Entrepreneur
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 1,087
- 620
CDM ni chama kilichotengeneza fursa nyingi sana tangu kuanzishwa kwake. Lakini fursa nyingi zaidi zilitengenezwa kipindi cha 2005-2010 na wengi walitegemea msumari wa mwisho kwenye jeneza la CCM ungepigiliwa rasmi mwaka 2010 kwenye uchaguzi uliopita. Lakin haikuwa hivyo. CDM walipata viti ving vya ubunge (ukilinganisha na mwaka 2005) lakini CCM walipata vingi zaidi. CDM walipata kura nying za Urais (ukilinganisha na vyama vingine vya upinzan), lakini CCM walipata nying zaidi (wengine wanasema walichakachua-SI HOJA YA LEO)
Lakini kwa muktadha huo huo, kura za urais na nafasi nyingi za CCM zilikuwa zimepungua hivyo kuwalazimu kujitazama UPYA, ni kwa nini kura zao zilipungua wakaja na mkakati wa kujivua gamba (wengine wanasema ni usanii-SI HOJA YA LEO). Sasa kwa chama makini kama CDM walitakiwa kujitazama UPYA ni kwa nini kura zao hazikutosha? Je nini kifanyike ili uchaguzi ujao kura zitoshe?
Lakini hali inavyoonyesha kuna hali ya kuridhika na IDADI ya wabunge waliopatikana ilihali ukijumlisha wabunge wote wa upinzani bado hawafikii hata robo tatu ya wabunge wa CCM, na ndio maana HOJA makini zinashindwa kupita. Sasa kwa kuwa CDM inajulikana kwa kuibua HOJA nzito na MAKINI na kwa kuwa CCM wapo tayari kudandia HOJA na kuifanya yao (i.e KATIBA MPYA, POSHO n.k), mkakati mkubwa zaidi ya MAANDAMANO unahitajika pamoja Kuendelea kujenga HOJA (hata kama zitaibiwa). Niseme wazi tu kuwa, maandamano ya CDM yanawaamsha Watanzania wengi juu ya haki zao na wajibu wao hivyo ni vizuri yakaendelea. Lakini si kila suala linahitaji maandamano na matamko
Wakati umefika sasa wa kutumia njia nyingine, wakati maandamano yakiendelea kama kawaida, kwani CCM watatumia njia zote hata chafu ili kuhakikisha CDM inapotea. Hivyo ninapendekeza kuwe na timu nne za kuratibu mambo manne tofauti yafuatayo
1. Kutumia njia za Kisheria
Kwa kuwa si kila suala linahitaji maandamano, basi ni vyema timu hii ikajihusisha na maswala ya kisheria kwa wale wote wanaopindisha sheria ili kupora haki za raia na za wanasiasa wetu. Mf. Mauaji, uchaguzi batili n.k
2. Maandamano
Hii inajulikana
3. CDM ndani ya Jamii
Timu hii ijihusishe na kutatua kero ndogondogo katika jamii, kwa vile CDM ina ushawishi mkubwa wa watu. basi itakuwa rahis kuwaorganise wananchi ili washiriki katika shughuli hizi. Mf. Uwezeshaji wa vijana kiuchumi, Ujenzi wa vyoo, upakaji rangi majengo n.k.
4. Mavuno
Operation zote zilizofanywa na CDM zimezalisha wafuasi wengi sana, hivyo ni muhimu kuwa na timu ya kuratibu wafuasi hawa ili waingizwe kwenye mfumo rasmi wa chama, pamoja na kuwa na chombo chao cha uongozi katika eneo lao.
Nawasilisha