CHADEMA malumbano na CCM yamezidi, angalia msiwasahau wapiga kura wenu msije poteza viti 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA malumbano na CCM yamezidi, angalia msiwasahau wapiga kura wenu msije poteza viti 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mantuntunu, Nov 14, 2011.

 1. M

  Mantuntunu Senior Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mie ni Mwanachama wa Chadema, lakini naona kama hawa wabunge wetu wanatumia muda mwingi jukwaani. Chonde msiwasahau wananchi majimboni kwenu msije poteza nafasi zenu mwaka 2015.

  Najua kuna umuhimu kuendelea kukoleza moto wa mageuzi kwa ajili ya 2015 manake watanzania bila kukumbushwa kumbushwa husahau haraka sana. Wapiga kura wenu ni lazima waone tofauti ya maendeleo baada ya nyie kushika nyadhifa za ubunge na kabla ama mtang'olewa kama wakina marsha wa ccm na kupoteza maana nzima ya upinzani.
   
 2. M

  Malova JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 775
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  uko sawa kabisa, inabidi wafanye kila kitu kwa kiasi wasielemee upande mmoja
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,322
  Likes Received: 875
  Trophy Points: 280
  jitahidi kufanya utafiti badala ya kuzungumza kwa hisia mbunge yupi hayuko jimboni kwake
   
 4. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwenye reds inaonyesha kuwa unajua umuhimu wa kupigania haki na kuwaamsha wananchi. Bila Operesheni Sangara, ambayo iliibua mpaka Kagoda ni watu wangapi walikuwa wakiifahamu na kuiunga mkono Chadema! Mikutano na Wananchi inamchango mkubwa sana katika kukijenga Chama na hakumzuii Mbunge kuleta maendeleo
   
 5. M

  Mantuntunu Senior Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu wewe ndo unazungumza kwa hisia, hebu soma vizuri mchango wangu, sijasema hawapo majimboni mwao nimewaasa wasielemee upande mmoja wakasahau hasa umuhimu wa kuwaletea wapiga kura wao maendeleo.
   
 6. u

  ureni JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,073
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye nyekundu chadema wataleta maendeleo gani?kwani wao ndio waliokamata dola?wakienda bungeni kutetea wananchi wao inakua ngumu kwa sababu ya uchache wao,Ni vigumu CDM kukuletea maendeleo kwa hapa Tanzania na katiba ya zamani kama hawana dola otherwise ifanyike marekebisho ya katiba.
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,176
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145

  Ni mwanachama lakini bado mchanga kisiasa.
   
 8. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kuwa jimboni na kutekeleza yale aliyoyaahidi ni vitu viwili tofauti kabisa. Wengi wao hata kupokea simu za watu waliokuwa wakiwafanyi8ka kampeni hawataki sasa watapata vipi habari yanayojiri kwa wananchi.
   
 9. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unazungumza kana kwamba hukuwa unahudhuria mikutano ya kampeni. Kuna mahali popote katika mikutano ya kampeni walisema CDM isipokamata dola hawatatekeelza ahadi walizotoa?

  Hata kama cdm haikukamata dola ni lazima waonekane wakijitahidi kutekeleza ahadi walizotoa. Kwa njia hiyo hata wakishindwa wananchi wataelewa kuwa walijitahidi lakini walishindwa.

  Lakini kwa wananchi wako huonekani kali siku wanasikia uko katika maandamano haya na yale watakuelewa kweli. Katika hilo lazima nimpongeze Mhe Halima Mdee ambaye tunamshuhudia akichapa kazi jimboni hata cdm haikukamata dola, huyu huwezi kumsikia akikimbilia maandamano yasiyo na mana yoyote.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 145
  Uhuru wa maoni hauna uchanga...hawa wanasiasa wapya ni muhimu sana Tuna washauri wazuri tu ambao si wanasiasa. Indeed ni mawazo ya neutrals or naive people that play significant role in swinging political direction

  yawezekana mawazo yake hayajakamilika.. Lakini msaada kimawazo ungemsaidia zaidi
   
 11. u

  ureni JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,073
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapo kwenye nyekundu, maanadamano wakati mwingine lazima yawepo ili kushinikiza haki ipatikane kama njia ya majadiliano imeshindikana.

  Wewe angalia kama itatengenezwa katiba ambayo inaleta upendeleo wa kimaslai kwa watu fulanifulani na sio kwa wananchi wote na unaiona kabisa haifai ni lazima ifanyike njia mbadala ya kushinikiza irekebishwe na njia mojawapo ni maandamano.

  Kama katiba ni mbovumbuvu hata ukifanyakazi kama Halima Mdee maendeleo hayatapatikana ni ndoto.Na ujue katiba mbovumbovu itakapopita wewe na familia yako na wajukuu mtateseka kwa miaka 50 ijayo tena.
   
 12. M

  Mantuntunu Senior Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante bwana MTM, manake wewe kweli ume-take time kusoma thread yangu, sikusema chadema wasiandamane la hasha maana yangu hasa nilimaanisha wabalance, iwe 50/50. Wasijisahau katika kujitahidi kuleta maendeleo katika majimbo yao wasije wakasahaulika. Wasingependa kupoteza majimbo ambayo wameyashika. Huyo Mzee wa Rula naona amenijibu kiushabiki!
   
 13. M

  Mantuntunu Senior Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yeah agree with you, ni vigumu cdm kuleta maendeleo katika nchi nzima ukizingatia mfumo uliopo bungeni kwetu wa kupiga kura, lakini wanaweza wakajaribu kwa kuanzia majimboni kwao.
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Maendeleo yataletwa na wale walioshika dola, utaletaje maendeleo na ww huna kisu cha rasilimali !
   
Loading...