CHADEMA leo wana nafasi ya kuweka historia ya kusimamia maadili ya chama kwa kuwafukuza Wanachama wake 19 kwa mpigo

Wakuu bila kuwachosha, nashauri kamati kuu ya CHADEMA ionyeshe sifa bora za kiongozi katika kutoa maamuzi sahihi kwa wabunge wa viti maalum, pasipo kutawaliwa na hisia, mitandao, msukumo wa watu wa nje n.k ,watawaliwe na kuongozwa na sifa za kiongozi bora katika kipindi kigumu. Nawasilisha

Ni hivi, leo kundi la wahuni wachache ni kupigwa chini ili wakashirikiane vizuri na shetani. Huu ushauri wako ungewapelekea CCM dhidi ya Membe.
 
Ni imani yangu viongozi wa CHADEMA leo wataweka mbele heshima ya chama kwa kulinda katiba ya chama hicho pale watapowafukuza wasaliti 19 kwa mpigo na kuweka historia ya kufukuza Wanachama Waandamizi 19 kwa mpigo ili kulinda Katiba ya chama.

Hakika leo itakuwa ni siku ya historia kwa CHADEMA na pigo kwa watu wa chama fulani na mamluki wao pamoja na taasisi zote zilizohusika katika hujuma hii iwapo CHADEMA watafanya maamuzi hayo ya kuwafukuza wasaliti hawa katika kikao chao cha leo tarehe 27/11/2020.

27/11/2020 itakuwa ni siku ya kukumbukwa. Kazi kwenu CHADEMA.
Mkuu umemsahau Aida Kenan naye alipaswa kufukuzwa au hakutumiwa wito , Leo ilitakiwa kumalizana na wasaliti wote kwa mpigo .
 
Mtafukuza wangapi?
Msitazame mnapoangukia, tazameni mnapojikwaa!

Msijione Vichwa kwa kufukuza wanaowasaliti, jiulizeni kwanini mnasalitiwa? Kwanini Viongozi wenu wanathamini vyeo na fursa kuliko Itikadi? Mtakabiliana vipi na usaliti...
Umeandika vizur lakini hilo la mnyika siyo kweli kwamba alikimbia kibamba. Hata slaa nlipokuwa KM alikoma kuwa mbunge wa karatasi. Tuseme alikimbia??
 
Huna Kumbukumbu
Dr Slaa alikuwa KM na Mbunge wa Karatu hadi 2010 alipoenda kugombea Urais ndipo alikoma kuwa Mbunge

Dr Kabourow alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema huku akiwa Mbunge wa Kigoma mjini

Umeandika vizur lakini hilo la mnyika siyo kweli kwamba alikimbia kibamba. Hata slaa nlipokuwa KM alikoma kuwa mbunge wa karatasi. Tuseme alikimbia??
 
Ni imani yangu viongozi wa CHADEMA leo wataweka mbele heshima ya chama kwa kulinda katiba ya chama hicho pale watapowafukuza wasaliti 19 kwa mpigo na kuweka historia ya kufukuza Wanachama Waandamizi 19 kwa mpigo ili kulinda Katiba ya chama...

Mkuu kwann unasema wabunge 19 wa viti maalum. Je aida hastaili kufukuzwa kwenye chama? Kama mnapinga matokeo kwann mlimruhusu Aida akaapishwa? Kwanini msingemvua uanachama na kumfukuza kabla kuapishwa?

Mkiwafukuza hao 19 mtakuwa mmewaonea na mtakuwa hamjawatendea haki wote 19.

Narudia tena kama mnapinga uchaguzi basi wafukuzeni wote adi Aida

Nipo hapa nasubiri kauli ya chair man
 
Mtafukuza wangapi?
Msitazame mnapoangukia, tazameni mnapojikwaa!

Msijione Vichwa kwa kufukuza wanaowasaliti, jiulizeni kwanini mnasalitiwa? Kwanini Viongozi wenu wanathamini vyeo na fursa kuliko Itikadi? Mtakabiliana vipi na usaliti

Hao kina Catherine Magige kama Halima angewaweka kwny orodha ya 'covid 19' wasingechomoa sema baada ya kutoswa lazima waigize uzalendo

Kuna Mtu aliaminiwa kuwa kaiva kiitikadi Chadema kama Dr Slaa, lakin kiko wapi leo?

Hata Halima Mdee alikuwa akiwacheka na kuwakebehi sana wanaosaliti kama Mashinji lakin leo kiko wapi?

Msishangae Mnyika akiahidiwa Ubunge wa kuteuliwa na Rais nae akabwaga manyanga maana Kibamba alikimbia baada ya kuona hana nafasi sio kuwa alitosheka na Ubunge

Hizo ni porojo zako tu wote wanafukuzwa na CDM it aendelee kupeta na wafuasi wa kutosha wapo tu hiki ni chama cha watu siyo mtu hao covid 19 wanafukuzwa bila hata shida yoyote. Wasaliti hata wawe wengi kiasi gani watafukuzwa tu ni bora kuwa na wafuasi wachache wasiokuwa na viashiria vya usaliti.
 
Then wewe unapata faida gani?
Watu wengine sijui uwa mnawaza kitu gani

Michango na mapambano ya Hao wadada kwa chadema unaijua?

Unajua mambo waliopitia Mpaka chama kimefika hapo?

Hata mkiwavua bado wanakuwa wabunge Sasa chama kinakuwa kimepata nn kama sio ujinga?

Wanakinomoa chama kwa kutumiwa na TISS hivi hapo kuna mchango gani mikakati yote wanapanga pamoja na TISS sijui mara TISS waandike barua kwenye mitandao ya kutoa shukrani sijui nini sasa kama wamechaguliwa na chama mbona wameitwa kwenye kikao cha chama hawakwenda ati simu nyenyenye mkiti mbona hawakwenda kumshukuru sasa. Uongo huwa hauwezi kudumu kama hivi umefikia mwisho hawana tena cha kusema wamejulikana kwamba hawakupendekezwa.
 
Mdee usaliti wake ni kupeleka majina ambayo hayana wanawake wa viongozi, hapo ndio amesaliti

Kwani Mdee ndo Katibu wa chama mbona Mahela alisema Katibu anatakiwa kupeleka majina hajapeleka hadi akamwandikia barua na kumpa form za kujaza sasa Mdee kuchaguliwa lini kuwa Katibu wa chama hao ni wabunge wa viti maaluma wa CHADEMA siyo wa bawacha kama anavofikiria Mdee
 
Wanakinomoa chama kwa kutumiwa na TISS hivi hapo kuna mchango gani mikakati yote wanapanga pamoja na TISS sijui mara TISS waandike barua kwenye mitandao ya kutoa shukrani sijui nini sasa kama wamechaguliwa na chama mbona wameitwa kwenye kikao cha chama hawakwenda ati simu nyenyenye mkiti mbona hawakwenda kumshukuru sasa. Uongo huwa hauwezi kudumu kama hivi umefikia mwisho hawana tena cha kusema wamejulikana kwamba hawakupendekezwa.
Kama ujui mambo kaa kimya
Kwaiyo na Ile list ya kwanza ambayo Mnyika amepeleka ni Tiss?
 
Mbona madiwani wameapa na hakuna kelele
Kwani Mdee ndo Katibu wa chama mbona Mahela alisema Katibu anatakiwa kupeleka majina hajapeleka hadi akamwandikia barua na kumpa form za kujaza sasa Mdee kuchaguliwa lini kuwa Katibu wa chama hao ni wabunge wa viti maaluma wa CHADEMA siyo wa bawacha kama anavofikiria Mdee
 
Wakati ule wanabadili gear angani hawakutizama nyie mtasemaje wala mtafanyaje pamoja na kwamba mlijiaminisha kuwa wasingeweza kuthubutu kufanya hivyo ila mwisho wa siku mkaamua tu kukubali mkapiga deki tukio likawa limepita hilo,na sasa nadhani watafanya maamuzi kwa kuangalia chama kinafaidika na hao wabunge 19 na sio kufanya maamuzi kwa kuhofia chama kitaonekanaje au nyie mtasemaje.

Chama hakihitaji kufaidika na hao wasaliti ni kiwafukuza tu hakuna njia nyingine tena wakifukuzwa watawachagua wanawake wengine kushika hizo nyadhifa na kuhamasisha wengine wengi kukikubali CHADEMA. Hakuna uamuzi mwengine ni kufukuza tu ndo linakuwa pita kwa wote walijiingiza kwa huo uchafuzi.
 
Do you think Hilo zoezi ni sawa na kwenda kufunga Ndoa tu?
 
Kina Halima wana mtihani mkubwa sana kuishi na jina la usaliti......na usaliti wao upo wazi kabisa, yaani unaenda kuhalalisha haramu wazi wazi.
 
CHADEMA kwa historia yake wakati wa matukio kama haya hawajawahi kuniangusha, naamini na leo wataendelea na msimamo wao wa kawaida.

Chama imara lazima kiwe na maamuzi imara siku zote.
hamna aliyefukuzwa adi saa hii
 
Back
Top Bottom