Chadema: Maandalizi ya Kuuzuia Mkutano wa CCM Yameanza Rasmi

Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
563
433
KATIKA kutekeleza tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) la kufika Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma wameanza maandalizi ya kupokea vijana zaidi ya 2000, anaandika Dany Tibason.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Malambaya Manyanya, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma amesema, kwa sasa viongozi wa mkoa wameanza maadalizi ya kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa kuanza kuwasili tarehe 21na 22 Julai mwaka huu.

Amesema, maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana ambao watatoka katika mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuzuia mikutano na vikao vya CCM.

Amesema, kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi cha kufanya kazi ya maadalizi ya ugeni huo ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma kutekeleza kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa.

Amesema, maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao ni pamoja na viongozi wa kitaifa wa Bavicha kwa maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi ya chakula.

“Wapo watu ambao wanadhani Bavicha wana mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu wa nchi.
“Tumekuwa tukiona jinsi mikutano ya Chadema pamoja inavyozuiliwa, na sasa msimamo wa Bavicha wa kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa lengo la kubadilishana uongozi katika ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais msitaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli.

“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokuja Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM.

“Kwa sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la kuzuia mikutano yote ya siasa ikiwa ni vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi 2020.”
Amesema, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani na mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) na kuwa, sasa wanashirikiana na polisi kuhakikisha mikutano ya CCM haitafanyika” amesema Malambaya.
 
Lini uvccm/ ccm walishawahi kukusanyika na kuzuia mkutano wa chadema??

Kwa hiyo uelewa wa bavichaaa ndio huu?
23/7/2016 dunia itashuhudia kama sharubu za mkwe huwa zinachezewa au la
 
KATIKA kutekeleza tamko la Baraza la
Vijana wa Chadema (Bavicha) la kufika
Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi
kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma
wameanza maandalizi ya kupokea vijana
zaidi ya 2000.
Akizungumza na waandishi wa habari
mjini Dodoma jana Malambaya
Manyanya, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa
wa Dodoma alisema, kwa sasa viongozi
wa mkoa wameanza maadalizi ya
kuwapokea wageni wao ambao
wanatarajiwa kuanza kuwasili tarehe 21
na 22 Julai mwaka huu.
Alisema, maadalizi hayo ni ya
kuwapokea vijana ambao watatoka katika
mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la
kutimiza tamko la Bavicha taifa la
kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dodoma kuzuia mikutano na vikao vya
CCM.
Alisema, kwa sasa mkoa tayari umeunda
kikosi cha kufanya kazi ya maadalizi ya
ugeni huo ambapo kwa nia njema
utafika mjini Dodoma kutekeleza kauli ya
Rais John Magufuli ya kuzuia vikao
vyote na mikutano ya vyama vya siasa.
Alisema, maadalizi hayo ya kuwapokea
vijana hao ni pamoja na viongozi wa
kitaifa wa Bavicha kwa maana ya
kutafuta mahali pa kulala na maandalizi
ya chakula.
“Wapo watu ambao wanadhani Bavicha
wana mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka
kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza
kauli ya mkuu wa nchi.
“Tumekuwa tukiona jinsi mikutano ya
Chadema inavyozuiliwa, na sasa msimamo
wa Bavicha ni kuzuia mkutano ya CCM
unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa lengo
la kubadilishana uongozi kati ya mwenyekiti
wa sasa wa CCM na rais msitaafu wa awamu
ya nne Jakaya Kikwete na Rais John
Magufuli.
“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka
mikoa yote nchini watakaokuja Dodoma
kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya
mkutano usio halali wa CCM.
“Kwa sababau mkuu wa nchi ametoa tamko
la kuzuia mikutano yote ya siasa ikiwa ni
pamoja na vikao vya ndani na mikutano ya
hadhara hadi 2020.” Alisema Malambaya.
Alisema, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano
ya vyama vya siasa vya upinzani na
mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa
Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) na kuwa,
sasa wanashirikiana na polisi
kuhakikisha mikutano ya CCM
haitafanyika.

ndoto za mchana hizo.
 
Hongereni sana ccm kwa kuwa na ukumbi mzuri na wa kisasa. Lakini mmenisikitisha mambao mlioweka huko kati kati maana zaweza kuwa silaha pale inapotokea chochote "penye wengi...." Hivyo best option ilikua na kuvipa viti vyote number kisha kila mkoa/wilaya wanapewa vitambulisho vyenye number kulingana na wilaya ama mkoa atokao.

All the best kwenye mkutano wenu na mmalize salama
 
Hongereni sana ccm kwa kuwa na ukumbi mzuri na wa kisasa. Lakini mmenisikitisha mambao mlioweka huko kati kati maana zaweza kuwa silaha pale inapotokea chochote "penye wengi...." Hivyo best option ilikua na kuvipa viti vyote number kisha kila mkoa/wilaya wanapewa vitambulisho vyenye number kulingana na wilaya ama mkoa atokao.

All the best kwenye mkutano wenu na mmalize salama
Green guard wapo wa kutosha
 
Back
Top Bottom