CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Alikuwa mwanachama mwanadamizi NCCR hadi mwaka 2000 akahamia TLP.nasema kwa hili ataumbuka sana bora anyamaze.Mheshimiwa Mwanakijiji vyama vina rekodi za wanachama wao.inapotokea Mtu anaficha sehemu ya CV yake lazima tumuogope kwani si mkweli.
kwa hili Mwanakijiji ukicheki na Lyatonga Mrema atakupa,najua kutofautisha kuwa kocha wa timu ya Taifa ni mbrazil hamfanyi awe mtanzania ,Kuku kuzaliwa kwenye ziziz la ng'ombe hamfanyi kuwa ng'ombe. Mbowe alihudhuria sherehe za rais JK kuapishwa sio CCM.
Kitila Tumekuwa nae Daruso alikuwa rais wetu tunamjua vizuri sana.

Mkuu weka ushahidi kukata mzizi wa fitina. Maneno tu watu watakubishia sana hapa.
 
Hukugombea Uenyekiti wa mkoa wa Dsm? na ukaukosa?

swali la nyongeza at any time hukuwa mfuasi wa Mrema alipokuwa NCCR na ukahama nae kwenda TLP?

Nina ushahidi mkubwa sana wa jambo hili na unajua unasema uongo,kwani kuna kosa gani wewe kuwa NCCR? KITILA wewe ni public figure maisha yako huwezi kuyaficha hasa hapa JF kila siku watu wanaumbuka.

Sijakataa kuwa niligombea uenyekiti wa UVCCM. Lakini sio kweli kwamba nilishindwa. Kilichotokea ni kwamba jina langu halikupitishwa kwenye vikao vya wahafidhina kwa madai kwamba nilikuwa na damu ya upinzani. Ambacho niligombea na nikashindwa ni ujumbe wa baraza kuu la UVCCM na nilishindwa na Chicago, matelefoni wa Temeke. Sasa kwa nini unazusha mambo hapa, inakusaidia nini? Utafanya watu wasikuamini kwa chochote unachosema kwenye forum hii.

Narudia tena sijawahi kuwa mwanachama wa NCCR wala TLP. Of course kuna viongozi wa NCCR na TLP niliokuwa na ambao hata sasa nawakubali akiwemo Mrema lakini haina maana kwamba nilikuwa mwanachama wa vyama vyao. Nilihama CCM mwaka 2005 na moja kwa moja nikajiunga na CHADEMA. Sasa ni lini nilikuwa mwanachama wa NCCR na TLP?

Kijana acha uzushi. Wewe huwezi kujidai unanijua kuliko ninavyojijua mwenyewe. Kwa taarifa yako mimi sio mtu wa kuficha habari zangu, nzuri na mbaya. Ningekuwa mwanachama wa hivyo vyama wala nisingebishana na wewe kwa sababu hakuna ubaya wowote kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Kama nimeweza kukiri kwamba nilikuwa mwanachama wa CCM, chama cha kifasadi na cha aibu kabisa, kwa nini nikwepe kukiri kwamba nilikuwa mwanachama wa NCCR au TLP kama ingekuwa ni kweli?
 
Mkuu weka ushahidi kukata mzizi wa fitina. Maneno tu watu watakubishia sana hapa.

Ni wewe uliyenihusia kuwa JF ina sheria zake, nimekupa hadi mwaka aliokwenda TLP unataka nini zaidi, nimekwambia alikuwa rais wetu Daruso mtu anapokuwa rais wako lazima umjue na umfutilie baada ya kumaliza chuo,jamaa ali SACRIFICE sana Udsm kwa hili tunampa tano zake.
Tatizo lake anapenda kuwa wenye vyama vinapokuwa juu akiona ovyo anahama.
Naomba niishie hapa labda akija bwana Kitila akitaka maelekezo zaidi nitarudi kumpa kumbukumbu.
 
Ndio haya nayapigania hapa.uwajibikaji na uwazi kwa vyama vyetu,haiwezekani mtu aliyechaguliwa na wanachama kwenye mkutano leo aitwe Mzigo mzito na Kitila Mkumbo.

Fikiria, ndio washachukua innji. Kisha wanaanza kutimuana ktk baraza la mawaziri!! ikulu hapatoshi!!!!!. Duh!!!!!!
 
Ni wewe uliyenihusia kuwa JF ina sheria zake, nimekupa hadi mwaka aliokwenda TLP unataka nini zaidi, nimekwambia alikuwa rais wetu Daruso mtu anapokuwa rais wako lazima umjue na umfutilie baada ya kumaliza chuo,jamaa ali SACRIFICE sana Udsm kwa hili tunampa tano zake.
Tatizo lake anapenda kuwa wenye vyama vinapokuwa juu akiona ovyo anahama.
Naomba niishie hapa labda akija bwana Kitila akitaka maelekezo zaidi nitarudi kumpa kumbukumbu.

mgagagigikoko kwa vile Kitila amekupa ruhusa kuweka ushahidi kuwa alikuwa mwanachama wa NCCR na TLP na kwa vile umesema kuwa kuku kuwa zizini hakumfanyi awe ng'ombe bila ya shaka una ushahidi mkubwa zaidi. Hivyo, naamini ushahidi pekee na ambao haupingiki ambao unaweza kusimama katika mahakama ya watu hapa ni ushahidi wa kadi.

Kwa vile umesema kuwa vyama vina rekodi, na kwa vile unajua mwaka ambao Kitila alijiunga na hivyo vyama vingine, nadhani itakuwa vizuri kutuonesha kuwa Bw. Kitila si msema kweli kwa kuweka hadharani namba ya kadi yake ambayo sisi wengine tunaweza kufuatilia NCCR na TLP ili kujua kama ilitolewa kwa mtu aitwaye Kitila Mkumbo.

Ni ushahidi huo tu utakaokubalika kuonesha kuwa Bw. Mkumbo aliwahi kuwa mwanachama wa vyama hivyo vingine na hivyo kuyatupilia mbali maneno yake kuwa alipohama CCM aliingia Chadema.

Ukiniuliza mimi the burden of proof is on you.
 
Fikiria, ndio washachukua innji. Kisha wanaanza kutimuana ktk baraza la mawaziri!! ikulu hapatoshi!!!!!. Duh!!!!!!

hawa hawawezi kuchukua nchi.... sisi ccm hatuna cha kutimuana wala nini.
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.

kidumu chama cha mapinduzi.
 
Ni wewe uliyenihusia kuwa JF ina sheria zake, nimekupa hadi mwaka aliokwenda TLP unataka nini zaidi, nimekwambia alikuwa rais wetu Daruso mtu anapokuwa rais wako lazima umjue na umfutilie baada ya kumaliza chuo,jamaa ali SACRIFICE sana Udsm kwa hili tunampa tano zake.
Tatizo lake anapenda kuwa wenye vyama vinapokuwa juu akiona ovyo anahama.
Naomba niishie hapa labda akija bwana Kitila akitaka maelekezo zaidi nitarudi kumpa kumbukumbu.

Nataka ule ushahidi uliosema kuwa utanipatia kwenye email uuweke hapa. Si unaona bado Kitila anakataa kuwa hajawahi kuwa NCCR, wala TLP?
 
hawa hawawezi kuchukua nchi.... sisi ccm hatuna cha kutimuana wala nini.
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.

kidumu chama cha mapinduzi.
wewe Masaka maji yakimwagika hayazoleki!
 
Kitila.

Wanaounda kamati kuu wamechaguliwa na Mbowe hili halina ubishi, ni Mbowe aliyewapa nafasi hizo Baregu na Ngaiza na wengine, ni sawa na kusema waziri Pinda,Ngereja na waziri Membe ambao wamepewa ulaji na JK waitwe na kuambiwa watoe maamuzi ya yaliyo na maslahi na JK au maslahi ya JK yanahatarishwa na mtu let say Sumaye, unafikiri jibu litakuwaje?

Chacha Wangwe.

Ni mbunge pekee katika Chadema aliyeshinda kwa ushindi mkubwa kwenye ubunge kwa wastani wa asilimia 65 hadi 70 hakuna mbunge yeyote wa upinzani Tanzania Bara aliyepata kura hizo, huko kote kapita kwa kishindo na kama angeenda kwenye Uenyekiti angechukua, kusema kuwa hana interpersonal skills ni kumkandamiza kwa vile wewe Kitila, Mnyika, Tundu Lissu, Zitto mko upande wa Mbowe ambao unaitwa upande wa wasomi, ndio maana mzee Halimoja amekuwa akitukanwa na upande huu kwa kujaribu kuwa na mawazo halisi, haiwezekani Wangwe akawa mzigo na mjinga wakati ameshinda kwa kishindo kikubwa jimboni kwake.

Kama mliuvumilia mzigo wake kwanini msisubiri hadi mwezi wa nane yaani mwezi mmoja tu wakati wa uchaguzi wa mkuu wa chama? kwa akili zangu ndogo inaonekana miezi saba aliyokaa madarakani kama makamu amejijenga kiasi mnaogopa kuwa akiingia kwenye mkutano mkuu kama makamu anaweza kuchukua uenyekiti.

Chadema kwa hili mmedhihirisha kuwa sio chama bali ni platform ambayo watu wanaitumia kufikia malengo yao,
kama vikao vya faragha wakufukuzwa ni Zitto Kabwe ambaye wote mnajua kuwa ana ukaribu mkubwa na JK kuliko Mbowe.

Wangwe amepunguzwa kasi au amefungwa spidi gavana na wenye chama chao.
Nataka kujua jamani kwani haruhusiwi kugombea huo uenyekiti kama tatizo ndio hilo?maana hapa tutajua nani mwenye tatizo kati yake na mbowe.
 
Ntaka kujua jamani kwani harsiwi kugombea huo uenyekeiti kama tatizo ndio hilo?man hapa tutajua nani mwenye tatizo kati yake na mbowe.

Nyote mmesema na kuandika saaaaaaaaaaana, lakini naona wote wanaomtetea Wangwe hawamjui, na vigezo wanavyotoa kuhusu uwezo wake ni vya kitoto. Mnamjua Wangwe halisi au Wangwe mnayemsoma magazetini? Chadema kingekuwa chama cha ajabu kumuacha Wangwe aendelee kuvuruga hata achievments kidogo zilizokwisha patikana, eti kwa kuogopa kukosolewa na watu kama inavyofanyika hapa.

Naelewa wale wa CCM mnaokerwa na jitihada za Chadema mmehuzunika kwani nia yenu chama kisambaratike mpate kufisadi nchi yetu. Mnakinyemelea kama fisi na mkono wa binadamu, na sasa mnachekacheka mkidhani mkono unadondoka. Wapi, hapati mtu kitu hapa!

Mna haki ya kumwonea Wangwe huruma lakini sio katika hili la kutaka kuvuruga chama. Walichofanya Chadema ni sawa, kumdhibiti kabla hajaleta madhara zaidi. Kama wametazama athari yake kwenye uchaguzi ni sawa tu, aingie huko akiwa mbunge kuliko akiwa kiongozi anayehujumua jitihada za viongozi wenzake.

Haiwezekani kwamba katika orodha ya viongozi wote wa Chadema yeye tu ndiye yuko sahihi, asikilizwe, asiguswe. Uongozi ni pamoja na kuchukua hatua. Kwa hili, uongozi wa chadema unastahili heshima na pongezi, siyo lawama.
 
hawa hawawezi kuchukua nchi.... sisi ccm hatuna cha kutimuana wala nini.
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.

kidumu chama cha mapinduzi.
Kumtimua mtu akishindwa kutekeleza majukumu aliyokabhiwa au aliyetumia vibaya madaraka aliyopewa ni jambo la kujivunia na ni lazima liwe linatendeka ili kujenga nidhamu. CCM inalinda hata watu wa aina hiyo hapo juu, na hilo ni tatizo kubwa sana kwa wananchi.

Tunachosema hapa ni kile kitendo cha kiongozi mmoja kuweka mbinu za kumtimua kiongozi mwenzie kwa sababu binafsi.
 
mgagagigikoko kwa vile Kitila amekupa ruhusa kuweka ushahidi kuwa alikuwa mwanachama wa NCCR na TLP na kwa vile umesema kuwa kuku kuwa zizini hakumfanyi awe ng'ombe bila ya shaka una ushahidi mkubwa zaidi. Hivyo, naamini ushahidi pekee na ambao haupingiki ambao unaweza kusimama katika mahakama ya watu hapa ni ushahidi wa kadi.

Kwa vile umesema kuwa vyama vina rekodi, na kwa vile unajua mwaka ambao Kitila alijiunga na hivyo vyama vingine, nadhani itakuwa vizuri kutuonesha kuwa Bw. Kitila si msema kweli kwa kuweka hadharani namba ya kadi yake ambayo sisi wengine tunaweza kufuatilia NCCR na TLP ili kujua kama ilitolewa kwa mtu aitwaye Kitila Mkumbo.

Ni ushahidi huo tu utakaokubalika kuonesha kuwa Bw. Mkumbo aliwahi kuwa 'mwanachama wa vyama hivyo vingine na hivyo kuyatupilia mbali maneno yake kuwa alipohama CCM aliingia Chadema.

Ukiniuliza mimi the burden of proof is on you.

Nilisema kuwa jamaa alishindwa kupata uenyekiti UVCCM mkoa wa Dar-es-salaam sikusema Dodoma,amekuja kukanusha na kukubali kwa pamoja kuwa 'niligombea sikushindwa kwa vile jina lilikatwa sababu nilionekana mpinzani',sababu hiyo hakupewa na CCM ameitunga, walikatwa kina Malecela,Malima na Lowassa kwenye michakato ya namna hiyo hawakuambiwa wana chembe za upinzani.
Kitila hakuomba 2005 uenyekiti ilikuwa nyuma baada ya kuukosa uenyekiti wa mkoa wa Dar-es-salaam, akaenda NCCR na TLP, wewe ni mwandishi wa habari za utafiti ukipewa dondoo basi unachimba deep, kukusaidia wapi uanzie muulize Zitto Kabwe.

Jk ni mwenyekiti wa CCM sote tunamiini hivyo kama Ilivyo kwa Mbowe na Mbatia ni wenyeviti wa Taifa lakini sidhani kama wewe au mimi tunajua kadi namba zao kuthibitisha hilo.
John Komba ni mwanaccm au John Mnyika lakini mimi na wewe hatujui namba zao ila kuna ushahidi mwingi wa kimazingira kuthibitisha hoja hii.
vyama vyote vina regista ya wanachama wake ukienda huko utapata hadi kadi namba ya Kitila Mkumbo, alikuwa rais wetu wa UDSM kwa kauli hii ujue kuwa alikuwa mtu maarufu na anachofanya tulikifuatilia kwa makini.

Siasa inahitaji uvumilivu chama anachosema Tishio hivi(Chadema) ni nguvu na jasho la watu la miaka zaidi ya 14 hadi wamefika kwenye peak, kama kina Mtei au Mbowe wangekuwa nao wanabadilisha vyama kila mara leo tusingekuwa tunajadili Chadema wamefanya nini, 1995 Chadema walikuwa hawana mgombea wa urais na 2000 ilikuwa hakuna mtu na 2005 ilibidi Mbowe ajitose kufungua milango.

Ushauri kwa wanaoingia kwenye siasa kuwa kunahitaji uvumilivu na subira tusikimbilie kula bila kulima historia ipo na tutaitumia kuweka rekodi sawa pale zipopindishwa.
 
...at any time hukuwa mfuasi wa Mrema alipokuwa NCCR na ukahama nae kwenda TLP?

.

Kitila ameshasema ukweli wake hapa.....kwa nini tunamng'ang'aniza uwongo?

Kama issue ni kuwa mfuasi wa Mrema, hiyo haiwezi kuwa hoja. hata hivyo, ameikubali, lakini hajasema alikuwa mwanachama NCCR-Mageuzi.

Watanzania wengi wenye akili nzuri waliokuwa watu wazima enzi za Mrema walimuunga mkono, siyo kwa sababu ya uzuri wake hasa, lakini sana sana kwa sbabu walichoshwa na ufisadi wa CCM na Mrema ndiye alionekana mtu jasiri aliyeweza kuthubutu kuwatikisa CCM.

Tusisahau pia kwamba enzi za kuvuma kwa Mrema ndizo zilikuwa za wananchi kwa mara ya kwanza tangu 1965 kujisikia huru kuwapinga watawala. Kama wewe hukuwa upande wa Mrema enzi hizo, sitashangaa kukusikia leo bado uko nyuma ya mafisadi.
 
Duh!
Mgagagigikoko mkuu wewe moto, tena wa kukalia mbali yaani duh..... Haya yangu macho!
 
Tatizo letu watanzania mimi nionavyo tunafikiri matatizo ya Tanzania yanasababishwa na chama hapo ndipo tunabugi step zote.

Kama nilivyowahi sema huko matatizo ya tz ni Tatizo la kitaifa wala si ya kichama.
Mapigano tunayopigana kutoa chama fulani eti tukifikiri ndio maendeleo yatapatikana ndio tunazidi jichimbia kaburini.Mapigano ya kweli yangeanza na kubadili fikira,mtazamo na maono ktk jamii ya watz ,hayo ndio mapigano ya kweli.

Kutoa chama fulani ni hatari kubwa kwa mazingira yale sana sana kinachokua kimefanyika ni kutoa fisi ama mbwa mwitu mzee aliyeshiba tayari na kuingiza fisi kijana mwenye njaa kali.

Alichokisema Mtanzania ndio msingi wenyewe wa HAKI na UPENDO na Mtanzamo makini ulio na masilahi ya wawakilishwa yani mtu hawezi kupewa kazi na mtu mwingine na akakatimuliwa na mtu mwingine yani CHADEMA ni chama ambacho kinawakirisha kamati kuu na si wapiga balot yani kwanamna nyingine kimewadhalau na kuwadhalilisha wote waliopiga hilo balot na kuona wangwe awawakilishe.
 
Masaa machache baada ya Kamati Kuu ya Chadema kufanya uamuzi wa kumsimamisha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Chacha Wangwe (Tarime) KLHN ilipata fursa ya kuzungumza kwa kirefu na wahusika wote wakuu.

Mahojiano yangu na Bw. Tundu Lissu (Mkurugenzi wa Katiba na Sheria wa Chadema na Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania) yalielezea kwa kirefu ni kwanini Chadema walifikia uamuzi huo na nini kilichojiri. Mara baada ya kuzungumza na Lissu nilipata pia nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Bw. Chacha Wangwe kuhusu kufungiwa kwake na zaidi ya yote kuhusu madai yaliyoainishwa dhidi yake kwenye Tamko la Kamati Kuu hiyo.

Mahojiano hayo ambayo yamechukua karibu saa nzima yatarushwa kwenye KLH News exclusive kesho ili kila mtu aweze kufanya uamuzi wake yeye mwenyewe baada ya kuwasikia.

We bring the news, from the news makers!
 
Back
Top Bottom