK hadi sasa hajafanya ziara ya kutoa shukrani na kutatua kero za kitaifa?
3, kama wewe hujui ajenda za chadema kwenye mikutano hiyo waulize wa tz wakiwemo wa mbeya.
4. Enziza propaganda na upotoshaji zimeisha.
 
Dr.W.Slaa said:

Dr.W.Slaa,

..nimesikitishwa na kauli yako niliyoi-highlight with red.

..kuna mahala pengine ulitumia maneno kama hayo kwa kiongozi ambaye sitapenda kumtaja hapa.

..kama kiongozi anayetafuta ridhaa ya kuongoza nchi nadhani ingependeza kama ungeachana na kauli kama hizo unapo-respond kwa maswali ya wananchi, hata kama maswali hayo yanakera.

..ungemjibu tu Watanabe, kwamba CDM mmefanya mikutano kadhaa, na suala kama muuliza swali ni "mvivu wa kufikiri na kutafiti" ungetuachia sisi tuamue.

..natumai utazingatia ushauri wangu wenye nia njema.
 
Kwanza kabisa wewe haujui ki undani kwanini chadema wanaandaa maandamano haki hakuna katika Tanzania ya leo,uchaguzi wa meya haukua wa haki namaanisha wakazi wa arusha wamenyimwa haki yao ya msingi ya kuwa na meya kutoka kwenye chama wanachokipenda na kilichoshinda kwa kishindo,kaka inaelekea unashsbikia CCM wanavyotumia ubabe kuendesha nchi hii? wewe ndio hautaki wananchi wa Arusha wanataka haki ndio maana wapo mstari wa mbele kutetea haki yao msitumie sababu zisizo na msingi kukizoofisha chama cha chadema.Sina chama mimi ni mwana harakati fikiri kabla ya kutenda
 
Kiukweli kaka ktk hili nakuunga mkono cos kuna wafanyabiashara ndogo ndogo na maduka wanalazimika kufunga maduka yao kisa maandamano ya kila cku,mpaka wengine wanakata tamaa na Lema waliamini atawatoa hatua moja kwenda nyingine kumbe wameleta mizozo isiyoisha na maandamano ya kila cku pasipo sababu za msingi,kweli wanadai haki ila mm na zani bungeni kungekuwa sehemu muhimu ya kudai haki za kimsingi kuliko kuwafanya watu kila cku kuwaza na kesho kunalipi linakuja,Lema afanye kazi,atekeleze ahadi kwa wananchi na sio kugombana na jeshi la polici,kwa ajili yake amelazimisha uongozi wa juu wote wa chama kuwa kufunguliwa mashtaka,ametoa ahadi nyingi sana anatakiwa awasimamie watendaji wa magamba kuakikishe pesa ktk halimashauri zinatumika ipasavyo,sasa mtu kila cku kec anawafanya watendaji walafi waendelee kula tu cos no barking dog,anatukatisha tamaa mwisho wa cku tutamchoka

Mkuu,
Licha ya misukosuko anayoipata Lema, anatekeleza ahadi zake. Mfano ni

1/ kuanzisha mfuko wa elimu ambao tayari unawasomesha sekondari watoto 100 wanaotoka kwenye familia zisizo na uwezo.

2/ kukarabati hosp ya mt meru na ujenzi wa majengo mapya unaoendelea sasahv.

3/ ujenzi wa daraja la sekei na barabara yake kwa kiwango cha lami.

4/ hatua za awali za ujenzi wa machinga complex mahali lilipo soko kuu la Arusha zinaendelea na wakuhamishwa wameshapewa taarifa.

Hizo ni baadhi tu ninazozifahamu mm. Tatizo ni kwamba hazitangazwi.

Kuhusu viongozi wa kitaifa, Dr Slaa walikuja Arusha na kufungua matawi ya cdm maeneo mbalimbali hapa mjini. Hiyo ni kuimarisha chama. Tayari cdm wamefungua ofisi yao ya mkoa huko Ngarenaro.

Mwisho naomba kukukumbusha viongozi wa cdm taifa hawawezi kuchoka kushughulikia swala la Arusha eti kwa sababu kuna matatizo sehemu nyingine. Hili wamelivulia nguo na wanalioga maana hakuna kukata tamaa wala kulala hadi kieleweke. Hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa. Na wananchi wa Arusha wanapodhulumiwa haki yao, haiwezekani kuwasaidia nusu halafu uwaachie. Lazima kufika mwisho!
 
Tokea kukamilika kwa uchaguzi mkuu wa 2010, viongozi wa CDM wamekuwa very busy kuhangaika na uchaguzi wa meya wa arusha tuu, hali hii imeanza kutukatisha tamaa sisi wapenzi na washabiki wa CDM kwa kuwa hivi sasa taifa linakabiliwa na matatizo kibao kupanda kwa gharama za maisha, kushuka kwa thamani ya shilingi yetu na hivi karibuni Seikali kushindwa kutimiza majukumu ya kifedha. Aidha watendaji mbali mbali serikali na taasisi na mshiriki ya umaa waliowekwa kimkakati katia asasi hizo wamefungulia ufisadi wa kutisha kwa kufuja fedha za ummma kama kwamba dunia na Tanzania ndio inafikai kikomo.

Che kushungaza wakati haya yote yakitokea viongozi wa CDM hawaonekani kujishughulisha kutaka kuleta mabadiliko katika matatizo haya badala yake kila siku ni uchaguzi wa meya Arusha. Halafu wanatutaka tuandamane nchi nzima kwa ajili hiyo.

Sio ombi tena tunawataka viongozi wetu wawaachie wat wa Arusha mamabo yao na waanze mara moja kushughulikia kero zinazotusumbua kama Taifa. Na huyo anayejiita Ndg Heche tokea achaguliwe kushika wadhifa wa Uenyekiti wa BAVICHA hatujamuaona kuja mitaani kuimarisha chama leo anatutaka kupitia vyombo vya habari tukaandamane tena kwa sababu zisizo na msingi wowote.

CDM tifani acheni kufikiria ndani ya boksi tu, tokeni ndani ya boksi muone hali halisi nje ikoje; ama sivyo mtkuja kujikuta mko peke yenu. Waulizeni akina Mrema, Lipumba n.k

Unatafuta bwana?
 
Kwanza kabisa wewe haujui ki undani kwanini chadema wanaandaa maandamano haki hakuna katika Tanzania ya leo,uchaguzi wa meya haukua wa haki namaanisha wakazi wa arusha wamenyimwa haki yao ya msingi ya kuwa na meya kutoka kwenye chama wanachokipenda na kilichoshinda kwa kishindo,kaka inaelekea unashsbikia CCM wanavyotumia ubabe kuendesha nchi hii? wewe ndio hautaki wananchi wa Arusha wanataka haki ndio maana wapo mstari wa mbele kutetea haki yao msitumie sababu zisizo na msingi kukizoofisha chama cha chadema.Sina chama mimi ni mwana harakati fikiri kabla ya kutenda

Hivi umeona umeya wa Arusha na maandamano ndio suluhisho la matatizo ya watanzania. Tunataka maendeleo sio malumbano yasio na tija wala maslahi kwa watnznia
 
Unaweza kuniambia hicho chma kinajemngwa wapi? hatuoni matawi mapya kufunguliwa, watu wanaotaka kadi za CDM hawajui zinzptikana vipi kila kukicha ni masuala ya meya mmoja tu. Umesahau ahadi za Dr SLaa kuwa kwa kutokuwa bungeni atapa fursa nzuri ya kukuza na kuimarisha chama hadi ngazi za mashina, Sasa haya masuala ya umeya wa Arusha ndio kukuza chama hadi ngazi ya shina?

Hoja yako ni nini? Toka lini JF imekuwa ukumbi wa kujadli mambo ya kufanywa na CDM nje ya taratibu za chama chao. GROW UP
 
Hivi umeona umeya wa Arusha na maandamano ndio suluhisho la matatizo ya watanzania. Tunataka maendeleo sio malumbano yasio na tija wala maslahi kwa watnznia
Join Date : 2nd November 2011, Posts : 3, Rep Power : 0 Kadai maendeleo kwa chama cha magamba kwa kuwa wamekuwa madarakani miaka 50. Sehemu ya maendeleo ni maisha bora kwa kila mtanzania ambayo yamegeuzwa kuwa bora maisha. Halafu mwambie aliyekutuma akutayarishe kutoa maoni hapa. Hapa si uwanja wa mazoezi
 
[/INDENT][/COLOR]

Dr.W.Slaa,

..nimesikitishwa na kauli yako niliyoi-highlight with red.

..kuna mahala pengine ulitumia maneno kama hayo kwa kiongozi ambaye sitapenda kumtaja hapa.

..kama kiongozi anayetafuta ridhaa ya kuongoza nchi nadhani ingependeza kama ungeachana na kauli kama hizo unapo-respond kwa maswali ya wananchi, hata kama maswali hayo yanakera.

..ungemjibu tu Watanabe, kwamba CDM mmefanya mikutano kadhaa, na suala kama muuliza swali ni "mvivu wa kufikiri na kutafiti" ungetuachia sisi tuamue.

..natumai utazingatia ushauri wangu wenye nia njema.

Umejibiwa hivi kwa sababu we ni mmoja wa wavivu wakufikiri. Toka lini umekuwa zaidi ya mshauri wa slaa kiasi cha kumuamuru azingatie ushauri wako? Ebu washauri vizuri waliokutuma na uwasisitizie wazingatie ushauri wako kama hawajakuona ni mpuuzi fulani
 
Huwezi zungumzia maendeleo yoyote katika nchi inayogandamiza haki na utu wa viongozi isiyoheshimu misingi ya demokrasia, suala la umeya wa Arusha wewe unachukulia kama kitu kirahisi, mimi nakuambia ukiona jambo lolote liliwahi kufanikiwa lisilokuwa na misingi mizuri. Sikubaliana na wewe kukata tamaa, vumilia ukombozi hauko mbali.
 
Mimibaba,

..soma jibu la Filipo post # 26 utaelewa nazungumzia nini.

..Filipo katoa maelezo ya kutosha bila kumuumbua muuliza swali, kwa kauli kama "mvivu wa kufikiri ..."

..sidhani kama ni vizuri kwa Dr.Slaa kutumia maneno makali kwa watu wanaomuuliza maswali.

..
 
Ni kweli waache ya Arusha harafu washirikiane na CCM Kuua watu na kupiga mabomu kama vile walivyowaua wamachinga Mbeya na kuwapiga mabomu,na vilevile washirikiane na CCM Kuwanyima mikopo wanafunzi wa UD na kuwapiga mabomu na kuwakata,washirikiane na CCM Kuwaibia watanzania madini na kuwafanya kuwa maskini,wawe wanasafiri kila siku ulaya kwa kodi za watanzania,wawe wanashirikiana kuwanyanyasa wananchi na kuwagandamiza.
 
Hivi umeona umeya wa Arusha na maandamano ndio suluhisho la matatizo ya watanzania. Tunataka maendeleo sio malumbano yasio na tija wala maslahi kwa watnznia

unataka maendeleo kutoka chadema mjinga nn, chadema ina kusanya kodi..chadema inaibana serikali tu kama ilivyo fanya kwenye swala la sukari na vyakula..
 
watanabe,
Mawazo yako ni kielelezo cha uvivu wa kufikiri na kutafiti .
I.Chama gani zaidi ya Chadema kimezunguka zaidi ya mikoa 13 na majimbo yote ya mikoa hiyo tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana?
2. Mbona huelezi kwanini JK hadi sasa hajafanya ziara ya kutoa shukrani na kutatua kero za kitaifa?
3, kama wewe hujui ajenda za chadema kwenye mikutano hiyo waulize wa tz wakiwemo wa mbeya.
4. Enziza propaganda na upotoshaji zimeisha.

Nashukuru sana kwa kuchukua muda kidogo kujibu hoja zangu.
Umesema CSDM imezenguka zaidi ya mikoa 13 na majimbo yake na kufananisha ziara hizi na za JK. Kwa bahati mbaya sana sikuwa nimezungumzia ziara mikoani ili nilizungumzia matatizo yanayolikabili taifa hili, mengine yakiwa mapya kabisa kwa maana hayakuwepo kabla ya uchaguzi kama vile Serikali kuonyeasha dalili za kufilisika na mfumuko mkubwa wa bei. Badala ya kila siku CDM kuonekana inagombea meya mmoja ingetuhamasisha tuandamane kuhusu matatizo haya. Kwa taarifa za uhakika nilizo nazo hata wanaokuja katika mikutano na maandamano ya arusha wanataka hilo lakini bado CDM inaonekana kucheza makida mkida kwa sababu ya meya mmoja tu.

Umezungumzia kuhusu ajenda za CDM na kutoa mfano wa mbeya. Na mwisho ukazungumza kidogo kuhusu propaganda. Kwa maoni yangu kudai mapambano ya wamachinga wa mbeya na polisi ni matunda ya CDM hizi propaganda za kisiasa ambzo sikuzitarajia kutokakwa msomi wa calibre yako. Kwani nafahamu dhahiri shahiri kuwa ukosefu wa ajira (unemployment) ndio unaowasukuma vijana wale kupambania haki yao ya kuendesha biashara zao pale walipopazoea.

Hivi inawezekana vipi wewe kama Katibu Mkuu wa CDM ushindwe kuwaongoza wabunge 45 tu kuwa na msimamo mmoja kuhusu hoja ya yenye maslahi makubwa ya kisiasa kama ya kufutwa kwa posho halafu leo uje kudai kuwa mapambano ya wamachinga na polisi ni mafanikio ya CDM.
Hoja nyepesi nadhaifu kama hizi ni dalili za wazi kabisa kuwa licha ya kuwa sasa wewe ni mtumishi wa chama unshindwa kutekeleza ahadi zako ulizokuwa ukitoa wakati wa kampeni ikwemo:-
a) Kuwaongoza wabunge wetu kumudu kutekelza ahadi kama ulivyoweza kutekeleza katika jimbo la Karartu wakati ulipokuwa mbunge; kinachoshuhudiwa sasa ni kila mbunge na lwake.
b) Kuimarisha chama hadi ngazi za mashina.

Kwa bahati mbaya viongozi wa kiafrika hususan Tanzania huwa hawataki kukosolewa, lakini lazima ukumbuke kuwa kura zako na za wabunge wa CDm hamkujiombea wenyewe; tulikuwepo tuliowaombea kwa lengo la kufanikisha mabadiliko katika TZ. Sasa huo ujumbe niliotoa ndio ujumbe wa wengi niliowafikia kuwaomba kura zao mwaka 2010 kuwa TZ sio meya wa AR tu.
 
Watanabe unapima watu wazima akili, haishangazi kwanini Dr. Slaa akakupa jibu alilokupa maana hajakutukana.
 
Unaweza kuniambia hicho chma kinajemngwa wapi? hatuoni matawi mapya kufunguliwa, watu wanaotaka kadi za CDM hawajui zinzptikana vipi kila kukicha ni masuala ya meya mmoja tu. Umesahau ahadi za Dr SLaa kuwa kwa kutokuwa bungeni atapa fursa nzuri ya kukuza na kuimarisha chama hadi ngazi za mashina, Sasa haya masuala ya umeya wa Arusha ndio kukuza chama hadi ngazi ya shina?

Wewe ni kisiki maana hata nikisema uko kama elimy ya Manyama nitakuwa nimekupa sifa .Ujenzi wa chama Chadema una anza na haki za msingi za umeya .Mliwanunua mkadhani mnaikomoa Chadema kumbe mmekalia kaa la moto .
 
[/INDENT][/COLOR]

Dr.W.Slaa,

..nimesikitishwa na kauli yako niliyoi-highlight with red.

..kuna mahala pengine ulitumia maneno kama hayo kwa kiongozi ambaye sitapenda kumtaja hapa.

..kama kiongozi anayetafuta ridhaa ya kuongoza nchi nadhani ingependeza kama ungeachana na kauli kama hizo unapo-respond kwa maswali ya wananchi, hata kama maswali hayo yanakera.

..ungemjibu tu Watanabe, kwamba CDM mmefanya mikutano kadhaa, na suala kama muuliza swali ni "mvivu wa kufikiri na kutafiti" ungetuachia sisi tuamue.

..natumai utazingatia ushauri wangu wenye nia njema.

Joka kuu wewe huoni kwamba mtu kusema ukweli na watu kuambiwa ukweli ndilo jibu pekee la matatizo au wewe kila kitu kiwe siasa ?
 
Back
Top Bottom