CHADEMA, Maalim na ACT Wazalendo kuweni makini kuliko umakini wenyewe

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Siku chache kabla ya hukumu ya Makama Kuu iliyohitimishwa kwa Maalim Seif kuporwa chama cha CUF niliandika makala nikianisha vidokezo vichache juu ya mwelekeo wake baada ya uporaji huo, Sikuandika kwa bahati mbaya, la hasha, nilimaanisha hasaa. Makala yangu ilikwenda kwa kichwa kisemacho "Maalim Seif anakwenda ACT? Litakuwa kosa la karne kwa Wazanzibar na Zanzibar HURU".

Kwanza niweke wazi, mimi ni mwanachama hai wa Chadema na ni kiongozi mwandamizi, vivyo hivyo mimi ni mchambuzi huru, na katika suala la Maalim Seif mimi nasimama kama mchambuzi huru, Baado makala yangu ya wiki jana ya angalizo kwa Maalim ni mbegu iliyomea na haitanyauka kamwe, Kwamaoni yangu nikiwa huru kabisa, Maalim Seif amezungukwa katika kuchagua wapi ajiunge kuendeleza mapambano, naamini amefanya kosa, litakougharimu upinzani nchini ikiwa Chadema haitaucheza mchezo huu kwa umakini, lakini litakinufaisha chama cha ACT tu sio upinzani mzima nchinj wenye kuitikisaa ccm, kwasababu walioratibu na kufanikisha yeye Maalim kujiunga ACT ndio walimpora chama na kwa tafsiri hiyo hao ndio wenye kura ya veto ACT, hawa wanaitwa wapembe nuksi.

Awali katika makala ile nilieleza kuwa, "Upinzani unamuhitaji mwanasiasi yoyote mwenye ufuasi, si kwamba katika kugombea, bali katika kuongeza wigo wa kitaasisi. kuelekea mapambano mapya. Ninaweza kuona na kutamka kwamba CUF haitarejea tena mikononi mwa wanacuf, itabaki mikononi mwa ccm hadi unyakuo wa ibilisi.

Nini mstakabali wa siasa za Zanzibar bila CUF? Ni dhahiri itikadi ya CUF ilibebwa na sera yake ya Uhuru wa Zanzibar mpya, Zanzibar ikawa Cuf, na Cuf ikawa Zanzibar, leo watwana wamepora chama kinakula na kulala viunga vya Lumumba. Nini mstakabali wa Zanzibar? Jibu lipo kwa Maalim Seif,

Maalim akichanga karata "vibaya" tu kupitia washauri wake, Nakuambieni, ameua ndoto za wazanzibar. Wataalamu wa siasa wa ccm kwa mara ya kwanza naweza kuwasifu mchezo wanaoucheza ni hesabu kali. Maalim Seif kujiunga Chadema ni kuongeza nguvu ya upinzani na kuhatarisha maisha ya ccm hasa kuelekea 2020. Maalim Seif kujiunga Jahazi Asilia ni kukikuza chama hicho na kupunguza upinzania kwa Tanzania. Vivyo hivyo Maalimu kujiunga ACT ni kukikuza chama hicho na kuwa chama chenye ufuasi katika siasa za upinzania kisicho na madhara kwa ccm. ACT haina chaguo katika mapambano haya isipokuwa ni kujiunga katika umoja wa vyama pinzani. Hili linategemea hulka zaidi za kiongozi wa chama hicho.

Kwenye karatasi za CCM vitu hatari kwao ni Chadema na muunganiko wao. Membe sihatari kwa ccm, bali hatari kwa mwenyekiti tu, na hilo linatoa kura ya veto kwa mwenyekiti kumnyanganya kadi ama mshurutisha ahame chama, Katika kuhama chama ndipo wataalamu wa siasa (TISS) watainjinia aina ya uhamaji na uelekeo wa Membe ambao hautaathiri CCM".

Nikaeleza tena kwamba, "Siasa ni hesabu kali sana, zinapigwa maili milioni kwenda mbele, Tiss wajanja sana wakitaka kuiua Chadema watainjinia Membe na maalim wajiunge na Zitto, na hawatakuwa na nguvu kwa ccm, lakini watakuwa wameibomoa Chadema ambayo inaisumbua ccm. Hivi ndivyo inavyoweza kuwa, ukizingatia sheria mpya ya vyama vya siasa ilishapitishwa lakini haisainiwi hadi mipango hii ikamilike, kwani sheria hiyo inazuia mwanachama akifutwa/kujiuzuru uanachama atalazimika kukaa miaka miwili ndipo ajiunge na chama kingine"

Baada ya kunukuu hayo toka kwenye makala yangu ya wiki jana, sasa naomba tazama mtiririko huu kisha anza kuunganisha dot na dondoo kadhaa nitakazokupatia, zitakusaisia kuelewa nini hasa namaanisha ninaposema Chadema, Maalim na ACT wawe makini kuliko umakini wenyewe;

Hukumu ya Kesi ya CUF ilitolewa Jumatatu mapema Machi 18, 2019 na Jaji Dk Benhajj Masoud. Siku hiyohiyo bila hada kupoteza sekunde, Maalim alitangaza kujiunga na ACT Wazalendo. Na hata kabla hajarudi nyumbani Zanzibar, kesho yake akakabidhiwa kadi, habari kutoka vyanzo vya mfumo zinasema hatua hiyo wanamkakati walishauri Maalim atangaza mapema sana kabla viongozi wa umoja wa UKAWA hawajaenda kumuona na kumpa pole kwani watambadili msimamo na kumshauri ajiunge na Mbowe, Mbatia, nk.

Kumbuka kesi hii imetolewa uamuzi siku chache tu baada ya mwenyekiti mwenza wa Ukawa Mheshimiwa Mbowe kutoka mahabusu alikokaa kwa siku 104, katika busara ya kawadi Maalim angeweza kukutana na viongozi wenzake wa Ukawa kabla ya hukumu au baada ya hukumu na kushauriana kama sio kusalimiana, kupeana pole na kuagana. Kumbuka vyama vya UKAWA hata kimoja hakikupata fursa ya kumuona mjumbe mwenzao (Maalim) baada ya kesi na kumpa pole isipokuwa Zitto tu. Hapa dot inaanza kuunganishwa na kule juu makala ya wiki jana.

Tarehe 30 Januari 2019 mswada wa sheria ya vyama vya siasa ulipitishwa na Bunge na siku hiyohiyo jioni ukawasilishwa mezani kwa Rais ili kutiwa saini uwe sheria, na siku 14 baadae yaani tarehe 13 Februari 2019 Rais akasaini, ambapo kwamjibu wa sheria za nchi mswada ukishasaini unatakiwa kutangazwa katika gazeti la serikali ndipo uanze matumizi yake. Lakini katika hali ya kustaajabisha na kutafsiri wazi ninachokuelezeni, mswada huo umechukua mwezi mzima kutangazwa gazetiji hadi jana tahere 22 Machi 2019 ndipo umechapishwa na sasa ni sheria kamili na utekelezaji wa sheria hiyo umeanza jana hiyo. Kwakukufahamisha tu, sheria hiyo inavifungu vinavyodhibiti uhamahamaji wa wanasiasa kwamba ukihama chama au ukifukuzwa au kujiuzuru, utatakiwa kukaa miaka miwili ndipo ujiunge chama kingine na kugombea uongozi.

Lakini hatua hii leo imefikiwa baada tu ya mchakato wa Maalim kujiunga na ACT. Yaani hakuna sababu yoyote yamsingi iliyotolewa na serikali kwamba kwanini tangu rais asaini sheria hiyo mwezi wa pili tarehe 13 hadi jana mwezi wa tatu tarehe 22 walikuwa hawajachapisha. Hili linafanya kuweka dot itakayotusaidia kuunganisha na mengine.

Mkutano wa vyama kule Zanzibar uliozaa AZIMIO la ZANZIBAR, haukuwa wa UKAWA, Bali uliandaliwa nje ya ukawa na vyama hivyo vikaalikwa tu, hakuna shaka kwamba waandaaji wa mkutano huo ndio waratibu wa namna ya uelekeo wa Maalim akitoka CUF, hili wenyewe wanasema hata Maalim hadi leo hajui. Vyama vimekuja kustuka huku vikiwa vimechelewa, wapanga mikakati wanevitumia vya Ukawa kufanikisha agenda yao. Hii ni dot ya tatu endelea kuunganisha.

Ziko kauli mbiu za kisiasa ambazo zinaashiria mwelekeo hasi wa malengo ya kisiasa, Mwelekeo huo unakubaliana na tetesi kutoka koridi za wanamikakati kwamba wao hawautaki upinzani wa Chadema kwakuwa una athiri chama tawala na serikali kwa nguvu kubwa ndani na nje ya nchi, kwamba kukatwa kwa misaada toka kwa mabeberu ni kwasababu ya chadema, hivyo wataalamu wa mbinu wa ccm (TISS) wanataka kujenga aina mpya ya siasa ambazo zitakuwa rafiki kwa ccm na serikali yake.

Hili linaanza kutiliwa jicho la shaka baada ya Maalim kujiunga ACT kumezaliwa kauli mbiu inayofanana na hoja ya hapo juu, kwamba sasa ACT ni #TheFutureIsBright ama #TheFutureIsPurple, kwa tafsiri ya kawaida kauli mbiu hizo hazina nia njema ya kuungana ama kushirikiana na Chadema kwakuwa chadema sio #TheFutureIsBright na #TheFutureIsPurple kama inavyotafsiriwa kimantiki na makada hao. Kwa kauli hii kwa wana-ACT wanaona Chadema sio Future Purple kwao. Hili likikubalika liimbwe na wanachama wa vyama vingine (Chadema) maana yake watakuwa wote wamehama nakuinadi ACT na kuacha vyama vyao.

Si kauli mbiu ya kimaungano bali ya kibinafsi yenye unafiki. Ifahamike wazi, ACT kama chama hakina makubaliano na vyama vya Ukawa kuwa wamoja. Isipokuwa Mbunge wake ndie ameomba kuwa sehemu ya wabunge wa Ukawa Bungeni ili kusimamia baadhi ya hoja, hivyo kuna makubaliano ya kibunge tu sio ya kichama. Na wale wanaoonekana kukosoa ujio wa Maalim ACT, zimeibuka kauli mbiu kwamba "Chadema na ACT tusikubali kugawanywa kwamba wako watu wanaotugawa". Hizi ni hoja za kijinga kabisa, Mtu mkubwa kama Maalim ahame chama kisha asijadiliwe katika pande zote? Haitawezekana acheni watu wajadili.

Lakini kubwa zaidi, Kauli ya Maalim Seif wakati akiongea na mtandao wa Kwanza Tv ameidhihaki sana Chadema ambayo viongozi wa ACT wanasema ni washirika, mshirika hatolewi dhihaka bali hufarijiwa kuheshimiwa tena kwa chama kikuu cha upinzani kama Chsdema. Katika mahojiano akijibu swali la mtangazaji Maria Sarungi kwamba kwanini amejiunga ACT, alisema, "Kwasasa chama kinachoaminika ni ACT, katika vyama bora tulivyoongea navyo tukafuata chama bora zaidi nacho ni ACT". Kwahakika maneno hayo kwa mwanachama makini anayelinda na kutetea chama cha hatafurahishwa kuambiwa hivyo na atalazimika kujitafakari juu ya ombi la kuungana na mtu anayekudhihaki hivyo.

Narudia, Chadema, Maalim na ACT kuweni makini kuliko umakini wenyewe, kwasasa muhanga wa dola ni Chadema, ACT sio tishio kwa dola bali ni silaha ya dola kuangamiza upinzani nchini baada ya kuhakikisha wanempora chama Maalim, watawala wanaamini Maalim aliyekwenye mikono ya Zitto ni mwepesi kuliko Maalim aliyekwenye mikono ya Chadema.

Njia ya haraka kuwadhibiti wanamfumo wa Lumumba walio ndani ya vyama vya upinzani, ni mbili tu, pamoja na sheria mpya ya vyama vya siasa kuweka masharti magumu, mfano kifungu cha 11A (2) kimeweka masharti juu ya vyama kushirikiana kuwa ni lazima vifanye hivyo miezi 3 kabla ya uchaguzi kufanyika, hali inayofanya kutafsiriwa kuwa ni kuingilia uhuru wa vyama kwani suala la kushirikiana linatokea kulingana na mazingira ya kisiasa ya wakati husika na hata kitendo cha kutaka Vyama kupeleka kwa Msajili hati ya makubaliano ya kuungana haina mantiki yoyote zaidi ya kuingilia uhuru wa Vyama husika.

Aidha Kifungu kidogo (2) kinasema kuwa ili Vyama vishirikiane ni lazima mikutano mikuu ya vyama hivyo ndio ifanye uamuzi huo. Huku ni kuingilia Katiba za vyama ambazo zimeweka utaratibu , kwa mfano kwa upande wa CHADEMA jukumu hilo lipo kwenye mamlaka ya Baraza Kuu Na sio Mkutano Mkuu.

Naaam, mosi, ikiwa Chadema itaona umuhimu wa mashirikiano na ACT, basi kiitishe mchakato wa makubaliano rasmi ambapo huo ukamilike kwa baadhi ya mambo kabisa yenye kujifunga katika umoja huo na sehemu ya hitimisho la makubaliano hayo isubiri takwa la kisheria linalosema hadi isalie miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kufanya hivyo kutadhibiti mahubiri ya usisi ya makada, na moja ya makubaliano ya awali iwe ni kuhuisha sera mbadala ya Chadema na kuifanya iwe ya umoja huo mpya ili makada na viongozi wahubiri popote walipo sera hiyo kuliko mahubiri ya The future purple na mengineyo yenye kuleta mgawanyiko.

Pili, Chadema iondoke katika dhana hii ya mashirikiano haraka sana na iwaaruhusu makada wao warejee kwenye siasa zao za asili za kikamanda zenye kuilaza ccm na viatu. Kufanya hivyo nikukiepusha chama kutumika kukijenga chama kingine kwa maslahi ya dola.

Na Yericko Nyerere
 
Leo nimekuelewa sana mkuu. Kitu rahisi kuhisi ni kama Zitto ni member wa St. Petersburg unit au la. Pamoja na harakati zake za kipinzani, bado namwona Zitto anafanya kazi za watu.
Kwanza ile U turn kutoka kuwa anamsifu Magufuli na kuponda "mazwazwa" na kuungana na "mazwazwa" haiko clear.

Tahadhari yako ina maantiki mkuu.
 
Narudia, Chadema, Maalim na ACT kuweni makini kuliko umakini wenyewe, kwasasa muhanga wa dola ni Chadema, ACT sio tishio kwa dola bali ni silaha ya dola kuangamiza upinzani nchini baada ya kuhakikisha wanempora chama Maalim, watawala wanaamini Maalim aliyekwenye mikono ya Zitto ni mwepesi kuliko Maalim aliyekwwnye mikono ya Lipumba.

Njia ya haraka kuwadhibiti wanamfumo wa Lumumba walio ndani ya vyama vya upinzani, ni mbili tu, pamoja na sheria mpya ya vyama vya siasa kuweka masharti magumu, mfano kifungu cha 11A (2) kimeweka masharti juu ya vyama kushirikiana kuwa ni lazima vifanye hivyo miezi 3 kabla ya uchaguzi kufanyika, hali inayofanya kutafsiriwa kuwa ni kuingilia uhuru wa vyama kwani suala la kushirikiana linatokea kulingana na mazingira ya kisiasa ya wakati husika na hata kitendo cha kutaka Vyama kupeleka kwa Msajili hati ya makubaliano ya kuungana haina mantiki yoyote zaidi ya kuingilia uhuru wa Vyama husika.

Aidha Kifungu kidogo (2) kinasema kuwa ili Vyama vishirikiane ni lazima mikutano mikuu ya vyama hivyo ndio ifanye uamuzi huo. Huku ni kuingilia Katiba za vyama ambazo zimeweka utaratibu , kwa mfano kwa upande wa CHADEMA jukumu hilo lipo kwenye mamlaka ya Baraza Kuu Na sio Mkutano Mkuu.

Naaam, mosi, ikiwa Chadema itaona umuhimu wa mashirikiano na ACT, basi kiitishe mchakato wa makubaliano rasmi ambapo huo ukamilike kwa baadhi ya mambo kabisa yenye kujifunga katika umoja huo na sehemu ya hitimisho la makubaliano hayo isubiri takwa la kisheria linalosema hadi isalie miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kufanya hivyo kutadhibiti mahubiri ya usisi ya makada, na moja ya makubaliano ya awali iwe ni kuhuisha sera mbadala ya Chadema na kuifanya iwe ya umoja huo mpya ili makada na viongozi wahubiri popote walipo sera hiyo kuliko mahubiri ya The future purple na mengineyo yenye kuleta mgawanyiko.

Pili, Chadema iondoke katika dhana hii ya mashirikiano haraka sana na iwaaruhusu makada wao warejee kwenye siasa zao za asili za kikamanda zenye kuilaza ccm na viatu. Kufanya hivyo nikukiepusha chama kutumika kukijenga chama kingine kwa maslahi ya dola.

Na Yericko Nyerere
Kamanda hivi hujui Mbowe na Mbatia ni makada? Hivi hujui kuwa dudu Ukawa ndilo liliibeba Chadema 2015?

Ila nikupongeze umekuwa mkweli kwa kuonesha hisia na vitendo kuwa uamuzi wa Seif na wafuasi wake umekuwa mwiba mchungu kwa Chadema na umeonesha wazi katika andiko lako.

Ni dhahiri mnatamani CCM iwaazime Membe, ombi lenu linafanyiwa kazi.

Wewe ni mmoja wa watu mliotumiwa kufanya ushirikina na hata kuua ingewezekana ACT na Zitto watoweke japo umeshindwa.Kama hila zenu dhidi ya Zitto zilishindwa Kati ya 2009-2015 hesabu maumivu.

Pia ni dhahiri huna taarifa kwamba sheria mpya ya vyama vya siasa imeshasainiwa.

Mwisho,nikupongeze kwa kukesha ukiandika hekaya zenye ramli lukuki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo nimekuelewa sana mkuu. Kitu rahisi kuhisi ni kama Zitto ni member wa St. Petersburg unit au la. Pamoja na harakati zake za kipinzani, bado namwona Zitto anafanya kazi za watu.
Kwanza ile U turn kutoka kuwa anamsifu Magufuli na kuponda "mazwazwa" na kuungana na "mazwazwa" haiko clear.

Tahadhari yako ina maantiki mkuu.
Jamaa alikuwa analazima sana muungano wa vyama vya upinzani, mpaka nikajiuliza nini kinachoendelea, anyway nina amin viongozi wakk makini naye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamanda hivi hujui Mbowe na Mbatia ni makada? Hivi hujui kuwa dudu Ukawa ndilo liliibeba Chadema 2015?

Ila nikupongeze umekuwa mkweli kwa kuonesha hisia na vitendo kuwa uamuzi wa Seif na wafuasi wake umekuwa mwiba mchungu kwa Chadema na umeonesha wazi katika andiko lako.

Ni dhahiri mnatamani CCM iwaazime Membe, ombi lenu linafanyiwa kazi.

Wewe ni mmoja wa watu mliotumiwa kufanya ushirikina na hata kuua ingewezekana ACT na Zitto watoweke japo umeshindwa.Kama hila zenu dhidi ya Zitto zilishindwa Kati ya 2009-2015 hesabu maumivu.

Pia ni dhahiri huna taarifa kwamba sheria mpya ya vyama vya siasa imeshasainiwa.

Mwisho,nikupongeze kwa kukesha ukiandika hekaya zenye ramli lukuki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fitina zenu zimekwama
 
Umedadavua vizur mtoa mada,ila hii kusema act si tishio kwa ccm hapo kidogo nishushe kwanza,hivi mtoa mada hujui nguvu alizonazo maalim upande wa zanzibar?labda ungesema act nguvu zake awekeze zanzibar na chadema nguvu zake awekeze tanganyika kwa jahazi la ukawa ili kumtoa huyu nduli ccm madarakani.

Inzi wa kijani mnaboa kweli,jadili hoja na sio kumshambulia mtoa hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, unazungusha mno na kuchosha!

Maalim alishaamua siku nyingi kwenda ACT, tokea ule mkutano wa Zanzibar, na wengi ndani ya UKAWA bila shaka walikuwa na taarifa hiyo.

Sasa hapa unaleta habari ndefu mno inayozunguka humo humo tu kiasi cha kumchosha na kumchanganya kichwa msomaji bila ya sababu yoyote.

Ndio, CCM wanaendelea na michezo yao ya kutafuta kila njia kuwadhibiti wote, sio CHADEMA tu, hilo halina mjadala na nyote mnalielewa vizuri.

Kama kusaini na kuchapisha hiyo sheria mpya kulitegemea uamzi wa Maalim, mbona wamempa mwanya, akahama ndipo wakachapisha, ili iweje?

Ukweli ni kwamba Maalim ndani ya CHADEMA ingekuwa shida. Huko ACT ndiko kulikomjaa tokea awali, na ilijulikana hivyo na wenye kutaka kujua.

Na kwa taarifa tu ni kwamba, hata angeingia CHADEMA, Urais Zanzibar kwa Maalim atakuwa anausikia tu kama hadithi fulani. Na ni kwa sababu hiyo hiyo itakayofanya CHADEMA au ACT kamwe wasiweze kuongoza Tanzania katika miaka hii ya karibuni.
Njia na chama pekee kinachoweza kujaribu ni CHADEMA, inayoweza kutengeneza "Tufani". Sasa hivi sioni wakiweza kuitengeneza 'tufani hiyo!

Wanasema "CCM itatawala milele." Maneno haya sio mzaha; yachukulieni kwa uzito wake.
 
Yeriko unasahau kitu kimoja CUF ilijengwa juu ya misingi fulani hivi ambayo kwa vyovyote vile ilikua ni ngumu sana kaa maustadh kuja chadema,
Pili chadema ni kama vile imepoteza muelekeo toka uchaguzi umalizike chama hakina agenda yoyote inayoisimamia wala kua na mawazo mbadala (na hii inatokana na kuondokewa watu makini walio kua nyuma ya pazia wenye uwezo wa kurise issues Kitilia, Dr Slaa pamoja na Zitto).
Kwa sasa mambo yote watu tunauo yapigia kelele au tunayoimba nayo kwa kiasi kikubwa yanaibuliwa na Zitto mfano korosho, kupigwa matrilioni na jiwe, ukiacha nyota ya Lissu ambayo Chadema inatembelea chama kama taasisi kimefeli sana tofauti na zamani, hivyo kabla ya kulalamikia kauli ya Maalim kua ACT ndio chama bora kwa sasa makamanda inabidi mjitafakari je Chadema ni ile ile au pumzi inaelekea kukata!!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umedadavua vizur mtoa mada,ila hii kusema act si tishio kwa ccm hapo kidogo nishushe kwanza,hivi mtoa mada hujui nguvu alizonazo maalim upande wa zanzibar?labda ungesema act nguvu zake awekeze zanzibar na chadema nguvu zake awekeze tanganyika kwa jahazi la ukawa ili kumtoa huyu nduli ccm madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maalim ni CCM ataitoaje CCM?
Last uchaaguzi alipinga matokeo kwa kwenda UK...
Easy
 
Back
Top Bottom