Chadema lazima waandae mpango mkakati usimamizi mchakato wa katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema lazima waandae mpango mkakati usimamizi mchakato wa katiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kweleakwelea, Nov 29, 2011.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  LEO HII TUMESOMA TAARIFA HII IFATAYO KUWA RAISI AMETIA SAINI SHERIA YA KATIBA, MASAA MACHACHE BAADA YA KUACHANA NA UJUMBE WA CHADEMA KAMA IFUATAVYO.......

  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.

  Hatua hiyo ya Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge.

  Aidha, kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka jana, 2010.

  Pamoja na kutiwa saini hiyo bado Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.

  Hivyo, Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yoyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  29 Novemba, 2011


  way foward:

  INAWEZEKANA MUDA ULIKUWA MDOGO, AU ILIKUWA NI MAPEMA KWA WAJUMBE WA CHADEMA KUWEZA KUTATHMINI USHIRIKISHWAJI WAO KATIKA FOLLOW UP YA MCHAKATO MZIMA.......

  LAKINI NI UKWELI KUWA YALE YALIYOJADILIWA NA PANDE MBILI YAANI SEREKALI NA CHADEMA YAMEONEKANA KATIKA UJUMBE HUU..................

  LA MSINGI SASA NI KUWA

  1. NI UKWELI KUWA MCHAKATO HUU BADO UNAWEZA KUWA NI MALI YA SEREKALI.......

  HIVYO

  1. CHADEMA WANAPASWA KUANDAA MPANGO MKAKATI - STRATEGIC PLAN WA KUHAKIKISHA KUWA WANAISIMAMIA SEREKALI KUFANYA YANAYOTAKIWA KAMA WALIVYOKUBALIANA....MPANGO MKAKATI HUWA UNAAINISHA WAZI WAZI KUWA NINI KITAFANYIKA LINI, NA NI NANI ATAKIFANYA, AKITUMIA RASILIMALI ZIPI, AMBAZO ZITATOKA WAPI...ILI KUFANIKISHA MALENGO YAPI...NA BAADA YA HAPO MAFANIKIO YATAPIMWA VIPI...KWAVIGEZO VIPI....NA NI LINI ZOEZI LINATAKIWA KUWA LIMEKAMILIKA!

  MPANGO HUU MKAKATI NI VYEMA UKARATIBIWA NA CHADEMA KWANI NDIO WAWAKILISHI WA WANANCHI WENGI WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI YAO MARA KWA MARA TUTAWATUMA CHADEMA KURUDI IKULU MAMBO YANAPOKUWA SIO MAMBO.

  cHADEMA WAO WASHIKE USUKANI NA MPANGO MKAKATI HUU UHUSISHE VYAMA VYA KITAALUMA NA ASASI MBALI MBALI ZINAZOHUSIKA NA MCHAKATO HUU - - - KAMPENI, UELIMISHAJI, NK NK

  PIA CHADEMA WASIMAMIE KWA KARIBU URATIBU WA ZOEZI ZIMA ILIKUEPUKA UKUSANYWAJI MAONI WA KISANII NA USIO WENYE UWAKILISHI...........

  DESIRED OUTPUT (MILESTONE) ZA STRATEGIC PLAN
  EG NI LINI KIWE TAYARI HII NI BORA ZIKAWAKILISHWA KWA RAISI ILI AWALI YA YOTE MAKUBALIANO YAFANYIKE KUHUSIANA NA TIMEFRAME...................KWA VYOYOTE SEREKALI NA TAASISI ZAKE ZINATAKIWA KUWA SEHEMU YA MPANGO MKAKATI WA KUANDAA KATIBA MPYA.........

  MAKUBALIANO HAYA YA KUSIMAMIA MCHAKATO WA KATIBA YAWASILISHWE KWA WANANCHI ILI IWE MKATABA KATI YA SEREKALI NA UMMA.....

  TUSIPOLIFANYA HILI BASI HIZI SIKU MBILI TULIZOENDA IKULU TUMEENDA KUCHEZA KIDUKU NA TUTAKOSA UMILIKI WA MCHAKATO, KITU AMBACHO NINAAMINI KABISA NDICHO TULICHOKIFUATA PALE IKULU!

  NAOMBA KUWASILISHA!

  MUNGU IBARIKI TANZANIA!
   
Loading...