Chadema: Maandalizi kuikabili CCM yameanza

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
KATIKA kutekeleza tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) la kufika Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma wameanza maandalizi ya kupokea vijana zaidi ya 2000, anaandika Dany Tibason.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Malambaya Manyanya, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma amesema, kwa sasa viongozi wa mkoa wameanza maadalizi ya kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa kuanza kuwasili tarehe 21na 22 Julai mwaka huu.

Amesema, maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana ambao watatoka katika mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuzuia mikutano na vikao vya CCM.

Amesema, kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi cha kufanya kazi ya maadalizi ya ugeni huo ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma kutekeleza kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa.

Amesema, maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao ni pamoja na viongozi wa kitaifa wa Bavicha kwa maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi ya chakula.

“Wapo watu ambao wanadhani Bavicha wana mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu wa nchi.

“Tumekuwa tukiona jinsi mikutano ya Chadema pamoja inavyozuiliwa, na sasa msimamo wa Bavicha wa kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa lengo la kubadilishana uongozi katika ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais msitaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli.

“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokuja Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM.

“Kwa sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la kuzuia mikutano yote ya siasa ikiwa ni vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi 2020.”

Amesema, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani na mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) na kuwa, sasa wanashirikiana na polisi kuhakikisha mikutano ya CCM haitafanyika” amesema Malambaya
 

Attachments

  • Chadema.jpg
    Chadema.jpg
    12.7 KB · Views: 62
Nawashauri hao vijana wafanye kazi muda wa kutumiwa Na wanasiasa umeisha....

Akina Mbowe wakikwaruzana Na serikali wanajilipa posho za kutosha Na Mawakili wazuri kwa fedha Chama.

Juzi tu Lissu kapewa Mawakili kumi Na saba kwa gharama za chama, sasa sijui wao watagharamiwa Na nani.
 
Nawashauri hao vijana wafanye kazi muda wa kutumiwa Na wanasiasa umeisha....

Akina Mbowe wakikwaruzana Na serikali wanajilipa posho za kutosha Na Mawakili wazuri kwa fedha Chama.

Juzi tu Lissu kapewa Mawakili kumi Na saba kwa gharama za chama, sasa sijui wao watagharamiwa Na nani.
Hapo fujo ipo wapi watu wanaoshirikiana na Polisi?
 
Ushauri kwa CHADEMA: kwakuwa wawakilishi wa vijana hao wakiwepo wabunge wao. Ni vema wakaenda wao kwakuwa kwa kwenda kwao watakuwa wamewawakilisha vijana takribani zaidi ya milioni, na si kwa kutumia unyumbu style. Halafu huyo jamaa anafanya propaganda nyepesi mno.. hizo ni kelele za chura!! Namalizia kwa kuwasisitiza kuwa msiende huko Dodoma kwa ushabiki!! Majuto ni Mjukuu!
 
Mbona mnaingiwa na hofu acheni Bavicha Wafanye mkutano wao ilimradi hawavunji amani.
 
Ningekuwa polisi siku hiyo ningempiga nyumbu mmoja rungu la kiuno ili liwe funzo kwa nyumbu wengine.
Ningechonga rungu maalum kama la Kipepe maana ningehakikisha navunja kiuno cha hawa vijana wadogo wanaowatumikia mafisadi.
 
10.jpeg

VIJANA CHADEMA A.TOWN TUKO NJIANI KWENDA DODOMA GARI SABA KUBWA TUNAKWENDA KUISAIDIA POLICE KWASABABU RAIS ALITOA TAMKO KUWA HAKUNA MIKUTANO YA SIASA.FULL STOP.

swissme
 
Nawashauri hao vijana wafanye kazi muda wa kutumiwa Na wanasiasa umeisha....

Akina Mbowe wakikwaruzana Na serikali wanajilipa posho za kutosha Na Mawakili wazuri kwa fedha Chama.

Juzi tu Lissu kapewa Mawakili kumi Na saba kwa gharama za chama, sasa sijui wao watagharamiwa Na nani.
Wale walio shikwa na mabango Kisutu ya kumkashfu Rais sijui kama uongozi ulirudi kuwa tetea, hii mizuka mingine bahna utawapa shida watoto na familia yako wakati Mbowe na viongozi wenzake watt wao wakiwa hawana wasiwasi! Mm nashauri tupige kazi siasa za kina mbowe zitagharimu maisha ya watu
 
Back
Top Bottom