CHADEMA - Let bygones be bygones

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,817
2,000
Kwa wana CHADEMA wote,

Katika kipindi hiki, ambacho dunia nzima inamuaga Mandela, na kukumbuka mazuri yake mengi, ambayo
kwa sehemu kubwa, yalitokana na kuwasamehe wale wote waliomkosea na kumtesa jela kwa miaka 27.

Huenda ni muda muafaka kwa CHADEMA kusema enough is enough; let bygones be bygones; yaliyopita si ndwere na tugange yaliyopo; kwamba huu ugomvi wa viongozi unaathiri chama na unawasikitisha wanachama wengi.

Kwanini msitumie hii nafasi kusahau yaliyopita na kuanza upya kwa faida ya chama chenu, wanachama wenu na taifa kwa ujumla? Huku ndio kutakuwa kumuenzi mzee Mandela kwa vitendo.

Tanzania inahitaji vyama vya upinzani ambazo ni imara na vinaweza kuwa mbadala ya CCM. Uimara huo katu hauwezi kuwepo wakati mnagombana. Itakuwa ni kujidanganya kufikiria CHADEMA iliyogawanyika itaweza kuishinda CCM. Fungueni macho na muone ukweli.

Palipo na mtafaruku, mara zote, kunakuwa na makosa kutoka pande zote. Ifike mahali mkubali kukaa pamoja na kutafuta suluhu ya kwenda mbele. Kama Mandela akiwa rais, aliweza kumwalika dinner mwendesha mashitaki ambaye ndiye alimfunga jela na alitaka Mandela anyongwe. Sisi ni nani mpaka tushindwe kukaa pamoja kwa faida ya vyama vyetu na wananchi wetu?

Hii ni nafasi pekee, itumieni vizuri. Watanzania wanawaamini, msiwaangushe shauri ya ubinafsi na kushindwa kusameheana pale panapokuwa na matatizo.

Nafasi kama hii inatokea mara moja, ishikeni na kuhakikisha haipotei.
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Mkuu Mtanzania unataka viongozi wa CHADEMA waseme yaliyopita si ndwere na tugange yaliyopo kwa kufunika kombe mwanaharamu apite?. Are you serious?. Naona wewe huitakii mema CHADEMA.

Kwani haya matatizo ya viongozi ndani ya CHADEMA yameanza leo au kwenye mgogoro huu peke yake?.

CHADEMA deep down ina matatizo makubwa sana lakini ninashangaa sana wanajitahidi kutibu matokeo ya matatizo badala ya chanzo cha matatizo.

Hata kama wakiganga yaliyopo, tatizo litakuwepo na litaendelea kuitafuna CHADEMA mpaka pale watakapo tibu tatizo kuu na la msingi ndani ya chama.

Hata kama wakitibu matokeo ya Tatizo, kitu ambacho wako busy kutaka kukifanya ndani ya CHADEMA, tatizo kuu litaendelea kukitafuna chama na yataibuka matokeo ya tatizo mengine tena kwa siku za usoni.

Tatizo la vyama vichanga kama CHADEMA vinasumbuliwa na wanachama wanafiki wanaosukumwa na ubinafsi katika maamuzi. Viongozi wanachofanya ni kuutumia unafiki huo katika kutimiza malengo yao, kitu ambacho kinaleta migongano baina yao katika majukumu yao yanayosukumwa pia na ubinafsi.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom