CHADEMA kwa hali ilivyo sasa ndani ya CCM badilini mbinu za ushindani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kwa hali ilivyo sasa ndani ya CCM badilini mbinu za ushindani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Dec 5, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Napenda kuchukua nafasi hii kukishauri chama kikuu cha upinzani kubadili mbinu ili kulinusuru taifa na matatizo makubwa huko tuendako. Kwa hali halisi ilivyo kwa sasa CCM wamezidiwa kimbinu na kiuwezo wa kufikiri na kupanga mkakati wa kujenga imani ya wanachi kwao. Kwa mfano kwa sasa badala ya kufikiri namna ya kushirikiana na wataalamu jinsi ya kutatatua kero lukuki zinazo wakabili wananchi wao wanagombania urais wa miaka 4 ijayo utadhani wana ahadi na Mungu kuwa watakuwepo wala hawaja soma hata alama za nyakati kuwa huko tuendako hakuna tena ile hali kuwa ukishinda ndani ya CCM ndio umeshinda ubunge au urais. Ndugu zangu kwa sasa CCM ni sawa na gari lililoko kwenye mteremko halafu usikani ukakatika au nisawa na kichaa aliyeshika rungu.

  Kutokana na niliyoyaeleza ni wazi kuwa CCM ametoka kabisa kwenye mstari wa siasa za kushindana kwa hoja na utawala wa kuheshimu sheria na hapa ndipo CHADEMA itakapo kosea ikidhani inashindana na chama hiki hoja na mikakati. CHADEMA isitegeme kupatikana kwa katiba huru chini ya utawala wa CCM katiba itakayo mbana kila mtu hakuna kitu kama hicho. Ushauri wangu kwa CHADEMA inahitajika mbinu mpya mbadala wa maandamano kwa kuwa kichaa huyu anaweza kuleta madhara makubwa, hana tena chembe huruma yuko tayari hata kujeruhi ili mradi abaki madarakani ambalo ndio lengo lake lililobaki na si kuwaletea wananchi maendeleo tena. Hata wenyewe kwa wenyewe walishasema wengi woa wameacha kufikiri kwa kutumia vichwa sasa wanatumia Masaburi mtu anayefikiri kwa kutumia masaburi ni hatari sana. Chadema fanyeni mikutano nchi nzima kwa tahadhari bila ya maandamano au mbinu nyingine kumepuka kichaa huyu mwenye rungu. Pili iacheni CCM na washirika wake waendelee na kutunga katiba yao mpya iko siku watatoka madarakani kukiwa na katiba mpya au bila katiba mpya hakuna kilicho na mwanzo kisicho na mwishi.
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapo CDM = CCM C

   
 3. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Kaka kapige Mswaki kwanza kisha Toa hiyo haja iliyojaa tumboni
   
 4. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Big up Joblube, kazi kubwa kwa CDM kwa sasa ni kuendesha mikutana na kutoa mikakati ya kulinda kura pindi za chaguzi hii katiba haitakuwa na mabadiliko na hata yakiwepo bado tume ya uchaguzi ipo palepale na ndio silaha kubwa ya ushindi kwa CCM
   
 5. josam

  josam JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 1,754
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Joblbde, well say & Welldone!

  Ujumbe wako umahili.
   
Loading...