Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Kitendo cha viongozi wa NCCR, CUF, TLP na ACT kwenda kuongea na Mwenyekiti wa CCM na kurudi kwa wananchi wakiimba nyimbo zilezile zinazoimbwa na CCM ambazo wananchi wamezichoka ni tafsiri sahihi kwamba CCM haina mikakati bali yupo mtu anaongoza haya mambo kwa namna anavyopendezwa yeye.
Siasa ni mkakati ambao katika mataifa mengi uandaliwa na wanamikakati wabobezi kwa kulipwa fedha nyingi. Tumewaita viongozi hawa ikulu lakini bado ukipita mtaani uoni Kama jamii imeshtuka kwa lolote, jamii inazidi kuhubiri kwamba Hawa wamekwenda kwa maslahi binafsi na wametishwa.
Ukiwa na jamii ya hivi unachopaswa kufanya ni kuweka mazingira ya uwanja sawa wa kisiasa na kurejesha imani kwao. Leo hii Chadema wanazidi kujiimarisha mioyoni si kwa sababu wanapendwa sana bali kwa sababu wameonyesha msimamo na wananchi wamewachoka waliopo madarakani.
Hali ya sasa ni sawa na hali ya kukataliwa, ukikataliwa umekataliwa. CHADEMA wanachanga karata zao vizuri kwa kutofuata mkumbo, wameondoka KM na bado wanachanja mbuga. Hii inatufundisha kwamba hata wabaki watu wawili bado wananchi watawaamini hao
Nini CCM wafanye? Waachane na mapambano na vyama pinzani waanze mikakati ya kukiimarisha chama kikubalike mashinani. Hakuna chama chochote kitakachoimarika kwa kuchukua wapinzani wake, chama kinaimarika kwa kuwaandaa wanachama wake na kuwalisha amini. Mwanachama wanayemwona Ni asset leo akitokea Chadema kesho atageuka liability kwao, hata uchukue wabunge wote wa upinzani kwa kuwapa ajira ipo siku wakikosa ajira watakusaliti au kukushinikiza uendelee kuwaajiri.
Mkakati wa kuchukua wabunge Chadema na vyama vingine for 4 yrs now bado haujabadili upepo wa kisiasa nchini, means chama kimefeli kutambua kiwekeze wapi zaidi. Kama unamchukua Mbunge na hakuna mwananchi anayeongozana naye kuja kwenye chama chako basi tambua huyo Mbunge hana watu nyuma yake.
Dr. Bashiru na Polepole mtalaumiwa huko mbeleni kwa kukiua Chama cha Mapinduzi mkidhani mnakijenga, mtalaumiwa kwa kuwaimarisha Chadema mioyoni mwa wananchi. Chagueni sasa kuwekeza kwa wapiga kura au kuangaika na wapigiwa kura.