CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
wakuu wangwe ameukwaa umakamo wa chadema.

anasema matumizi ya helikopta hayana faida na mkuu wa nyumba mbowe asema itatumika mambo hayo wakuu.

nn next?
 
wakuu wangwe ameukwaa umakamo wa chadema.

anasema matumizi ya helikopta hayana faida na mkuu wa nyumba mbowe asema itatumika mambo hayo wakuu.

nn next?

CHADEMA: Hatuna mgogoro

na Tamali Vullu

MBUNGE wa Tarime, Chacha Wangwe (CHADEMA) jana aliyameza maneno yake mbele ya waandishi wa habari na kukana taarifa zilizomhusisha yeye akikirushia tuhuma kadhaa chama chake.

Katika siku za hivi karibuni, kuelekea uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, mbunge huyo, ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo, alinukuliwa akikituhumu chama hicho kwa ukabila na matumizi mabaya ya ruzuku.

Chacha, ambaye alifanikiwa kuinyakua nafasi hiyo, jana alikana kuhusika na baadhi ya taarifa za vyombo vya habari na kueleza kuwa hakuna mgogoro katika chama hicho kama inavyodaiwa.

Wakati Wangwe akifanya hivyo, Baraza Kuu la chama hicho, nalo lilijibu tuhuma hizo na kueleza kuwa chama hicho hakina mgogoro na ruzuku ya sh milioni 60 inayopata kila mwezi haiwezi kukigawa, kwani chama kinaweza kuendeshwa bila ruzuku.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu tuhuma mbalimbali dhidi ya chama hicho zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari.

“CHADEMA ni chama kimoja, hakijagawanyika na hatuna mgogoro wa aina yoyote. Kuna baadhi ya vyombo vya habari vilivyo karibu na CCM vinatumika kuandika mambo yasiyokuwepo.

“Kamwe chama hakiwezi kugombanishwa na ruzuku ya serikali, kwani kimefuzu bila ruzuku. Ruzuku inachangia asilimia ndogo sana katika chama… hata ruzuku ikifutwa, CHADEMA tutakwenda mbele,” alisema Mbowe.

Alisema sehemu kubwa ya fedha zinazotumika kukiendesha chama hicho zinatokana na michango ya baadhi ya viongozi na kwamba matumizi ya fedha ya chama yanawekwa wazi kwa kiongozi yeyote anayehitaji.

Akizungumzia tuhuma za kushamiri kwa ukabila ndani ya chama hicho, pamoja na kukanusha, Mbowe alisema kuwa chama chenye ukabila ni CCM, ambacho kina mawaziri wengi wanaotoka Mkoa wa Kilimanjaro, wakati Mkoa wa Kigoma hauna mwakilishi ambaye ni waziri.

“Mkoa wa Kilimanjaro una mawaziri wanane huku ukiwa na wakazi wapatao milioni 1.2, lakini Mkoa wa Kigoma ambao una wakazi karibu milioni 1.7 hauna waziri hata mmoja… mtu hupaswi kuzungumza kama huna takwimu,” alisema.

Hata hivyo, Daniel Nsanzugwanko, ambaye ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, ni Mbunge wa CCM kutoka Mkoa wa Kigoma. Pia, Christopher Chiza ambaye ni naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika naye anatokea Mkoa wa Kigoma.

Lakini, akitetea hoja yake, Mbowe alisema kuwa ingawa wabunge hao kutoka Mkoa wa Kigoma ni manaibu mawaziri, hawaingii katika vikao vya Baraza la Mawaziri, ambamo hujadiliwa masuala yenye kupanga mustakabali wa taifa na kuwa kazi yao kubwa ni kujibu maswali bungeni.

Wangwe alisema hoja nyingi zinazotolewa katika baadhi ya vyombo vya habari si sahihi na wakati mwinigine huwa hazijasemwa kama zinavyoripotiwa.

“Ndani ya chama lazima tuzungumze ili tulete changamoto kwa Watanzania kwa lengo la kujenga chama, lakini baadhi ya vyombo vya habari wanatoa hoja hizo ‘out of contents’ (nje ya mada) au wakati mwingine hazijazungumzwa kabisa,” alisema Wangwe ambaye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Bara, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Amani Walid Kabourou aliyehamia CCM.

Alisema kwamba dhana kwamba chama hicho kina mgogoro inapandikizwa na CCM kwa lengo la kutaka kuwasambaratisha.

“Ndani ya chama hatuna mgogoro, ila tuna mdahalo na tumejenga utamaduni wa kuzungumza, na mikakati yetu tunaiweka wazi, lakini baadhi ya vyombo vya habari wanaigeuza ili kuonekana kuna mgogoro,” alisema.

Alisema kama Makamu Mwenyekiti, atakuwa na ushirikiano na viongozi wengine kwa lengo la chama kushika madaraka, ili kutoa mfano kwa vyama vingine ambavyo vinafanya mambo yake kwa siri.

Akitoa taarifa ya Baraza Kuu la chama hicho lililokutana juzi, Mbowe alisema pamoja na mambo mengine, baraza limepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya Katibu Mkuu.

Alisema Baraza Kuu limepokea na kutathmini ziara zilizowahi kufanywa kwa kutumia helikopta katika mikutano ya kuwashukuru wananchi, kuhamasisha uwajibikaji wa serikali na kujenga chama na kubaini manufaa yaliyopatikana kutokana na ziara hiyo kwa CHADEMA na kwa taifa.

“Baraza Kuu limetafakari gharama za ziara za helikopta na kuwianisha na ziara nyingine na kuazimia kwa kauli moja kuendelea na kutumia helikopta katika awamu nyingine ya ziara za CHADEMA kama ambavyo iliazimiwa pia na Mkutano Mkuu wa CHADEMA mwaka 2006,” alisema.

Alisema baraza hilo limeridhia matumizi ya helikopta, kwani si anasa na yana tija kwa Watanzania na ufanisi katika kuendeleza chama.

Mbowe alisema Baraza Kuu pia lilipokea, kujadili na kupitisha mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2008 na kusema mpango kazi huo utahusisha shughuli ambazo zitafanywa pia na kurugenzi mbalimbali za chama katika masuala ya utawala, uenezi, habari, sheria, bunge, halmashauri, vijana, wanawake, wazee, rasilimali, oganizesheni, mafunzo na mahusiano ya kimataifa.

Aidha, baraza limeridhia umoja wa madiwani wa CHADEMA unaojumuisha madhumuni, uanachama, muundo na masuala mengine muhimu yanayohusu taratibu za umoja wa madiwani.

“Umoja huu ambao wanachama wake ni kila diwani wa CHADEMA, utawaunganisha madiwani wa CHADEMA vizuri zaidi katika kutekeleza wajibu wao katika maeneo wanayowakilisha na kwa chama kwa ujumla,” alisema.

Sambamba na hayo, pia baraza limeazimia chama kiendelee na ushirikiano wa vyama vya upinzani vya CUF, TLP na NCCR-Mageuzi kwa lengo la kudumisha demokrasia nchini, kuunganisha nguvu katika kutetea maendeleo na hatimaye upinzani kuweza kuchukua dola.

Pia baraza hilo limetoa ratiba ya uchaguzi mkuu wa CHADEMA utakaofanyika mwakani kuanzia ngazi ya vitongoji hadi taifa.

“Mwezi Januari mwakani utakuwa wa maandalizi. Februari na Machi kutafanyika uchaguzi wa vitongoji, Mei na Juni uchaguzi wa matawi na Oktoba mosi hadi 20 uchaguzi ngazi ya majimbo.

“Novemba 20 hadi 30 utakuwa uchaguzi ngazi ya wilaya na Desemba 5 hadi 10 uchaguzi ngazi ya mikoa,” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema kuwa Kamati Kuu itakutana Desemba 12 mwakani, Baraza Kuu, siku inayofuata na Mkutano Mkuu utafanyika Desemba 14 mwakani.
 
Alisema kuwa Kamati Kuu itakutana Desemba 12 mwakani, Baraza Kuu, siku inayofuata na Mkutano Mkuu utafanyika Desemba 14 mwakani.

Na hii ndiyo itakuwa siku ya uchaguzi kwa mwenyekiti taifa? au hawa wenyeviti wa vyama vya upinzani ni wa maisha?
 
wakuu wangwe ameukwaa umakamo wa chadema.

anasema matumizi ya helikopta hayana faida na mkuu wa nyumba mbowe asema itatumika mambo hayo wakuu.

nn next?

Huyu naona ni pandikizi la CCM na amewekwa ili kukivuruga CHADEMA. Wasipokuwa makini kweli atawavuruga. Akiendelea kuongea upupu wake ambao hauna maslahi kwa CHADEMA ni bora kumtosa tu.
 
Huyu Chacha Wangwe nilikuwa namwangalia kwenye TV akiwa anawatunishia misuli bungeni kwa misimamo yake. Nadhani anajitahidi kwa kiasi chake.
 
Naona shule ya HULL haijamsaidia Mh Mbowe.. sijui ndio ule msemo kila unavyosoma sana ndio unakuwa mjinga zaidi... hivi M/kiti mzima anazungumza utumbo huu... eti Kilimanjaro ina mawaziri 8 halafu anaji jibu mwenyewe kuwa naibu waziri sio waziri kwani haingii ktk kikao cha Baraza la mawaziri!

Kwa msingi huo basi hiyo hesabu ya 8 kaipata wapi? bila kujumlisha na manaibu waziri tena wengine wakiwa wabunge wa Dar Es Salaam akina Mlaki. Nadhani Quantitative Method mkuu alikuwa anaikimbia pale Hull....
 
msanii tu huyooooo
 
TAARIFA KWA UMMA

DONDOO ZA MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA KUU LA CHADEMA

Taarifa hii ni kuwajulisha wanachama wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla kuwa Baraza Kuu la CHADEMA lilifanya kikao chake katika kawaida cha kila mwaka siku ya jumanne tarehe 18 Disemba 2007 katika ukumbi wa Hoteli ya Land Mark Dar es salaam.

Ajenda katika kikao hicho zilikuwa: Kuthibitisha Muktasari wa kikao cha Baraza Kuu cha tarehe 12 Agosti 2006 na yatokanayo na muktasari huo; Taarifa ya Katibu Mkuu; Taarifa ya Fedha; Mpango Kazi na Bajeti; Kanuni za Umoja wa Madiwani; Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA mwaka 2008; Taarifa ya Ushirikiano wa Vyama na Kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti(Bara).

Zifuatazo ni dondoo za msingi kuhusu maazimio yaliyofikiwa na kikao cha Baraza Kuu kuhusu ajenda mbalimbali zilizojadiliwa:

Baraza kuu limepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya Katibu Mkuu

Taarifa hii kwa pamoja na mambo mengine imejumuisha kazi mbalimbali ambazo CHADEMA imezifanya katika mwaka 2007. Taarifa hii imehusisha pia taarifa za kurugenzi mbalimbali za makao makuu ya CHADEMA. Baraza kuu limesikitishwa na taarifa potofu za magazeti zenye kulenga kujenga taswira kwamba kuna mgogoro. Baraza kuu limepokea na kutathmini Ziara ya helikopta ya kushukuru wananchi, kuhamasisha uwajibakaji wa serikali na kujenga chama na kubaini manufaa yaliyopatikana kutokana na ziara hiyo kwa CHADEMA na kwa taifa.

Baraza kuu imejadili na kupokea taarifa ya fedha ya CHADEMA

Taarifa hii imehusisha mapato na matumizi ya CHADEMA katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Baraza kuu limetafakari gharama za ziara za helikopta na kuwianisha na ziara nyingine na kuazimia kwa kauli moja kuendelea na kutumia helikopta katika za awamu nyingine za CHADEMA kama ambavyo iliazimiwa pia na Mkutano Mkuu wa CHADEMA mwaka 2006.

Baraza Kuu limepokea, kujadili na kupitisha Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2008:

Mpango Kazi na Bajeti unajumuisha Shughuli mbalimbali ambazo zimepangwa kufanya katika mwaka 2008 pamoja na bajeti ya kutekeleza mpango huo. Mpango Kazi huo utahusisha shughuli ambazo zitafanywa pia na kurugenzi mbalimbali za chama katika masuala ya utawala, uenezi, habari, sheria, bunge, halmashauri,vijana, wanawake, wazee, rasilimali, oganizesheni, mafunzo, mahusiano ya kimataifa nk.

Baraza Kuu limepokea, kujadili na kuthibitisha Taratibu Umoja wa Madiwani wa CHADEMA

Mwongozo wa Umoja wa Madiwani wa CHADEMA(UMC) unajumuisha madhumuni, uanachama, muundo na masuala mengine muhimu yanayohusu taratibu za umoja wa madiwani wa CHADEMA umeridhiwa. Umoja huu ambao wanachama wake ni kila diwani wa CHADEMA utawaunganisha madiwani wa CHADEMA vizuri zaidi katika kutekeleza wajibu wao katika maeneo wanayowakilisha na kwa chama kwa ujumla.

Baraza kuu limepokea na kujadili taarifa ya ushirikiano wa vyama

Taarifa ya ushirikiano ilijumuisha makubaliano na kazi mbalimbali ambazo zimefanywa na ushirikiano wa vyama vya siasa vya upinzani vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR Mageuzi imepokelewa. Baraza kuu limeazimia kuwa CHADEMA iendelee na ushirikiano wa vyama kwa lengo la kudumisha demokrasia nchini, kuunganisha nguvu katika kutetea maendeleo na hatimaye upinzani kuweza kuchukua dola.

Baraza kuu limepokea, kujadili na kupitisha Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA mwaka 2008:

Ratiba ya uchaguzi mkuu wa CHADEMA imepitishwa rasmi ambapo uchaguzi utafanyika mwaka 2008. Baraza Kuu lilipitisha azimio la kutangaza ratiba ya uchaguzi(Ratiba hiyo imeambatanishwa pamoja na Taarifa hii kwa umma, maelekezo zaidi kuhusu uchaguzi huo yatatolewa baadaye).

Baraza Kuu limefanya uchaguzi na kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti(Bara).

Baraza kuu lilifanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti(Bara). Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa: Chacha Zakaya Wangwe(Mb) aliyepata kura-56. Na Said Amour Arfi(Mb) aliyepata kura:- 38 na hakuna kura ambayo iliharibika. Hivyo kwa matokeo hayo Chacha Wangwe(Mb) alitangazwa rasmi kuwa Makamu Mwenyekiti(Bara).

Taarifa hii imetolewa 20/12/2007 na:

Freeman Mbowe
Mwenyekiti Taifa
 
Kama waziri ni wa kutoka mkoa fulani hata kama kagombea ubunge mkoa mwingine haibadilishi ukweli kwamba ni mwenyeji wa Mkoa fulani.

Tusubiri labda Mbowe atatupa majina ya mawaziri hao wanane. Mikoa ya Kigoma, Lindi, Mtwara na Tanga iko nyuma sana kimaendeleo labda ni kwa kosa kuwa na mawaziri wengi wa kuipigia debe mikoa hiyo.
 
Si Mbowe tu, katika mkutano huo alianza kutaja majina watu wakawa wanamalizia. Naamini watanzania wanajua majina ya mawaziri na manaibu wao....

Mawaziri: Mramba, Prof Maghembe, Zakhia, Asha Rose(by then) nk....

Manaibu: Chami, Mwangunga, Mathayo, Rita Mlaki nk....

Endeleza orodha...

JJ
 
...who cares kama waziri katoka wapi as long ni MTZ na ana sifa za kuwa waziri sioni big deal hapo
 
msanii tu huyooooo

Nani kakwambia Mbowe na Kikwete wana uhusiano? Usanii ni sifa kuu ya JK na Lowassa (msanii aliyeusomea shahada ya kwanza Mlimani).

Mtajaribu kupulizia upupu wenu kuchochea migogoro ndani ya chama cha watu, lakini wapi! Mnafanya kazi bure kama mnadhani kusimama kwenu kunategemea kufa kwa CHADEMA!

Hiki ndicho kinachoitofautisha CCM na CHADEMA. CCM imezoea kunyonga wenye mawazo tofauti ndani ya chama, mijadala haifanyiki, wajumbe hawakosoani wala hawaruhusiwi kutofautiana. Na bado wanajidai wanaongoza kidemokrasia. Ndiyo maana CHADEMA sio CCM!
 
Si Mbowe tu, katika mkutano huo alianza kutaja majina watu wakawa wanamalizia. Naamini watanzania wanajua majina ya mawaziri na manaibu wao....

Mawaziri: Mramba, Prof Maghembe, Zakhia, Asha Rose(by then) nk....

Manaibu: Chami, Mwangunga, Mathayo, Rita Mlaki nk....

Endeleza orodha...

JJ

Huu ni ubaguzi wa dhahiri, hauna tofauti na wale manazi wa enzi za Hitler ambao walianza kuorodhesha ni vinyozi wangapi, masonara wangapi, madaktari wangapi nk ni wayahudi, na wakapitisha kwa pamoja "azimio" la kuwashughulikia. Yaliyofuata, historia ni shahidi. Kwa kweli mnatutisha sana, maana najua mkimaliza na hao mnaodai wa Kilimanjaro, mtaanza na wengine na najua wengi hatutapona katika mchakato huu wa ubaguzi. Mnatisha kuliko ukoma, nasikitika kusema.
 
Wakati wanaorodhesha majina ya wanakilimanjaro walioko CHADEMA na kuhitimisha kuwa ni chama cha wachaga hamkuona kuwa ni unazi wa Hitler. Nadhani sasa ujumbe umefika wa madhara ya kile CCM walichokuwa wakikifanyia propaganda kila walipopita. CHADEMA tulisema huo ni ubaguzi mmbaya mkaishia kusema kwamba tunajitetea! Sasa kibao kimehamia kwa CCM ndio kimeeleweka. Ama kweli commonsense is not that common. Anyway, CHADEMA si sera ya CHADEMA kubagua wachaga wala kabila lingine lolote. Yoyote anahaki ya kulitumikia taifa letu popote ili mradi ana sifa na uwezo kwa mujibu wa nafasi inayohusika. I am out on this debate for now. Naamini CCM watakuwa wamejifunza. Tuendelee na mijadala mingine tafadhali.

JJ
 
Si Mbowe tu, katika mkutano huo alianza kutaja majina watu wakawa wanamalizia. Naamini watanzania wanajua majina ya mawaziri na manaibu wao....

Mawaziri: Mramba, Prof Maghembe, Zakhia, Asha Rose(by then) nk....

Manaibu: Chami, Mwangunga, Mathayo, Rita Mlaki nk....

Endeleza orodha...

JJ

Haya sasa si unaona mkorogo huo wewe dogo Mnyika.. Shamsha Mwangunga kwao Kongwa Dodoma mnampa U-kilimanjaro mnachukua marehemu (Mbathia) mnatia kwenye hesabu... mnachukua hata walio jiuzuru ( Migiro ) ili kulazimisha hoja.

Endeleeni tu na M/kiti wenu kilaza....
 
CHADEMA:
Hii ni 2008 (karibu). Sioni mahali popote mlipoainisha "MALENGO YANAYOFIKIWA" na mipango ya kuyatekeleza na kuyafikia malengo hayo! Hasa mkielekea 2010! Au bado ni mbali mno? Au pengine ni siri ya ndani inayokwenda chini kwa chini?
Kama mnadhani bado ni mbali mno, mnajidanganya, na mtaendelea kubaki hivyo hivyo mlivyo sasa, au na kurudi nyuma zaidi
 
Wakati wanaorodhesha majina ya wanakilimanjaro walioko CHADEMA na kuhitimisha kuwa ni chama cha wachaga hamkuona kuwa ni unazi wa Hitler. Nadhani sasa ujumbe umefika wa madhara ya kile CCM walichokuwa wakikifanyia propaganda kila walipopita. CHADEMA tulisema huo ni ubaguzi mmbaya mkaishia kusema kwamba tunajitetea! Sasa kibao kimehamia kwa CCM ndio kimeeleweka. Ama kweli commonsense is not that common. Anyway, CHADEMA si sera ya CHADEMA kubagua wachaga wala kabila lingine lolote. Yoyote anahaki ya kulitumikia taifa letu popote ili mradi ana sifa na uwezo kwa mujibu wa nafasi inayohusika. I am out on this debate for now. Naamini CCM watakuwa wamejifunza. Tuendelee na mijadala mingine tafadhali.

JJ

Mnyika usiondoke. Sikia kwanza mantiki ya lalamiko langu na hofu yangu. Ni kwamba nakatishwa tamaa kuona kwamba hata ninyi ambao tuliwategemea mtuletee jambo tofauti, zuri zaidi, mnaingia kwenye mtego huohuo. Mngeweza tu kujibu hizo tuhuma vizuri tu bila kulazimika kuanza kuorodhesha majina ya watu na makabila yao kwenye CCM. Hii orodha mnayotoa inajenga hisia kwamba wote ninyi, CCM na CHADEMA mna tatizo la uchaga, data mnazotoa ni ushahidi wa kufikisha watu kwenye consensus kama hiyo. Matokeo yake hao mnaoita wachaga watasakamwa huko CCM na kwenye CHADEMA na kwingineko, na itakuwa hatari. Wakiwamaliza hao, manazi watachagua kabila lingine, na baadhi yetu tayari tunajisikia vulnerable, ndio maana tuna hofu. Naomba tu ukubali kwamba haikuwa sahihi kwa mwenyekiti wako kujibu hoja hiyo kwa kuorodhesha wachaga wa CCM, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumtusi aliyekutusi, kurekebisha kosa kwa kutumia kosa, ambayo kimantiki inafanya kosa liwe kubwa zaidi, na anayeonekana zaidi ni yule mkosaji wa mwisho. Ni hivyo tu ndugu Mnyika.
 
Haya sasa si unaona mkorogo huo wewe dogo Mnyika.. Shamsha Mwangunga kwao Kongwa Dodoma mnampa U-kilimanjaro mnachukua marehemu (Mbathia) mnatia kwenye hesabu... mnachukua hata walio jiuzuru ( Migiro ) ili kulazimisha hoja.

Endeleeni tu na M/kiti wenu kilaza....

weee! wacha kumuita M/kiti Kilaza... dont you know he is ... undertaking seriose studies at the moment? Kuchanganya Majina na mikoa mtu anayetoka..ikiwa ukilaza...anayefanya oparation ya kichwa akifikiri anafanya oparation ya Goti..utamuitaje?
 
Back
Top Bottom