CHADEMA kwenda Mahakamani kupinga matokeo ya Udiwani katika Kata ya Turwa, Mara

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Aliyekuwa Mgombea Udiwani Kata ya Turwa kupitia chama cha Demokorasia na Maendeleo (CHADEMA) Charles Mnanka amesema ataenda mahakamani kupinga matokeo ua uchaguzi yaliyompa ushindi aliyetangazwa mshindi kupitia Chama Cha Mapinduzi Chacha Ghati.

Mnanka amewambia Waandishi wa Habari kuwa ataenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi, Chacha Ghati maarufu Chacha Kamanda wa Chama Cha Mapunduzi ambaye aligombea udiwani Kata ya Turwa na kutanagazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Peter Julius.

"Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Mdogo wa Kata ya Turwa, Peter Julius ambaye ni Mtendaji wa Kate ya Turwa ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime katika Mkoa wa Mara alitangaza matokeo kwa kupendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa hali hiyo tutapinga matokeo hayo mahakamani," alisema Mnanka.

Pia Mnanka aliongeza kuwa Chama chake kinalalamikia Msimamizi Msaidizi wa Mchaguzi kwa kumtangaza mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi kuwa ndiye aliyeshinda nafasi ya udiwani Kata ya Turwa hadi baadhi ya matokeo ya vituo Tisa kati ya 13 Chadema inaongoza huku Chama cha mapinduzi kikiwa kinaongoza vituo Vinne tu.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Demkorasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Chacha Heche alisema kuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi alikiuka tamko la Tume ya Uchaguzi hususani Fomu Namba 21c na Namba 24c ambapo Chama cha Chadema hakikukabidhiwa fomu hizo na matokeo yake.

Heche aliongeza kuwa wamefikia hatua ya kujadiliana kwenda mahakamani kupinga matokeo ya ushindi wa Chama cha mapinduzi ndani ya kata ya Turwa baada ya kuona kuwa baadhi ya taratibu zilikiukwa katika kituo kata cha kupiga kura cha Turwa (B) ambacho wanalalamikia kuwa matokeo yake yaliyotangazwa na msimamizi msaidizi sio sahihi kwani Chama Cha Mapindizi walipewa kura 400 katika kituo hiki huku CHADEMA wakiandikiwa kuwa wamepata kura 100 katika kituo hiki jambo ambalo sikweli, aliongeza kusema.

Katibu huyo pia alisema kuwa Chama chake kitaenda Mahakamani kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea udiwani wa Chama cha mapinduzi kwasababu wanamatokeo ya vituo vyote na kwa matokeo hayo Chadema inaonyesha imeshinda vituo vingi kuliko CCM.

Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Turwa Peter Julius jana alimtangaza Mshindi nafasi ya udiwani Kata ya Turwa Mgombea wa CCM, Chacha Ghati ambaye alipata kura 1401 huku mshindani wake wa Chama cha (CHADEMA), Charles Mnanka akiambulia kura 1121 na Mgombea wa Chama cha NCCR Mageuzi akiambulia kura 17 tu.
 
Tumeshaenda sana mahakamani lakini hamna jipya tukumbuke sikuzote ukienda mahakamani kuwashtaki ccm basi itakula kwako.........bunge,mahakama,dola na katiba ni mali ya ccm huwezi kupata haki juu yao.

Njia muhimu ni kususia uchaguzi zote au tupiganie vyama vingi vifutwe ili wabakie wachawi(ccm)
 
Kesho utasema hata Kanisani na Msikini hamuendi tena kwa maana Mungu pia kashikwa na CCM, ukisikia kukata tamaa ya maisha ndo huku!
 
Tumeshaenda sana mahakamani lakini hamna jipya tukumbuke sikuzote ukienda mahakamani kuwashtaki ccm basi itakula kwako.........bunge,mahakama,dola na katiba ni mali ya ccm huwezi kupata haki juu yao.

Njia muhimu ni kususia uchaguzi zote au tupiganie vyama vingi vifutwe ili wabakie wachawi(ccm)
Huu sasa ni uchuro sio manung'uniko tena ndugu zangu Chagadema.
 
Back
Top Bottom