Chadema lazima tuongelee na tujenge nidhamu ya chama sasa tukielekea kutwaa mamlaka ya nchi 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema lazima tuongelee na tujenge nidhamu ya chama sasa tukielekea kutwaa mamlaka ya nchi 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by George Maige Nhigula Jr., May 7, 2012.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu Zangu Wana Jamii,

  Ni takribani yapata wiki ya pili sasa Tangu Halimashauri kuu ya chama cha demokrasia na maendeleo ilipokaa na kupitisha maazimio mengi na moja wapo ambalo ni muhimu sana kwa chama ni uboreshaji wa Nidhamu ya chama wakati chama kikijiandaa kutwaa mamlaka ya kuongoza taifa letu kuelekea kwenye chaguzi mbalimbali za hapo usoni kama uchaguzi wa serikari za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Ndugu zangu napenda kuipongeza kwa dhati halmashauri kuu ya chama kwa kuibua na kulipa umuhimu mkubwa swala la nidhamu ndani ya chama. Hakika hatutaweza kufanikiwa bila ya kujenga nidhamu thabiti miongoni mwetu na kwa viongozi wetu.

  Ni dhahili kabisa chama kinachojiandaa kutwaa Dola na kuongoza taifa letu lazima kiwe na nidhamu ya hali ya juu ambayo inatoa taswira ya uongozi na serikari itakayo undwa na kuaminiwa na wananchi pindi kitakapopata ridhaa ya wananchi. Hivyo napenda kuunga mkono uongozi wetu kwa kutambua umuhimu wa nidhamu katika chama.

  Lakini napenda kutoa angalizo kuwa hili swala la nidhamu ni muhimu sana hivyo sijaona kama wanachama na viongozi mbali mbali wamelielewa na kulipokea vizuri na kulichukulia kwa uzito wake, na kulitilia mkazo hata kwenye makongamano, mikutano na vikao vyote mbalimbali vya chama. Nakubaliana kabisa na mwandishi Danny Rye, kutoka School of Politics and Sociology, Birkbeck College, University of London ambaye aliongelea kuhusu umuhimu wa masuala ya nidhamu kwenye chama cha siasa kinachojiandaa kutwaa dola na kitu kikubwa sisi wapenda mabadiliko tunashindwa kutambua NGUVU YA DOLA NI ZAIDI YA TASHWISHWI HASI, nanukuu maneno ya Danny Rye kama ifuatavyo

  "What is missed, however, is the extent to which power may be more than just a negative force of constraint. What if we saw
  Power as productive, positive, or constitutive for example? Would that not lead us towards some different conclusions as regards the location of power, the production of political identity and the role of the subject in it? What this requires is a repositioning.
  Examining parties from the vantage point of power, rather than vice versa will allow us to look differently at the question of discipline, how it is generated and sustained" mwisho wa kunukuu. 

  Sisi sote kwa pamoja tunaweza kujenga nidhamu kwa kujikita zaidi katika kujenga mawazo mapya na chanya ya kujenga nchi yetu upya by learning forward rather than dwelling on past failures, hata mwandishi Danny Re amenukuu maneno ya waandishi Jensen and Owen, Chama kinapokuwa na mtazamo mmoja, dira moja na kujumuika pamoja inajenga msukumu mkubwa ambao ni muhimu sana kwa ujenzi wa nidhamu imara. hivyo basi sina uhakika kama wapenda mabadiliko wote tuna mtazamo mmoja(shared value),tunajumuika pamoja (socialization) na tuna lengo moja sahihi ( shared vision). hivi vitu vyote vyaweza kutusaidia kujenga nidhamu iliyo imara.

Ni dhahiri kabisa nidhamu inaweza kuenekana kutokana na tabia za wanachama na viongozi na nidhamu inaweza kuboreshwa zaidi kama tutazingatia yafuatayo


  1) Overt behavior
(Tusijenge chama kwa mtindo wa mashabiki)
  2) Covert behavior

  3) Structural power

  4) Routinized Power

  5) Micro power (hapa ndipo chama kinabidi kipate political identity kutokana na mwenendo na tabia za wanachama)  Nikipata nafasi nitaendelea kuongelea kwa undani zaidi hizo behavior tano hapo juu na umuhimu wa Nidhamu kwa chama kinachojiandaa kutwaa dola.
Nashukuru naomba tusaidiane kujenga nidhamu ili tuweze kuaminiwa na watanzania wengi zaidi kama sio wote.

   
 2. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watanzania watakuelewa baada ya kujeruhiwa na "nidhamu ya chama" ya CCM? Hilo somo hebu lirudie tena ili sisi wegine tuliokosa imani na nidhamu za vyama tukuelewe.
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mkuu tunashukuru sana kwa uchambuzi mzuri big up hofu na shaka ni hii kampeni ya vua gamba vaa gwanda inaweza kukusanya makokoro yasiyokuwa na dispine.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  imekaa vyema sana...
   
 5. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Well said and analyzed.... Wenye masikio na wasikie!
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Hiki sio kipindi cha nidhamu hasa ktk hiki kipindi cha harakati, Hiyo nidhamu unayoingolea mleta thread bado sijakusoma kuwa ni nidhamu ipi hiyo? Hizi si zama za nidhamu hasa kwa serkali kandamizi kama hii, Nidhamu ambayo labda ningekuelewa ni ya uadilifu 2 na kuheshimu viongozi wa chama lakini kama unamaanisha nidhamu kwa serkali hii ya CCM hilo halitawezekana kwani sometimes sisi kama CDM tunatakiwa tuwe disobidient & undispline kwa sheria kandamizi za ccm ili tuweze kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hii serkali kiziwi, Pia unatakiwa ujue kuwa neno Nidhamu limekuwa ni tunguri la kutukandamiza na kutuziba mdomo watz hata pale tunapoona tunaonewa.

  Shardcole@Tabora1
   
 7. A

  AUDACITY OF HOPE New Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shardcole,

  Statement aliyotoa Dogo Janja pale NMC, it was inappropriate, it was a divisive statement tena mbele ya mwenyekiti wake wa Taifa, Statement kama hizo zinawatisha baadhi ya watanzania wenzetu ambao wamechoshwa na ccm na wanahamu kubwa ya ku support Chadema.

  Hivyo ndo maana Mh. Mbowe alirekebisha pale pale Jukwaani ili kutoa assurance kwa moderate people, Kama chadema kinajiandaa kuchukua dola ni muhimu sana kuzingatia nidhamu, we need everybody kwenye safari ya ukombozi.

  Na the way forward inabidi kwenye political rally wazungumzaji wote lazima wawe wanatoa speech zao kwa maandishi kabla ya kuongea na mwenyekiti anazipitia kabla, na kama kuna lugha isiyo ya kupendeza basi inaondolewa kabla ya mtu hajaongea. Lazima tuepukane na vitu vitakavyowapa ccm talking point hivyo nidhamu ya chama lazima iwe ya hali ya juu.
   
 8. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nidhamu ya Nasari kutangaza jamuhuri ya Meru
   
Loading...