CHADEMA kuweni makini na Nyalandu, soon ataunga juhudi

1.wimbi la kuhamia CCM kwa wabunge kutoka 2018... Hawakuwa CHADEMA asilia?

2.CHADEMA wana machinery ya vetting? Kuepuka kuchukua 'wasio'

3.chadema asili wote wazee hapo mwanzo walikuwa CCM

4.unaweza washauri CHADEMA wakasikia? Wewe kwa CHADEMA ni kidudu, kisisimizi, takataka kabisa... CDM huwa haishauriki, unapata wapi guts hizo? Au unafikiri wanaokupa like humu ni CHADEMA? Hauijui CHADEMA acha kujipendekeza.... Kamuulize mfia chama Slaa, alichokipata , muuulize mtafuta wanachama wengi na kupeleka chama hatua ya juu bwana zitto, muulize mwanakijiji!!.. washauri wote wa CHADEMA waliokipenda waliitwa wasaliti,!!! Wewe usiye na jina halisi unakishauri kuanzia wapi?
haya sasa kikowapi sasa
 
Habari za Jumapili wakuu,

Katika hali isiyoshangaza kabisa ya mwana kurejea nyumbani (CCM) ikiwa inaendelea kwa sababu tu za kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais Magufuli, napenda kutoa rai na kukiasa CHADEMA kwamba huu ndio muda sahihi kwao kuchukua hatua stahiki dhidi ya wana CCM waliobaki ndani ya chama.

Lazaro Nyalandu kwa sasa ndiye amebaki katika safu ya juu ya CHADEMA anayetokea CCM, ni vema wanaCHADEMA mkawa makini na mtu huyu kwani muda si mrefu ataunga juhudi za Rais kwa kigezo tu anarudi kwa chama chao cha nyumbani.

Ni muda sahihi sasa kubaki na wanaCHADEMA asilia, hawa wachumia tumbo wanaohama vyama kila kukicha baada ya kukosa wanachokitafuta kuwaondoa chamani mapema.

CHADEMA mnatakiwa kumvua Nyalandu uanachama, huyu hawafai na ndani ya mwaka huu msipochukua hatua atawakimbia mchana kweupe.

Sent using Jamii Forums mobile app

ndio nikakwambia CDM hauwezi waambia kitu wakasikia
 
Puyet Babel,
Kabla ya kuandika chunguza kwanza kilichomuondoa Nyalandu ccm , pia fuatilia maisha binafsi ya Nyalandu utagundua kitu , labda kwa faida yako na wengine huyu Nyalandu ndiye Mtanzania Pekee aliyemo humu Nchini mwenye Network kubwa zaidi ya kimataifa na ana exposure ya kutosha kumtoa ushamba
?????
 
Puyet Babel,
Kabla ya kuandika chunguza kwanza kilichomuondoa Nyalandu ccm , pia fuatilia maisha binafsi ya Nyalandu utagundua kitu , labda kwa faida yako na wengine huyu Nyalandu ndiye Mtanzania Pekee aliyemo humu Nchini mwenye Network kubwa zaidi ya kimataifa na ana exposure ya kutosha kumtoa ushamba
Naimani bado unaamini Nyalandu ni mjanja sio mshamba na ndio mtanzania mwenye Network kubwa zaidi ya kimataifa.Maana nimeona maoni yako mengine kwenye uzi mwingine hayaendani na haya.
 
Naimani bado unaamini Nyalandu ni mjanja sio mshamba na ndio mtanzania mwenye Network kubwa zaidi ya kimataifa.Maana nimeona maoni yako mengine kwenye uzi mwingine hayaendani na haya.
Nyalandu hajahamia ccm kuganga njaa , ni mkakati fulani , subiri utajua
 
Siusemei moyo wa Nyalandu. Lakini Nyalandu hakuja Chadema kwa mafuriko yale ya kipindi cha uchaguzi, yeye aliacha mambo ya CCM na hiana zao baada ya ndugu yake Mnyaturu na mbunge mwenzake kupigwa risasi nyingi kama nyati wa mwituni na Wabunge wa CCM kukatazwa kwenda kumuona.

Hilo la Nyalandu ni la kiutu na takatifu sana kuweza kulinganisha na matukio ya hao "manungayembe" wengine.

Pia ukiangalia genuineness ya Nyalandu ni kuwashirikisha hadi wazazi wake, kijiji chake na jamii iliyo mzunguka kuelewa kwa nini amebadili imani yake.

Sikatai kuwa haiwezekani kugeuka msaliti! Maana wapo mpaka waanzilishi wa mageuzi wamegeuka kuwa wasaliti na hata huko ndani ya CCM wapo ambao sio wa kwao na ndio wanaofanya mipango yote miovu ya CCM na serikali wakiamka tuu wanaikuta inajulikana Chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
Muombe radhi mleta uzi!
 
Back
Top Bottom